Akimtimua mkewe atakuwa na makosa?

kaka talaka haitolewi kanisani........talaka inahusu ndoa ya aina yeyote......umeoa wewe????
Kama walifunga kanisani lazima magomvi yao yote yapelekwe huko na sio mahakama za kiraia. mahakamani talaka utapewa ila kumbuka Mungu hataki talaka. suala la kutoachana kwa wanandoa ni suala la Kimungu ktk sheria asili(natural law). kumbe hata kama talaka imetolewa kokote, si halali na ni dhambi mbele ya Mungu.
 
Mkuu unahoji yote haya kwakua hujapata misukosuko imara ya ndoa, mwanamke anaefanya umalaya elihali ana ndoa ni hatar sana. Kiburi na jeuri yake ambavyo ni zao au product ya umalaya wake huivuruga sana nyumba.

Tambua wazi kwa waliooa,maendleo hupatikana tu endapo mtafikiri pamoja, sasa hamuelewani kuna nini hapo.? Dhambi hutendeka na huwa twapata nafasi ya kutubu but siyo kwakubeba mizigo mizito eti kisa ukristo.
sio agizo langu kutoachana, ni agizo la Mungu. mbele ya Mungu hata ndoa iwe na migogoro kiasi gani hamna talaka. sio mimi nisemaye ni Yesu. ukimpa talaka ukaoa mwingine ujue huo ni uzinzi. ila amani ikitoweka sana kanisa Katoliki limeruhusu watengane kwa muda bila kuoa au kuolewa! kumbe dhana ya kutubu huku umemwacha mkeo ili uoe mwingine sio sawa mbele za Muumba.
 
Jamaa amefunga ndoa,ndoa ina miezi kadhaa hata mwaka bado ikafika kipindi wife akapata ujauzito.
Alipoenda kuanza clinic,vipimo vikaonesha ana maambukizi. Clinic wakamuambia aje na mumewe wapime wote, mume akapima hana hayo matatizo yupo salama.

Je jamaa afanyeje, ndoa na iwe basi au? Na pia mke ndo jeuri, kiburi, dharau na kejeli zimezidi mno mpaka nyumba inakuwa siyo sehemu ya kuishi mshikaji tena.

Je mshikaji akimtimua huyo wife atakuwa kakosea?

Huyo jamaa atakuwa na blood group O+, thats why kampa ujauzito wife wake mwenye HIV lakini yeye hana..
 
nani alikwambia ndoa ya kikristo haivunjiki brother......kuna mtu aliumbwa kuishi akiteseka milele? kanisa au msikiti ni wakala serikali, na ndoa inavunjwa na serikali.....acha fikra dhoofu...
Sababu itakayovunja ndoa ya kikristo ni "uzinzi" tuu
 
Ndoa za Kikristo hazina talaka! fuatilia ujue, kaulize uambiwe. Yesu alikataa talaka kabisa!
Isipokua sababu ni uzinzi,ngoja nikufundishe Mathayo 5:31-32 hasa huo mstari wa 32 anasema isipokua kwa habari ya uasherati unapaswa kumpa talaka na hapo Mungu hana hatia na wewe,Cha msingi mtu ukiisoma biblia jaribu kumaliza mstari wote upate uhalisia
 
Sababu itakayovunja ndoa ya kikristo ni "uzinzi" tuu
hata uzinzi si sababu ya kuvunja ndoa ya Kikristo. injili ya Mathayo 19 inayosema hivyo ilimaanisha ndoa za watu waliooana wakati ni ndugu ndiyo zaweza kuvunjika. hata hivyo huko si kuvunjika ndoa kwani tangu mwanzo wake muungano huo wa kindugu ulikuwa batili. no talaka kwa Wakristo! waulizeni viongozi wenu wa dini
 
Samahani,umesoma vizuri mkuu?Hapo hapajaongelewa ndugu hebu kaa vizuri muulize tena Yesu alimaanisha nn alipokuwa anawaambia mafarisayo hajagusia undugu hapo,Yaani kwa msisitizo uasherati/uzinzi kwa mkristo yoyote mahali popote hamna ndoa tena hapo tatizo ni viongozi wa dini wanazani wanayo hekima zaidi kuliko Yesu eti wakisema kweli wataleta mifarakano
 
ni hivi ndugu: Biblia iliandikwa kwa lugha za Kiebrania, Kiyunani kidogo na Kigirigi. ikaja kutafsiriwa kwa Kilatini kisha Kiingereza na baadae Kiswahili na hata kwa vilugha. Waebrania walitumia neno 'porneia' kumaanisha ndoa ambazo zinaweza kuvunjwa. wenzetu Waingereza wameziita 'illicit marriage' sisi kwa Kiswahili hatuna neno moja hivyo tukaita uzinzi. kumbe porneia ilinaanisha ndoa za kindugu ndizo zinafunguliwa kwani tangu mwanzo hizo si ndoa. kwa wale waliofunga ndoa kihalali hamna talaka. kama vp nitumie namba yako nikujuze zaidi
 
KJV yenye maana ya karibu na kiebrania/kiyunani inayasema hayo kuwa ni sexual immorality na "commit adultery" je yamekosewa?
 
walifunga ndoa ya namna gani? kama ni Wakristo hamna talaka!

Acha utoto ukristo ndiyo unakaa na mke au wewe ndiyo unakaa na mke? Watu wengi wamekufa kwa ujinga wa kung'ang'ani ndoa wakidhani wanamtii Mungu kumbe wanaangamia kwa ujinga wao dini haikuja kukufanya uishi kwa mateso wala majuto ila wajinga wengi wamedanganywa hivyo na wanapukutika kila siku.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom