Aksofu Kilaini amsifu DC aliyewachapa walimu

MdogoWenu

JF-Expert Member
Dec 23, 2009
555
915
MTANZANIA


Askofu msaidizi wa Jimbo Katoliki la Bukoba, Methodius Kilaini, amesifu hatua ya aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Albert Mnali, a kuwachapa viboko walimuu wa shule za msingi za Katerero na Kanazi kutokana na kushindwa kutekeleza vizuri wajibu wao.

Pongezi hizo alizitoa jana mjini hapa, wakati akijibu hoja mbalimbali zilizotolewa na wadau wa maendeleo wakati wa kongamano la kutathmini mustakabali wa maendeleo ya Kagera kwa kipindi cha miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika.

"Huyu mkuu wa Wilaya alikuwa na sababu zote za kuwachapa viboko walimu wazembena walioonekana kutotekeleza wajibu wao wa kazi vizuri, watendaji na viongozi wa serikali wasipotimiza vizuri wajibu wa kazi ndio wanaochangia ongezeko a umaskini katika Mkoa wa Kagera", alisema askofo Kilaini.

Alisema ni aibu kwa Mkoa wa Kagera kuwa miongozi mwa mikoa maskni wakati unazo rasilimali nyingi.

Alisema baadhi ya watumishi na viongozi wa serikali hawawajibiki ipaswavyo na badala yake wanaendekeza masuala ya ukiritimba wanapokuwa ofisini.

"Inashangaza kuona baadhi ya watumishi na viongozi wa Serikali wanaochangia kwa kuwawekea vikwazo wanaendelea kufanya kazi Mkoa wa Kagera", alsiema Askofu Kilaini.

Alisema uwajibikaji usiofaa na ukiritimba unaoendekezwa na baadhi ya viongozi na watumishi wa serikali ndio unaorudisha nyuma maendeleoa ya Kagera.

Alisema baadhi ya watumishi na viongozi wa serikali wanafanya kazi kwa utashi wao na wengine wanawawekea vikwazo.

Naye mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kanali mstafu, Fabian Masawe, alisema kamwe hatakubali kufanya kazi na watendaji wazembe.
 
Yuko sahihi. Nchi hii wengi wanastahili kuchapwa viboko. Sijui kwa nini walimfukuza Mnali. Alionyesha njia jinsi ya kuwafanya watumishi wawajibike. Nadhani tuanze kuchapana
 
Yuko sahihi. Nchi hii wengi wanastahili kuchapwa viboko. Sijui kwa nini walimfukuza Mnali. Alionyesha njia jinsi ya kuwafanya watumishi wawajibike. Nadhani tuanze kuchapana
Viboko! je watumishi wakivaa kaptula ya jinsi kwa ndani,viboko vitapenya?
 
Sio sahii, kwanini walimu tu dnio wanachapwa? basi wangechapwa wote hadi JK maana na yeye hatulii nchini kutatua matatizo yetu kila siku anasafiri nje ya nchi
 
Viboko! je watumishi wakivaa kaptula ya jinsi kwa ndani,viboko vitapenya?


Hukumbuki adhabu za kikoloni mkuu. Watu walichapwa hadi tukawa na reli toka Dr hadi Mwanza na Kigoma. Kumbuka wakati huo kulikuwa hakuna mitambo ya kunyanyua mataruma lakini viboko viliwafanya watu wakatandika reli. Kama amevaa jeans atagakuliwa na kuvuliwa kisha anatandikwa bakora barabara.
 
inawezekana yuko sahii lakini kama ni kuchapana viboko je, kiongozi wa juu kabisa akifanya kosa nani atamchapa kiboko kama kuchapa ni njia sahii. Tunaangalia kutokuwajibika kwao lakini tunasahaukujiulioza ni kwa nini Watanzania hawataki uwajibikaji.

Walimu, wahudumu wa afya ni baadhi ya watumishi ambao wanalipwa kidogo sana katikati ya watu wanaotumbua utajiri wa nchi hii. Kumbuka analipwa 150,000 wakati kuna mbunge akikaa siku moja kwenye kikao na pengine bila kufatilia mijadalaaamua kusinzia analipwa 70,000 kwa wakati ule kitendo cha mkuu wa wilaya kilipotokea.

Kuna watumishi wa sekta nyingine serikali wanapokezana safari za nje na kwa siku wanalipwa wanalipwa zaidi ya USD500. Na swala hili la mkuu wa wilaya lilitokea wakati rais wetu anatembea dunia mithili ya Vasco Da Gama na delegation kubwa kuliko kinachoenda kuombwa. Kwa mtindo huu wa matanuzi mnategemea asiyekuwa sehemu ya matanuzi atahamasika na kufanya kazi ipasavyo wakati au keso atakula nini, akiumwa yeye au wa kwake karibu atafanya nini. Huku ni kujidanganya.

Kama tunataka watu wafuate tunachohubiri na kuelekeza tunatakiwa viongozi waonyshe mfano. Lakini kama viongozi na sehemu ya uchafu, rushwa, uporaji wa mali ya umma kwa njia mbalimbali hata kwa safari na warsha zisizoisha tusitegemee uwajibikaji kwa watumishi wa kada ya chini na kati. Kama viongozi wa juu hawawezi kuwajibish
 
yule mzee mnali namkubali ni mchapakazi huwa hakai ofisini kama hawa wa sasa,na huwa pia anajichanganya na wananchi bila woga ni muongeaji mzuri hata jokes nilimpenda uwajibikaji wake alipokuwa mkuu wa wilaya moja mwanza
 
Huyu Mnali Alijaribu!! Ila kwa Hali Ilivyo sasa Tunahitaji akina Mnali Wengi zaidi!!
 
Bado Kiliani anaamini kuwa Kikwete ni chaguo la mungu? kama jibu hapana, wananchi wanaweza kumchapa viboko kwa kudanganya umma na kusababisha hasara kubwa - uchumi mbovu?
 
Huyu mkuu wa Wilaya alikuwa na sababu zote za kuwachapa viboko walimu wazembena walioonekana kutotekeleza wajibu wao wa kazi vizuri, watendaji na viongozi wa serikali wasipotimiza vizuri wajibu wa kazi ndio wanaochangia ongezeko a umaskini katika Mkoa wa Kagera", alisema askofo Kilaini.

mkisoma hii habari vizuri hajamsifu bali kasema alikuwa na sababu zake kwa kukerwa na uzembe
mtoa mada jaribu kuwa makini usiharibu maana.
 
Mbona Askofu Kilaini hakumtetea wakati DC Mnali alipowajibishwa hizi ni sawa na sifa anazopewa marehemu.
 
Yuko sahihi. Nchi hii wengi wanastahili kuchapwa viboko. Sijui kwa nini walimfukuza Mnali. Alionyesha njia jinsi ya kuwafanya watumishi wawajibike. Nadhani tuanze kuchapana
kweli kabisa mimi naanza na huyu kijana wangu apa ofsini

 
Bado Kiliani anaamini kuwa Kikwete ni chaguo la mungu? kama jibu hapana, wananchi wanaweza kumchapa viboko kwa kudanganya umma na kusababisha hasara kubwa - uchumi mbovu?
Ni kweli bado Kikwete ni Chaguo la Mungu! Wala Kilani hakukosea. Kikwete ni chaguo la Mungu ili watanzania mjifunze!
 
Unafiki unamsumbua, nadhani viboko hivyo kilaini angevianzia kuwachapa maaskofu/mapadiri wanaodhalilisha watoto.
 
Back
Top Bottom