Akili za Mbayuwayu !!!

ngoshwe

JF-Expert Member
Mar 31, 2009
4,131
925
Mara nyingi viongozi wetu wamekuwa wanafiki. Katika mambo ambayo yanaendelea kumpatia sifa kimataifa Mhe. B.W. Mkapa (Rais Mtaafu wa Tanzania) ni upeo wake wa kufahamu,kuchambua na kuweka sawa masuala mengi ya kijamii, kiuchumi na kisiasa.

Mkapa bado anatambulika katika safu za Viongozi wa Taifa letu na amekuwa akionekana kuwa mpigania haki mzuri sana kwa mataifa mengine ikiwemo kuhusika katika upatanishi wa jirani zetu wa Kenya katika mgogoro uliotokana na uchaguzi wao Mkuu wa mwaka 2007.

Mkapa anajua sana matatizo ya nchi yake ikiwemo yale ya Kikatiba pia na angeweza kusaidia kushauri kupatiwa ufumbuzi kama alivyokuwa Baba wa Taifa. Lakini cha kusikitisha yupo kimya sana hapa nyumbani na anaonekana akiongelea hukooo "nyumba za jirani" mambo ambayo kwa busara zake angeweza kabisa kuwasaidia wanasiasa wetu ndani ya chama chake kupata akili za "mbayuwayu" na kulewezesha Taifa letu likwamuke katika wimbi la matatizo ya kijamii, kiuchumi na kisiasa...

Nini Busara za vingozi kama hawa??wanasubiri mpaka wafe ndo waje kuandikwa vizuri zaidi na kuenziwa??.


 
Last edited by a moderator:
mambo hayo............................................kikwete aliusema tumwache apumzike na anafanya mapumziko nje ya nchi na anasaidia zaidi nchi za nje..........kwa hiyo kwa heshima ya rais tumwache mkapa apumzike
 
Mkapa hana udhu wa kusema lolote hapa nyumbani. Alitumia vibaya madaraka yake kwa kujilimbikizia mali na ndiye aliyeliingiza taifa letu kwenye matatizo ya ubepari na ubeberu mamboleo kwa kujidai kwamba yeye anajua zaidi.
 
jamani, kwenu nyie ambao mko bongo, tunaomba mtupatie maana ya huu msamiati "mbayuwayu", kwasababu kuna jamaa fulani humu aliiniita mi mbayuwayu nikadhani ananitukana. wengine hatujarudi huko bongo kwa miaka kadhaa sasa tunajiandaa kurudi kipindi hiki cha uchaguzi. explanation please!
 
Ubungoubungo, Mbayuwayu ni ndege wanojenga nyumba zao kwa kutumia tope na mra nyingi hujengea kwenye vibaraza vya nyumba,ni ndege wanaopenda kukaa majumbani.
 
@ubungoubungo jamaa jana haukukutukana, huyu ndege 'rahisi' kampa umaarufu kwa kutoa mfano wake kwenye hotuba yake kwa wazee wa dsm juzi.

kwamba ndege huyu alimuuliza ndege ng'ong'onda (sina uhakika na jina) anawezaje kutoboa miti....., akajibibiwa aruke juu sana kisha agonge mdomo wake kwenye jiwe na afanye hivo mara mbili.
mbayuwayu akapaa aliposhuka hakuthubutu kugonga lile jiwe kisha akajiambia mwenyewe.......'akili zako changanya na zako'
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom