Akirudi kazini mpe dk 15 apumzike!!

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,956
22,144
Wanaume hupenda kuwa wenyewe muda fulani (kukimbilia pangoni) hasa akiwa amerudi nyumbani kutoka kazini au akiwa anatatizika na jambo lolote.
Hivyo basi inawezekana wewe kama mwanamke ndani ya ndoa umezoea mume akirudi kutoka kazini unamkaribisha home kwa kumpiga maswali na kuanza kumueleza kila aina ya matatizo na karaha ambazo zimetokea siku hiyo bila kumpa hata muda wa yeye kupumzika kidogo.


Sina maana kwamba mumeo akirudi nyumbani ule jiwe bila kumpokea au kumuuliza kazi ilikuwaje, nazungumzia suala la kutompa muda angalau dakika 15 kupumzika kabla hujaanza kutoa maswali yako na matatizo yako.

Pia naamini dunia ya sasa wote wanawake na wanaume tunafanya kazi iwe ofisini au shambani hata hivyo tukifika nyumbani kila mmoja hujitahidi kumweleza mwenzake nini kimeendelea au kupeana taarifa mbalimbali za familia ukweli ni kwamba bado mwanaume huhitaji dakika kama 15 kabla ya kujiunga na familia.

Kumbana maswali na kumwambia matatizo na shida tangu anaingia mlangoni si jambo zuri sana kwa mwanaume kwani hujisikia ainaishi na mama yake na si mke wake maana mama yake alizoea kumbana maswali tangu anaingia nyumbani kutoka shule.
Kama angekuwa anataka kuishi na mama yake basi asingekuoa wewe bali amekuoa wewe kwa sababu wewe ni tofauti na mama yake.

Baada ya kuchoshwa na kazi, na boss, au wateja au foleni za magari njiani anapowahi nyumbani anachohitaji akifika nyumbani ni busu na hugs kutoka kwa mke wake then aoge na kupumzika kidogo kama dakika 15 hivi ndipo atakuwa tayari kujibu maswali ya mkewe na kuendelea na story zingine pia.

Mpe muda wa kurelax akishafika nyumbani kwani kumbana maswali punde tu anaingia nyumbani kunaweza kusababisha yeye kuchelewa home kwani hujisikia ni usumbufu.
Akishakuwa tayari ameridhikana muda wake kuwa kwenye hilo cave unaweza kuona anaanza kuzunguza mwenyewe then anza kumpa hayo maswali yako.

Pia akigundua wewe ni msumbufu, hata siku ukiwa na point za maana anaweza kupuuzia maana umezoea kuchonga sana akiingia tu mlangoni hata kabla hajafika chumbani.

Ubarikiwe!​
 
mi huwa naboreka pale ninapotoka kazini njaa inaniuma badala ya kupewa chakula na pokelewa na busu na manjonjo kibao wakati hayo yote sio hitaji kwangu kwa muda ule
 
haaah haah mkuu umenena vema.
Haya wadada mpooo???
Mjuu kupuuzia haya ndio kukaribisha nyumba ndogo tunazozipiga vita kila uchao.
 
What about a woman, naye akirudi toka shamba/Sokoni anapaswa kupewa muda gani kabla hujaanza kumhoji kuwa kwanini hakuna chakula ndani au shati langu la buluu kwanini halijanyooshwa?
 
mi huwa naboreka pale ninapotoka kazini njaa inaniuma badala ya kupewa chakula na pokelewa na busu na manjonjo kibao wakati hayo yote sio hitaji kwangu kwa muda ule

We naye si ushukuru hata hayo wenzio wanaambulia patupu kabisa....
 
Back
Top Bottom