Grader
JF-Expert Member
- Feb 23, 2009
- 445
- 64
'Wanaume Sura Mbaya Hutoa Mbegu Nyingi Za Kiume Wakati wa Kujamiiana'
Wanaume wasio na mvuto hutoa mbegu nyingi sana za kiume wakati wa kujamiiana kulinganisha na wanaume wenye mvuto Monday, July 13, 2009 5:09 AM
Wanawake wanaotaka kupata mimba haraka inawabidi watafute wanaume wenye sura mbaya kwani matokeo ya utafiti wa wanasayansi umeonyesha kuwa wanaume wasio na mvuto hutoa mbegu nyingi sana za kiume wakati wa kujamiiana kulinganisha na wanaume wenye mvuto.
Wanasayansi wamegundua kwamba wanaume wenye sura zenye mvuto hutoa kiwango kidogo cha mbegu za kiume wakati wa kujamiiana.
Wanasayansi wanafikiria kuwa wanaume wenye sura zenye mvuto kibailojia huwa wanazihifadhi baadhi ya mbegu zao za kiume katika kila tendo la kujamiiana ili waweze kupata nafasi ya kuwatia mimba wanawake wengi zaidi.
Kwa upande wa wanaume ambao hawana mvuto wowote kwa wanawake hujua fika kwamba ni wanawake wachache watakaowakubalia kulala nao kwahiyo wanapopata nafasi humwaga mbegu zao zote za kiume walizonazo wakijua bahati inaweza isirudi mara mbili.
Utafiti huo ulifanywa na wanasayansi katika vyuo vikuu vya Oxford na University College London vyote vya Uingereza.
Wanasayansi hao walisema kuwa utafiti wao umethibitishwa katika majaribio waliyofanyiwa kuku na samaki na kwamba matokeo yatakuwa ni sawa hata kwa binadamu.
Ripoti iliyotolewa kwenye tovuti ya chuo kikuu cha UCL ilisema kuwa "Jinsi mwanaume anavyozidi kuwa na mvuto ndivyo ambavyo wanawake wengi wanavyopenda kujamiiana naye, hii inamaanisha inambidi atoe mbegu chache za kiume kwa kila mwanamke atakayekutana naye".
"Ingawa kwa kufanya hivyo hupunguza uwezo wake wa kuzalisha katika kila tendo la kujamiiana lakini huwafanya wawe na watoto wengi kwa ujumla".
"Wanaume wasio na mvuto hufanikiwa kupata wapenzi wachache ambao huwathamini sana na kwa kutoa mbegu zao zote za kiume katika kila tendo la ndoa huongeza uwezekano wao wa kupata watoto".
Utafiti huo ulisema kuwa kutokana na sababu hizo, kwa makadirio wanaume wenye mvuto huwa na uwezo mdogo wa kuzalisha kulinganisha na wanaume wasio na mvuto.