Akina mama kwa nn mpo hivi?

Ni kweli wakinamama sometimes hawapendani lakini hili la daladala nakataa, utakuta mtu anaona kabisa gari imejaa lakini anapanda hivyo hivyo na mtoto wake/watoto wake. Kunyanyuka siwezi kwani na mimi nakua nimechoka tena nimechoka hasa cha kufanya naweza mpokea mtoto kama ni msafi maana wengine sio wasafi kabisa anapanda na mtoto ananuka mikojo + mchafu hadi kero huyu atanisamehe mwingine anazaa kama anatenda unakuta wa kwanza anamiaka 3, wapili 2, watatu kambeba mgongoni na anapanda daladala lililojaa aku mwenzangu kuna mambo mengine mwatuonea wakinamama kwani wanajitakia wenyewe

Daa yani, kwa hili jamani ni hata ukiona kwene daladala watu hawakwambii mlete mtoto tukusaidie, usilalamike.
Imagine ndo asubuhi umejipandia zako daladala unaenda kwene pilika pilika, mtu mtoto, mchafu, mikojo, kanga aliofunikwa nayo daaaa,

Jamani naomba msamaha tu.
Lakini kama mtoto ni msafi, wala sekunde haipiti, utasikia MLETE MTOTO TUKUSAIDIE.
 
Kwa nn akina mama mpo hivi?
Unakuta kwenye daladala mama amepanda ana mtoto mchanga seat za karibu kuna akina mama utakuta wameuchunaaaaaaa kumwachia seat au kumpokea mtoto kimyaaaaa mpaka sisi wababa nyumba tusimame kumpisha akina mama kwa nn mna roho mbaya jamani??
Hata kwa wajawazito huwa mnafanya hivi hivi. Kwa nn jamani?
Hata bar ukienda na mwanamke tu kosa huduma unapata mbovu kwa nn akina mama hivyo?

Nahisi wanawake tuna hulka ya kutopendana sisi kwa sisi,
Mi nakumbuka hata shule bwana, msichana mwenzio anaweza asikusaidie kitu anachokifahamu, lakini akamsaidia mvulana.
Akakunyima material, akampa mvulani.

Hata kumweleza mwalimu wa kike tatizo inakuwa ngumu kidogo kuliko mwalimu wa kiume.
Duu Maofisini sasa, mwanaume anaweza kupata huduma nzuri kwa haraka kuliko mwanamke.

Duuu labda ni hulka ya kike.
 
Kama gari limejaa naye anapanda ina maana kaamua kusimama, sasa kwa nini apishwe? ila incase of emergency yan kazidiwa watu wanajua huyu jaman anawahi hosp watampisha.
 
Back
Top Bottom