Akikosolewa Alikiba sawa, ila akikosolewa Diamond chuki!

Lavit

JF-Expert Member
May 16, 2011
13,136
27,079
Hazijapita siku nyingi toka Alikiba atoe video na audio ya Lupela, nyuzi nyingi zilianzishwa kuponda kazi yake na wengi wakisisitiza kwamba video ni mbaya!!

Sasa leo baada ya kutoka video ya Diamond na AKA, kila anayeenda tofauti na mitazamo yao na kukosoa video eti anaitwa hater! Mara hawapendi maendeleo ya Mtanzania mwenzao na upuuzi mwingine mwingi!!

Hivi hawa watu wao wanampenda Kiba na kutaka kuona anafika mbali? Wanachokifanya siyo chuki kama wanachohubiri dhidi ya watu wanaokosoa kazi za Diamond?? Inawezekana kweli kazi zote za kiba zikawa mbaya kwao? Au ndiyo hiki kinachoitwa ushabiki maandazi?
 
Mkuu Lupela haiwezi hata kuinusa hii make me sing ni video kali kiukweli imechangamka ina ladha tofauti ukilinganisha na hii ya kiba.
 
Hazijapita siku nyingi toka Alikiba atoe video na audio ya Lupela, nyuzi nyingi zilianzishwa kuponda kazi yake na wengi wakisisitiza kwamba video ni mbaya!!

Sasa leo baada ya kutoka video ya Diamond na AKA, kila anayeenda tofauti na mitazamo yao na kukosoa video eti anaitwa hater! Mara hawapendi maendeleo ya Mtanzania mwenzao na upuuzi mwingine mwingi!!

Hivi hawa watu wao wanampenda Kiba na kutaka kuona anafika mbali? Wanachokifanya siyo chuki kama wanachohubiri dhidi ya watu wanaokosoa kazi za Diamond?? Inawezekana kweli kazi zote za kiba zikawa mbaya kwao? Au ndiyo hiki kinachoitwa ushabiki maandazi?
Tatizo ushabiki maandazi mwingi na ile timu timu isiyokuwa na maana..."always am support the good music alive" kukosolewa kwa mwanadamu ni kawaida chukua makosa kayafanyie kazi...mbona kiba wamemkosoa sana huyo diamond ni nani mpaka asikosolewe.
 
Unajua kuna mashabiki wengine wanajiona wao wanajua Kila kitu. Wanapenda kuona msanii Fulani anakosolewa tu ila akikosolewa wa kwako ni tabu sana
 
hii kitu haiwezi kuisha mkuu,wala isikuumize kichwa...
tangu lini ukaona mashabiki wa Ali Kiba wamesifia kazi ya Diamond...
pia ni lini ushawahi ona mashabiki wa Diamond kusifia kazi za Ali Kiba..?
hata wewe huu uzi wako pia umeutoa kiSHABIKI zaidi...
hii kitu haiwezi kuisha hadi hawa watu waache MZIKI..!
 
Tuweni wakweli jamani lupela imechuja mapema sana uwezi fananisha na hii make me sing. Hii kitu ni international na itaanza kupenya taratibu kwenye masikio yenu mpk wanaoponda ndio watakuwa wapenzi wakubwa wa hii.
 
Tatizo ushabiki maandazi mwingi na ile timu timu isiyokuwa na maana..."always am support the good music alive" kukosolewa kwa mwanadamu ni kawaida chukua makosa kayafanyie kazi...mbona kiba wamemkosoa sana huyo diamond ni nani mpaka asikosolewe.
Diamond ni Icon wa TaifA
 
Watu wengine bhana; utafikiri huyo Kiba akikosolewa hao mashabiki wake wanakaa kimya!! Halafu haya mambo simple tu! Leo hii ukiwa shabiki wa soka la Ulaya halafu ukaikosoa Liverpool inaleta mantiki manake hawana cha kuonesha pamoja na ukongwe wao lakini ukiwakosoa Man City au Chelsea au Barcelona kule Spain, unatakiwa kutoa hoja vinginevyo utaonekana kiroja!
 
Tatizo ushabiki maandazi tu wengine ikibadilishwa verse kidogo tu ikawa kiingereza hta maana yke hawajui ila ndio watashabikia verse tamu kumbe hta kilichoimbwa ukiwauliza hawajui
 
Back
Top Bottom