...akililia wembe mpe...!

Mbu

JF-Expert Member
Jan 11, 2007
12,753
7,844
...baada ya miaka kadhaa ughaibuni na mkewe mkubwa, mshkaji alikwenda kuoa bongo kinyemela bila mkewe kujua.
Ili kuuziba nyufa, mheshimiwa aliamua kufa na kupona, iwe isiwe bi mdogo huyo, (ambaye tayari weshajaaliwa kachanga kamoja), naye aje kuishi ughaibuni.

...kimbembe kikabakia kwenye maombi ya Viza...
Wenye nchi yao hawakukubali mpaka ithibitike mtoto kweli ni halali ya huyo baba.
Majuzi majibu ya DNA yametoka, mtoto sio wa huyo baba.
Mbaya zaidi, wenye nchi yao wamempa Viza Huyo bi mdogo aje amjoin mheshimiwa ughaibuni, ...bila hicho kichanga!

...Namsikitikia jamaa hela alizotumia kuanzia kwenye kulea mimba, gharama za labour, kulea kichanga, maombi ya viza, gharama za solicitors, gharama za maombi ya settlement viza, (sasa ni tshs 1m/= na ushee),... na hicho kipigo kitakatifu...

Yaani sijui nianzie wapi kumpa ushauri!
 
To hell with all ze costs...haendi mtu Ughaibuni, hata kama kaogaje au amepata hiyo Viza!...Cheating about a child is full intolerable...Wa nini mtu wa hivyo?

Bahati si yake...We Chapa zako malapa Ulaya, mwache huyo mzinzi aendelee kunyonyoa nyau Bongo!

Alaaa!
 
Umpe pole ya nini???
si amejitakia mwenyewe, yeye kama ana mke wake kwa nini asitulie. Mwache aone uchungu. Tena mwambie jamaa yako kwamba hata mkewe atamwacha pindi akisikia hilo.

Kila la heri.
 
Mbona makubwa!!! Mtendwa katendwa, yeye alivyokuwa anaoa kinyemela bila mke wake kujua sasa hayo ndio malipo yake.

Anyway huyo mtu wala asijaribu kumchukua huyo binti, maana tayari mdada sio mwaminifu kambambikia mtoto. Inaelekea huyu mdada shida yake ilikuwa ni kwenda ughaibuni wala hakumpenda huyo jamaa. Hivyo akimpeleka tu ughaibuni atakuja kuachwa.
 
Duu,kwakweli Malipo hapa hapa Duniani,Mwambie Mungu anampenda amemuonyesha mapema,hizo gharama asamehe tu.
 
Hivi kumbe mtu kuitwa mtoto wa fulani ni lazima biological proof? Vipi kuhusu watoto adopted? Au inakuwa vipi kama mhusika alikubali kuoa mke mwenye mtoto tayari, ina maana mtoto huyo hutengwa? Au wale ambao wake zao hupandikizwa mimba kwa mbegu za mwanamke na/au mwanaume asiye mumewe, ina maana watoto wa zao hilo huwa hawapati hizo viza? Kuna watu kadhaa ninaowafahamu ambao nasikiaga huwa hawana uwezo wa kuzaa, lakini waliendaga South Africa na Ufaransa wakarudi na watoto wanaoitwa wa kwao, hapo DNA najua itagoma, sasa biological proof ya ubaba/umama inakuwaje, na ina maana watoto hao huko ughaibuni wanabaguliwa?

Naomba kuelimishwa
 
Hivi kweli walitumia vigezo gani hapo Ubalozini,kwanini walitaka uhalali wa mtoto na hakika alikuwa na birthcertificate,au mwenyewe alikuwa na wasiwasi ??
 
Nimeona mara nyingi siku hizi kama ukitaka kumwalika mtu mwenye mtoto (hasa USA) ofisi ya uhamiaji kupitia ubalozini wanaomba DNA proof.
 
To hell with all ze costs...haendi mtu Ughaibuni, hata kama kaogaje au amepata hiyo Viza!...Cheating about a child is full intolerable...Wa nini mtu wa hivyo?

Bahati si yake...We Chapa zako malapa Ulaya, mwache huyo mzinzi aendelee kunyonyoa nyau Bongo!

Alaaa!

Hapo umekosea mzinzi si mwanamke peke yake, mwanaume ndio mzinzi mkubwa maana yeye tayari ana ndoa.............kilichomuwasha nini hadi kwenda kutafuta mwanamke mwingine?
 
MWISHO WA UBAYA NI AIBU!
Jamaa si alitaka kumfanyia mkewe ubaya kwa kwenda kinyemela kuoa? Sasa kiko wapi?
Mbu unataka kumshauri vipi zaidi ya kumwambia ukweli?
 
...baada ya miaka kadhaa ughaibuni na mkewe mkubwa, mshkaji alikwenda kuoa bongo kinyemela bila mkewe kujua.
Ili kuuziba nyufa, mheshimiwa aliamua kufa na kupona, iwe isiwe bi mdogo huyo, (ambaye tayari weshajaaliwa kachanga kamoja), naye aje kuishi ughaibuni.

...kimbembe kikabakia kwenye maombi ya Viza...
Wenye nchi yao hawakukubali mpaka ithibitike mtoto kweli ni halali ya huyo baba.
Majuzi majibu ya DNA yametoka, mtoto sio wa huyo baba.
Mbaya zaidi, wenye nchi yao wamempa Viza Huyo bi mdogo aje amjoin mheshimiwa ughaibuni, ...bila hicho kichanga!

...Namsikitikia jamaa hela alizotumia kuanzia kwenye kulea mimba, gharama za labour, kulea kichanga, maombi ya viza, gharama za solicitors, gharama za maombi ya settlement viza, (sasa ni tshs 1m/= na ushee),... na hicho kipigo kitakatifu...

Yaani sijui nianzie wapi kumpa ushauri!

DUH! Hii Kali! mama pamoja na kujua kuna uwezekano wa kwenda majuu hakuacha kujirusha viwanja vya ugenini. Hata majuu kwa makubaliano maalum watu wana mke zaidi ya mmoja hasa waarabu na wasomali lakini mke wa pili anakuwa anajulikana kwa ndugu wa karibu kabisa na mara nyingi hata kwa mke mkubwa.
 
baada ya kisa mkasa kuna kitabu kinaitwa hivyo kimetungwa na emmanuel makaidi sijui viko wapi hivi vitabu, hiyo ni laana ya mke wandugu, jamaa alijiona kijogoo akakutana na tetea ana mayai tayari
 
To hell with all ze costs...haendi mtu Ughaibuni, hata kama kaogaje au amepata hiyo Viza!...Cheating about a child is full intolerable...Wa nini mtu wa hivyo?

Bahati si yake...We Chapa zako malapa Ulaya, mwache huyo mzinzi aendelee kunyonyoa nyau Bongo!

Alaaa!

Duh,nimecheka sana mzee jinsi ulivyo-react.Sipati picha....what if ingekutokea wewe.......

Well,pole kwa aliyefikwa.Mpumbavu hujifunza kwa makosa yake.Jifunze. The rest is history. Badili uelekeo wa upepo haraka sana by 180 degrees!
 
Malipo ni hapa hapa duniani, kesho akhera hesabu tu! Serves him right! naye huyo mwanadada kakosa na majuu pia. hamna cha gharama hapo, amelipia uzinzi wake! asiwe ameambukizwa ngoma basi, hiyo gharama itakuwa child play!

Mbu...u dont need to feel sorry for your buddy unless u were part of the plan! hebu twambie how do u feature in this?
 
To hell with all ze costs...haendi mtu Ughaibuni, hata kama kaogaje au amepata hiyo Viza!...Cheating about a child is full intolerable...Wa nini mtu wa hivyo?

Bahati si yake...We Chapa zako malapa Ulaya, mwache huyo mzinzi aendelee kunyonyoa nyau Bongo!

Alaaa!

...ha ha haaaaa! duuuuh,....
unajua hawa waingereza saa nyingine hata mimi nawashangaa...
Wamempa viza huyo binti sijui aje ulaya kum stress zaidi mshkaji???

Kama wewe ulivyo react, naogopea jamaa ataua mrembo akija huku,...murder case inanukia hapa! :D:D:D
 
Umpe pole ya nini???
si amejitakia mwenyewe, yeye kama ana mke wake kwa nini asitulie. Mwache aone uchungu. Tena mwambie jamaa yako kwamba hata mkewe atamwacha pindi akisikia hilo.

Kila la heri.

mswalie mtume bana,
hujafa hujaumbika...mbona unawaombea mabaya wenzio? yaani mke mkubwa nae amuache kisa DNA imekataa? ha ha haaa...
Jamaa anatakiwa kufarijiwa huyu, naogopea asije kuwa chizi!
...mpaka sasa kadata! binafsi nampiga chenga kwani nishazimaliza kila sentensi za pole!
 
Mbona makubwa!!! Mtendwa katendwa, yeye alivyokuwa anaoa kinyemela bila mke wake kujua sasa hayo ndio malipo yake.

...aaah, si unajua tena...ruksa kuoa wanne, na kumuarifu mke ni sunna tu!

...Anyway huyo mtu wala asijaribu kumchukua huyo binti, maana tayari mdada sio mwaminifu kambambikia mtoto. Inaelekea huyu mdada shida yake ilikuwa ni kwenda ughaibuni wala hakumpenda huyo jamaa. Hivyo akimpeleka tu ughaibuni atakuja kuachwa.

...hata asipomchukua yeye, Viza keshapata! ...Qatar airways ticket bei chee tu...
 
Back
Top Bottom