Akili . . . . . !!!!

Eiyer

JF-Expert Member
Apr 17, 2011
28,258
20,709
Jamani,mimi naamini kujifunza hakukuishia darasani,na sipendi kufanya mambo kimazoea.Kuna hii kitu nimekua nikisikia tangu mdogo,AKILI.Je ni nini?Je ni ufahamu?Inapimwaje?Shule kwa mfano,yule anaefaulu masomo huonekana ana "akili" lakini ukija mtaani unamkuta ni mlevi,mnyanyasaji,mkatili,mpenda fujo n.k,je huyu kweli ana akili?Au ubongo ni akili?Nijuavyo mimi ubongo ni kifaa anachotumia mtu kufikiri.Sasa akili iko wapi?Inakaa mwilini?Je ni eneo lipi inakaa?Au ufahamu ndio akili,Kama ni ndio ufaham ni akili?Hebu fungukeni mtusaidie sisi wenye kutanzwa na hii kitu!
 
Duniani kuna watu wa aina nyingi tusema dokta,injia,profesa n.k kuna vitu wanafanya kwa kweli unachelea kusema hawana au hana akili. Hata nami nashangaa pia nadhani wataalamu watakuja kwa undani kufafanua akili na ilipo ni kweli kichwani au sehemu nyingine ya mwili?
 
kwa ufahamu wangu akili ni jina analopewa m2 mwenye uwezo mkubwa wa kufikili na wala si kitu au kiungo cha mwili na hupimwa kwa kuangalia IQ(Intelligence Quotient) ya mtu na si darasan tu bali katika mazingira yanayomzunguka
naomba kuwasilisha wakuu
 
Jamani,mimi naamini kujifunza hakukuishia darasani,na sipendi kufanya mambo kimazoea.Kuna hii kitu nimekua nikisikia tangu mdogo,AKILI.Je ni nini?Je ni ufahamu?Inapimwaje?Shule kwa mfano,yule anaefaulu masomo huonekana ana "akili" lakini ukija mtaani unamkuta ni mlevi,mnyanyasaji,mkatili,mpenda fujo n.k,je huyu kweli ana akili?Au ubongo ni akili?Nijuavyo mimi ubongo ni kifaa anachotumia mtu kufikiri.Sasa akili iko wapi?Inakaa mwilini?Je ni eneo lipi inakaa?Au ufahamu ndio akili,Kama ni ndio ufaham ni akili?Hebu fungukeni mtusaidie sisi wenye kutanzwa na hii kitu!

mkuu eiyer,
akili ni ule uelewa,ufahamu na uwezo wa mtu kutafakari na kutumia maarifa aliyonayo kutoa suluhu ya matatizo mbalimbali(solution to different problems) hapa ieleweke kuwa tatizo si (negative thing) ila kama kitu kihitajicho kutatuliwa.
mfano mwanafunzi anapokuwa kwenye mtihani anakumbana na things which need solution. atatumia uelewa ufahamu na uwezo wake wa tafakuri kutoa suluhu kwa kadri inavyompasa.
akili ni imaginary kama ilivyo thought,yani huwezi ukapasua ubongo ukapima au kuona akili. akili hupimwa kwa kadri mtu anavyoweza kuleta suluhu ya mambo mbalimbali,mfano anaulwiza kitu ama anapaswa kufanya jambo analifanya kwa ufanisi na uhakiki.kwa wakati stahiki, akili hutofautiana baina ya watu.
sasa tunapokuja katika katika mtu mwenye akili kufanya matendo mabaya ni hivi huyu anaweza akawa ana ufahamu mkubwa ama uelewa mkubwa katika kitu fulani lakini sio katika kitu kingine kwa maana nyingine hakuna mwenye akili katika kila kitu. na tabia maadili na akili vyaweza visiende sambamba.
 
napenda sana kuwa najiuliza vitu ambavyo watu huwa tunatake for granted kuwa tunajua kumbe hatujui.sisi binadamu we have much to learn everyday. kwani hatujaweza hata kujielewa na kueleza hata yale yanayotuhusu kila kitu.
kazi kwelikweli.
 
mkuu qualified,
si kama katika hesabu wanasema problem find solution hivyo sio tatizo kwa maana ya negativity ya kitu hicho ila kwa vile inahitaji solution.nilikuwa namaanisha hivyo mkuu

negative si lazima ilete madhara but hata kitu kisicho na manufaa ni negative kwa mfano 1+1 isipokua na jibu ni problem saabu haina manufaa always remember 'soln is there to make sense' and that sence is positive
 
Kwa uelewa wangu akili ipo, ila haionekani(invisible) na (haishikiki)untoucherble. Akili inapimwa na inakuwa kadri mtu anavyo kuwa. "IQ" inteligence of quotent, ni kipimo cha ufahamu. Mtoto huwa anazaliwa na IQ 0 kama ilivyo kwa nyani. Kila siku anavyozidi kukua ndo akili yake inavyozidi kukua. Mtu mwenye IQ Kubwa ni 1700. Tafauti ya binadamu na nyani ni kuwa nyani IQ yake inaanzia 0 inaishia 500. Angefanikiwa kufikisha iq 700 angeweza kuongea angalao kama mtoto,angeweza kuita maji mma! Mtu mzima, wengi wanaufahamu wa IQ 1500-1600 wale wenye ufahamu mkubwa wana IQ 1750. Mtu ukifikisha miaka 70 na kuendelea kulingana na mabadiliko ya mwili, IQ yako inaanza kudumaa!
 
IPO formuler pia ya ku calculate IQ ya mtu!nikiikumbuka nitaitupia
 
HATA MIMI HUWA NAJIULIZAGA SANA KUHUSU AKILI/IQ
Huwa najiulizaga pia Mtu akiwa na uwezo mkubwa wa kukariri, hiyo ni akili?
Mtu akiwa anafanya mambo ya hovyohovyo (comedian) akawafurahisha watu huyo ana akili au IQ kubwa?
mtu akiwa ***** au wa mwisho darasani lakini anaujuzi juu aina fulani ya mchezo au ufundi, ana akili au IQ kubwa?
Mtu akiwa bingwa wa kuwaimbisha mabinti (tongoza) na kufanikiwa , ana akili au IQ kubwai?
Mtu akiwa na elimu kubwa (PhD in Business) halafu hawezi kufanya biashara ,huyo ni bwegeee hana IQ kubwa?
 
duh we ni nouma aisee.

Mtu akiwa na uwezo wa kuongea viziri sana, je ndio kusema ana akili? Tena akili ya kupewa dhamana ya uongozi.....

Tafakari chukua hatua
 
Akili ni nafsi isiyoonekana ambayo huboreshwa kwa vichocheo vingine kama kufikiri au kutafakari na kutenda ili kupata matokeo yanayoweza kuwa mazuri au mabaya. Akili huendana na kufikiri,udadisi,ufahamu,uelewa,umakini na utulivu. Mara nyingi mtu akifikiri vizuri na kutenda yaliyosahihi na matokeo yake kuwa mazuri,mtu huyo atasemwa ana akili.

Mtu asiye mgonjwa,ghafla akatenda kitu cha ajabu kama walivyofanya askari kumpiga na mmoja wao kumwua mwandishi wa habari Daudi Mwangosi na kujutia kitendo chake hicho cha kinyama baadaye, mtu huyo atasemwa hana akili timamu. Akili ni uwezo wa kufikiri na kutenda kwa ufanisi.Lakini bado matokeo ya kufikiri na kutenda yanaweza kuwa chanya au hasi.
 
mkuu!tunaposema mgonjwa wa akili tunamaanisha nini? Ni kitu gani kinakuwa hakipo normal kinapelekea kuugua Kichaa,uwendawazimu na au kuwa chizi? Hapa nafsi haihusiki. Nafsi inakaa kwenye moyo while akili inapatikana kwenye ubongo.
 
Hii TOPIC imeniweka njia panda, unajua huku mtaani kwetu kuna jamaa
ana matatizo ya akili. Yaani ana uchizi hasa tena kaishia Form II Pamoja
na uchizi wake anapoingia kwenye mchezo wa draft anaogopwa sana yaani
akili yake ni kubwa katika kulicheza draft. Si draft tu hata bao ambalo linahitaji
akili na hesabu za haraka, kweli inashangaza hii akili ni nini?
 
mi nafikiri uwezo wa kupata ufumbuzi haraka si kwamba iq yako ni kubwa bali ni kuweza kutumia kiasi cha iq ulichonacho efficiently
fact:iq kubwa ni kuweza kuhifadhi vitu vingi bila kusahau kiurahisi japo kumbukumbu zako zaweza kuwa kwa haraka ama taratibu

nawasilisha wakuu
 
Hii TOPIC imeniweka njia panda, unajua huku mtaani kwetu kuna jamaa
ana matatizo ya akili. Yaani ana uchizi hasa tena kaishia Form II Pamoja
na uchizi wake anapoingia kwenye mchezo wa draft anaogopwa sana yaani
akili yake ni kubwa katika kulicheza draft. Si draft tu hata bao ambalo linahitaji
akili na hesabu za haraka, kweli inashangaza hii akili ni nini?

Don't mix up Intelligence and smartness!Not every smart person is intelligent
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom