Akikataa mapenzi na urafiki ufe?

WomanOfSubstance

JF-Expert Member
May 30, 2008
5,457
956
Kuna kipindi cha radio kinazungumzia mada ya mahusiano baina ya wanawake na wanaume.Kitu kilichonistua ni ujumbe uliosema " akikutaa kimapenzi basi na urafiki ufe".Ina maana wanawake na wanaume hakuna urafiki isipokuwa mapenzi? Inakuwaje kwa wale ambao hawana " uwezo" wa kutoa penzi ?
 
...WOS,....mijitu ya aina hiyo haina tofauti na wale waajiri wanaogomea ajira mpaka wapewe penzi!
Sijui haina ndugu wa kike kwao?
 
...WOS,....mijitu ya aina hiyo haina tofauti na wale waajiri wanaogomea ajira mpaka wapewe penzi!
Sijui haina ndugu wa kike kwao?

Kwa kweli nimeshtuka..nikakumbuka kwenye mashule kuna wasichana na wavulana huwa na urafiki wa kushirikishana mambo ya masomo, nikaingia maofisini nikajiuliza inakuwaje kwa workmates ambao hujikuta wakielewana sana kwa sababu ya mambo ya kazi.Nikaja sehemu za biashara ambapo wanawake na wanaume huweza kuwa na networks ambazo hazihusu " mapenzi"... nikajikuta najiuliza maswali mengi.Ina maana wanaume hawa wote wanalenga kupata penzi? Jibu likaja kuwa " siyo lazima...."
Kama ulivyosema, watu kama hawa waweza kusababisha tafrani kwenye jamii!!...
Lakini kabla hatujamhukumu...... huenda kuna ujumbe anaotaka kuutoa, labda hatujampata vizuri?
 
Naona hapa alikua na maana ya mwanamme akimwomba mwanamke wawe wapenzi na mwanamke kukataa na kuomba wawe marafiki wa kawaida,ile lets just be friends ok? ambayo ni njia ingine ya kumkataa mtu.
 
Ddd yuko right....... Ni kuwa ukiomba penzi na ukijataliwa ni vyema hata huo urafiki ufe labda kwa kuona wanaume wengi huwa hawawezi kustahamili hiyo situation anyway
 
Huo urafiki bora ufe naona,Maana huo urafiki gan tena ambao utakuwepo hapo?
 
urafiki una husisha ku match characteristics and interest so it depends.
Next hii inategemeana mwanzo ulikuwaje is it ,I love you because I need you or I need you because I love you.
 
Pengine alianzisha urafiki ili apate penzi. Kama penzi hakuna, urafiki una maana gani tena.

Ni kama wale wanaosoma ili wapate kazi, na sio kuelemika. Kama kazi hakuna, basi hakuna kupoteza muda kwenda shule.
 
Hii inashtua.

Vipi kama urafiki uliunganishwa na kazi? I mean kama mlikuwa mnafanya kazi pamoja kwa muda mrefu kama team members. Urafiki ukavuka mipaka ya kazi na kuingia kwenye ngazi ya familia. Ikatokea rafiki huyo anakutaka kimapenzi, ukakataa, ina maana urafiki huo ufe?
 
mnaweza mkawa marafiki tu hata kama mmoja amemkataa mwingine kimapenzi kifupi ni kuelewa nini mwenzako anamahanisha anapokukatalia mapenzi

binafsi mie baadhi ya wachumba zangu wa zamani kabla sijaoa bado wamebaki kuwa rafiki zangu tunawasiliana kwenye facebook na tunajuliana hali bila tatizo lolote na wengine wameolewa na nimechangia na kuudhuria harusi zao ni uelewa tu wa mtu kukataliwa sio chanzo cha chuki ni matokeo tu ya kihisia ambayo tunabidi tukubaliane nayo na kuyakabiri
 
Kuna kipindi cha radio kinazungumzia mada ya mahusiano baina ya wanawake na wanaume.Kitu kilichonistua ni ujumbe uliosema " akikutaa kimapenzi basi na urafiki ufe".Ina maana wanawake na wanaume hakuna urafiki isipokuwa mapenzi? Inakuwaje kwa wale ambao hawana " uwezo" wa kutoa penzi ?
Mwenzio akikataa kuwa mwenzi wako kimapenzi....usilazimisha. Unaweza endelea na urafiki kama kawa. Tena kwa uzoefu wangu mimi ndiyo una-kuwa free nae sana!:violin:
 
Urafiki gani tene utakuwepo hapo, marafiki hushare intrst, na intrst yako wewe ni kugongana, na yeye hataki kugongana....PIGA CHINI.
 
Hao watakuwa na matatizo kwa hiyo yeye kila akiwa na rafiki wa kike lazima atoe penzi ? inatisha
 
Kwa kweli nimeshtuka..nikakumbuka kwenye mashule kuna wasichana na wavulana huwa na urafiki wa kushirikishana mambo ya masomo, nikaingia maofisini nikajiuliza inakuwaje kwa workmates ambao hujikuta wakielewana sana kwa sababu ya mambo ya kazi.Nikaja sehemu za biashara ambapo wanawake na wanaume huweza kuwa na networks ambazo hazihusu " mapenzi"... nikajikuta najiuliza maswali mengi.Ina maana wanaume hawa wote wanalenga kupata penzi? Jibu likaja kuwa " siyo lazima...."
Kama ulivyosema, watu kama hawa waweza kusababisha tafrani kwenye jamii!!...
Lakini kabla hatujamhukumu...... huenda kuna ujumbe anaotaka kuutoa, labda hatujampata vizuri?
kwahiyo huo urafiki wa maslahi ila ule urafiki wa kweli kabisa hauwezekani!!!! labda awe gay!!!!
 
mimi sitaki urafiki na mtu alonitaka kimapenzi ..................na anikalie mbali kama nimeshamwambia simtaki :D
 
Nadhani kikubwa ni motive ya urafiki wao. Kama ilikuwa ni mapenzi, hana budi kumuacha. Lakini kama ni suala lingine, si busara kumwacha kutokana na kwamba mapenzi siyo motive ya urafiki wao!
 
Hao watakuwa na matatizo kwa hiyo yeye kila akiwa na rafiki wa kike lazima atoe penzi ? inatisha

Sio lazima utoe penzi...ila kama ikifikia wakati wa mmoja kutaka penzi, ilhali upande mwingine haupo tayari, basi urafiki hauwezi kuwepo tena!
 
Back
Top Bottom