Akina dada/mama hamtosheki au hamjiamini?

Kyachakiche

JF-Expert Member
Feb 16, 2009
983
207
Nimekuwa mara nyingi nikijiuliza ni kwanini Wanawake wamekuwa mstari wa mbele katika kuanzisha vyama visivyo vya kiserikali(NGOs), Vikundi mbalimbali vya maendeleo, harakati,..nk kuliko wanaume. Kwa mfano, katika gazeti la Tanzania Daima toleo la leo No 1917 Ukurasa wa 3, kuna habari kuwa "Wanawake kuanzisha chama cha siasa". Ndani ya habari hii kumeelezwa kuwa, kati ya Vyama vya siasa 19 vilivyoko katika orodha ya Msajili wa Vyama vya Siasa, hakuna hata kimoja kinacho ongozwa na mwanamke. Kwa maana nyingine hii ni moja ya sababu yao kuu kutaka kuanzisha chama cha siasa.
Naomba kujua je, utitiri wa vyombo vyote hivi bado haujawatosha au ni hulka yao ya kupenda mambo mengi? Hebu cheki mifano hii michache! TAMWA, TAWLA, UWT,WAMA,WAWATA, MEWATA...nk!
 
Back
Top Bottom