Akili zetu wanaume zinatutosha wenyewe, we acha tu!

ndyoko

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
4,971
1,649
Hiki ni kisa cha kweli kimetokea leo Mjini Dodoma. Endelea kupata uhondo............

Mtu anatoka 'guest' kufanya 'mambo' na mpenzi wake. Bahati nzuri ghafla anamuona dada yake naye anatoka guest na bofriend wake wakiwa wenye furaha baada ya kupeana raha. Ajabu kaka mtu hasira zinampanda na kuanza kumtolea maneno ya vitisho dada yake pamoja na bf wake. Kila mtu aliyesikia mkwara ule alimshangaa yule kaka kwa kukosa kwake busara. Iweje mtu mzima anayejua nini maana, uzuri na umuhimu wa mapenzi kwa mtu mzima kama dada yake, amtolee maneno ya vitisho ili hali naye ametoka kufurahia 'sex' na gf wake!

Hapa naomba niwaulize vidume wenzangu. Hivi ni kwa nini baadhi yetu tunapata 'uchungu' dada zetu wanapobanjuliwa na wanaume wengine wakati sisi wenyewe tunafanya hivyo kwa dada za wenzetu? uchungu huo unatokea wapi? Je ni kweli kwamba wanaojisikia uchungu dada zao wanapotoka na vidume vingine ni kwa sababu hao wakaka hawana ustaarabu wa mapenzi wanapokuwa 6x6 hivyo wanadhani dada zao nao wanakutana na kadhia wanazawafanyia dada za wengine? Hivi ni kitu gani hasa kikupe hasira na uchungu kwa dadako, ili hali yeye ndiye anayefurahia huo uhusiano na mpenzi wake?

Mbona wao huwa hawana kokoro akikukuta na gf wako-tena walivyo na upendo ndo kwanza atakushauri jinsi ya kuboresha mahusiano yenu. Hebu wanaume, jaribuni kuukubali ukweli kwamba raha unayoipata wewe uwapo na gf wako, dada yako naye anahitaji kupata hiyo raha kutoka kwa bf wake. Acheni hasira, kila mtu anapenda raha ya mapenzi. Hebu maindini bizinesi zenu, waacheni dada zetu wale raha na wapenzi wao kama nyinyi mnavyopenda kula raha na dada wa wenzenu.

Badilikeni!
 
"zinawatosha wenyewe" maana yake nini?
Au ndio mnajitetea kabla hata ya kufanya makosa?
Nwy wakaka kuwajali dada zao jambo la kawaida tu, I have been there.
 
we use them selfishly (we use them exclusively to our own advantage)
 
Me sitokuwa na uchungu kuona dada yangu anabanjuliwa, sasa asipobanjuliwa ni mimi ndio wa kumbanjua au??Yeah ni sawa tu akabanjuliwe sema ajali afya yake ukimwi mwingi now...
 
Isije ikawa ni tabia ya ma player. Wanaona uchungu kuwa dada zao wanachezewa kama wao wanavyochezea dada za watu. Makaka watulivu wanaweza kuwa different na nimeshawaona makaka waliotulia hawanaga time na kuchunga dada zao. :A S-coffee:
 
In most cases Wanaume wengi wana tabia za Kishenzi... Na wanajuana as men kua wanatabia za kishenzi hasa katika kukamilisha haja zao za miili. Ni mengi wanaume hufanyia mabinti/dada/mama wa wenzao bila kujale end result ya huyo mwanamke husika - wakijipa moyo kua haiwahusu.

Ndio maana weengi huumia saana wanapogundua dada/mtoto/mama yao anatoka na mwanaume fulani (hasa kama huyo mwanaume haeleweki in a man's perspective world). That is why most fathers wako soooo protective wa watoto wao wa Kike... yaani hujaribu kwa kila njia aweze timiza kila kitu ili mtoto wake yasimpate yale ambayo hata yeye mwenyewe hufanya kwa watoto wa wenzie.... BUT kama inavojulikana dunia haiendi hivo.... What comes around comes back around, na kila mla cha wenzie... chake pia huliwa.
 
mimi nimewahi kwenda 'out' kwenye first date mdada akiwa amesindikizwa na kaka yake
twice......tulikaa wote bar na kunywa na story kama kawaida...halafu mida mida kaka mtu akatuacha tu peke yetu
 
Hiki ni kisa cha kweli kimetokea leo Mjini Dodoma. Endelea kupata uhondo............

Mtu anatoka 'guest' kufanya 'mambo' na mpenzi wake. Bahati nzuri ghafla anamuona dada yake naye anatoka guest na bofriend wake wakiwa wenye furaha baada ya kupeana raha. Ajabu kaka mtu hasira zinampanda na kuanza kumtolea maneno ya vitisho dada yake pamoja na bf wake. Kila mtu aliyesikia mkwara ule alimshangaa yule kaka kwa kukosa kwake busara. Iweje mtu mzima anayejua nini maana, uzuri na umuhimu wa mapenzi kwa mtu mzima kama dada yake, amtolee maneno ya vitisho ili hali naye ametoka kufurahia 'sex' na gf wake!

Hapa naomba niwaulize vidume wenzangu. Hivi ni kwa nini baadhi yetu tunapata 'uchungu' dada zetu wanapobanjuliwa na wanaume wengine wakati sisi wenyewe tunafanya hivyo kwa dada za wenzetu? uchungu huo unatokea wapi? Je ni kweli kwamba wanaojisikia uchungu dada zao wanapotoka na vidume vingine ni kwa sababu hao wakaka hawana ustaarabu wa mapenzi wanapokuwa 6x6 hivyo wanadhani dada zao nao wanakutana na kadhia wanazawafanyia dada za wengine? Hivi ni kitu gani hasa kikupe hasira na uchungu kwa dadako, ili hali yeye ndiye anayefurahia huo uhusiano na mpenzi wake?

