Sikonge
JF-Expert Member
- Jan 19, 2008
- 11,550
- 6,062
So far, inaonekana hakuna anaejua.
Akaja Sikonge, anatueleza ngoma za Wasukuma, tena za enzi hizo. Wakati tunataka kujua kinachoendelea sasa hivi Uyui, Tabora, ambacho local leaders wanasema kinasababisha huku kujamiana jamiana ovyo. Sikonge alichoeleza ni kama ndoa za hiari hiari hivi, hatuelezwi hizo ngono ya ovyo ovyo zinavyotokea. Anasema hiyo ilikuwa ni OLD school. Unaweza kukuta siku hizi hawa New Generation wanamalizana na mtoto hapo hapo. Kwa hiyo nae hajui.
Kuhani, yaani ukisoma maelezo yangu unaona kuwa SIJUI KITU? Duu mu wee una kipaji cha kubisha ili tu UBISHE. Naona hata nikuelezee na kukupa VIDEO, bado utasema kuwa hiyo ni sehemu moja tu na kuwa sikuona Tabora nzima.
Kama uliuliza kwa dhati basi angalia maelezo ya Bubu kutakakusema ya mwanzo. Ile habari imechanganywa na mwandishi wa habari hata hakufanya kazi ya ziada kuuliza na kupata ukweli halisi. Nilivyokuwa mdogo na mimi nilisikia hivyo hivyo. Nafikiri Wasukuma huwa hawataki kusema kinachofanyika huko. Sijui kama ni mwiko au lahh. Siku moja tuliamua kuwafuata ili tuangalia Porno la bure. Tulikaa hadi mtu wa mwisho akaondoka na mabinti almost yuko kwao na hakuna kilichofanyika. Ilikuwa chagulaga moja baada ya nyingine. Tukarudia mara ya pili story ni zile zile. Tukajua hii ilikuwa HABARI feki na hatukuenda tena kuangalia wanavyo chaguana.
Simtetei Kikwete. Ila kwa hili naona yuko sawa. Kama nilivyosema ni kuwa HAMNA NGOMA YA CHAGULAGA. Ila ipo ngoma ya PUVA. hata bubu kasema hilo. Hamna ya vijana kusimama na kuchagua ila humkimbiza msichana na wakimkamata humzunguka kundi na mmoja kuchaguliwa. Akichaguliwa, wengine bado husubiri na wao wapewa nafasi yao.
Inavyoonekana wanaopata Mimba wengi wao ni wanafunzi wa Secondary. Kama ni hivyo, mtu hapa anataka KUKIMBIA MAJUKUMU. Kama watoto wako Secondary, na wanapata Mimba, watia mimba ni waalimu, mi-Sugardaddy, vijana wenye senti zao, wanafunzi wenzao nk. Nafikiri muda wa kwenda ngomani unakuwa umepungua. Somo inabidi lianzishwe Secondary ili kuzuia hivi vitendo. Mliona kwenye Disco la watoto Tabora, hadi watoto wanauziwa Pombe. Na kama si janga hilo hakuna hata mmoja leo angelisema. Mkoa wa tabora kuna Uzembe wa aina nyingi sana. Viongozi wanatafuta sababu za KIJINGA ili kupeleka lawama sehemu nyingine. Kwa nini wasiseme POMBE pia zinasababisha? Disco pia linasababisha? Au na wao wana hisa huko?
Kuhani, kama una akili kweli (nafikir unazo) owanisha matukio hayo na ukumbuke kuwa Tabora ni mkoa masikini sana. Sasa ukichanganya vyote vitatu utaona kama kweli CHAGULAGA ndiyo mleta mimba.