Mbona wao huwa hawana kokoro akikukuta na gf wako-tena walivyo na upendo ndo kwanza atakushauri jinsi ya kuboresha mahusiano yenu. Hebu wanaume, jaribuni kuukubali ukweli kwamba raha unayoipata wewe uwapo na gf wako, dada yako naye anahitaji kupata hiyo raha kutoka kwa bf wake. Acheni hasira, kila mtu anapenda raha ya mapenzi. Hebu maindini bizinesi zenu, waacheni dada zetu wale raha na wapenzi wao kama nyinyi mnavyopenda kula raha na dada wa wenzenu.

Badilikeni!

Wanaume tuna akili finyu when it comes to love business, ndio maana yanaoa mtu ameshazaa halafu linajidai "mke wangu, je aliyemzalisha!!
 
mimi nimewahi kwenda 'out' kwenye first date mdada akiwa amesindikizwa na kaka yake
twice......tulikaa wote bar na kunywa na story kama kawaida...halafu mida mida kaka mtu akatuacha tu peke yetu

Hapo ujue hao siri yao moja, huyo Mdada humtafutia Wadada Kaka yake.
 
Kuna kijana mmoja alikuwa ananitaka, siku hiyo akaja home na kumuomba kaka yangu aniite mimi (ila sikuwepo home), kaka akamuuliza wa nini? Akajibu ni rafiki yangu nataka niiongee nae (kaka alihisi ananitaka kimapenzi). Kaka akaingia ndani akatoka na bonge la panga, akamkimbiza na panga hadi karibu na kwao, tokea siku hiyo ananiogopa km nini hata akiniona anapita mbali!
 
Wanaume tuna akili finyu when it comes to love business, ndio maana yanaoa mtu ameshazaa halafu linajidai "mke wangu, je aliyemzalisha!!

eh kweli wanaume mna akili finyu.........Kumbe kila mnaezaa naye mnamwita mke!?
wengine tunataka kuzaa na nyie tu lakini hatuna haja ya kuolewa....sababu si kila mzazi anafaa kuitwa baba.
 
Kuna kijana mmoja alikuwa ananitaka, siku hiyo akaja home na kumuomba kaka yangu aniite mimi (ila sikuwepo home), kaka akamuuliza wa nini? Akajibu ni rafiki yangu nataka niiongee nae (kaka alihisi ananitaka kimapenzi). Kaka akaingia ndani akatoka na bonge la panga, akamkimbiza na panga hadi karibu na kwao, tokea siku hiyo ananiogopa km nini hata akiniona anapita mbali!
Usione fahari kwa hilo. Kaka yako ana ushamba wa karne ya 18
 
Jaman mie nahisi sijui ndio maumbile au vp,
Mie ilinitokea hivi;Kwetu hatuna kaka mkubwa kaka yetu ni mdogo wangu wa pili asa siku moja akanikuta natoka church niko na mkaka tunatembea njian tunaongea alipotufikia akanisalimia akamsalimia na yule mkaka alafu eti akasimama akamcheki kiaina alafu akaondoka kumbe kaenda kusimama mahali mie nipokatiza njia ya kwenda hm na yule kaka akaondoka zake kumbe eti alimfata yule kaka na kuanza kumhoji kuhusu mie yule kaka akamwelewesha kuwa ss ni marafiki tu,eti mdogo wangu akamwambia acheze mbali na mie lol!

Nilipojua nilimwita mdogo wangu nikaongea naye kwa upendo na kumshukuru kwa kunijali na kumtoa wasiwasi kuwa niko makin sana na kwa umri nilionao namudu kupambana na wanaume kwa hiyo asiwe anaingilia kwa namna yoyote nitakapo hitaji msaada wake basi nitamwambia,akanielewa natangu siku hiyo wala hana habari hata akiniona na mtu.
 
In most cases Wanaume wengi wana tabia za Kishenzi... Na wanajuana as men kua wanatabia za kishenzi hasa katika kukamilisha haja zao za miili. Ni mengi wanaume hufanyia mabinti/dada/mama wa wenzao bila kujale end result ya huyo mwanamke husika - wakijipa moyo kua haiwahusu.

Ndio maana weengi huumia saana wanapogundua dada/mtoto/mama yao anatoka na mwanaume fulani (hasa kama huyo mwanaume haeleweki in a man's perspective world). That is why most fathers wako soooo protective wa watoto wao wa Kike... yaani hujaribu kwa kila njia aweze timiza kila kitu ili mtoto wake yasimpate yale ambayo hata yeye mwenyewe hufanya kwa watoto wa wenzie.... BUT kama inavojulikana dunia haiendi hivo.... What comes around comes back around, na kila mla cha wenzie... chake pia huliwa.

Kweli ADii,

Bahati mbaya, hao ndio wanaume. Yaani wanaume wako hivyo hivyo...

Naomba kuboresha list yako kama ifuatavyo.
1. Kuna wanawake ambao ambao mtu hutamani kufa au kuua wakiguswa....... Mke na mama mzazi!!
2. Kuna wale ambao katika umri fulani au bila makubaliano yanayaeleweka, inauma sana tena sana kuona mtu anawagusa....mtoto na dada
3. Kuna wale ambao itamuuma kidogo endapo wanamendewa ila anaweza kuvumilia...ndugu wengine wa kike na rafiki wa kike ambaye umemzoea sana!!

Nadhani mwanamume angependa mbali na mke wake, wanawake wengine wasiguswe kabisa...Wabaki matowashi!!

Babu DC 1947!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom