Akaanza Kutetemeka Alipomuona

Tembomtata

JF-Expert Member
Oct 3, 2011
266
426
Nilipokuwa Mzumbe nikipata nondoz yangu ya kwanza nilibahatika kupata na toto moja matata kwel kwel,na bila kuamini mim ndo nilikuw wa kwanza kufungua ukurasa kwa mtoto yule nilikuta wajanja bado kabisaaaa hawajagusa ,ki ukweli tulipendana sana(hadi sasa),tulipomaliza chuo mim nikaamua kijiendeleza kwa mwaka mmoja wakati ule yeye alikuwa nyumban akitafuta kazi, kwa bahat mbaya hakufanikiwa kupat, kwa vile wanajiweza kidogo wakamwambia akajiendeleze kwa kupiga Msc pale IRA-UD.

Kwa vile mim ni mkaazi wa kilimanjaro kuonananae ikawa ishu kidogo lakin angalau mara 1 kwa miez 2 tukawa tunaonana, juzi nikasema nika mtembele mtoto wang, basi nikafika vizuri nika chukua chumba pale Landmark-ubungo nikawa najilia vyangu taratiiiiiibu sasa nikakaa.

Ijumaa,mpaka j4, lj3 akaenda darasan, basi ilipofika saa 7 nikapanda zang mliman nikamwambia aje tupate lunch pale hill park basi mtoto akaja tukawa tunapiga vitu vyetu sasa, baada ya muda wakaja jamaa flan wakawa wamekaa meza ya mbali kidogo, basi binti akaniambia kuwa wale ni classmates wake ila akaanza kutetemeka kishenzi,akawa ananiambia huwa wanamtaniga darasan.

Muda si muda jamaa mmoja kati ya wale akapita akienda maliwatoni binti akakosa comfdnce akawa anasmile minikawa na mpigisha story baada ya kuona hali ile basi jamaa akapita baadae akarudi kukaa kweny kiti chake, basi binti akaniambia tuondoke mahali pale bila kusita nika mwambia poa tuhamie samak samak wakat tunatoka akaniomba akawasalimie basi akaenda akaongea nao kama kwa nusu dakika kisha akarudi akanishika kiuno tukaondoka zetu, wakati tunaelekea huko akaniambia wale jamaa wana gari na huwa wanawatokeaga madem weng,na madem huwa wanashobokaga na gari lao,

Ila mim nikawa na maswal mengi
1.kwanin akose comfednce alipowaona wale jamaa?
2.kwanin aliporudi alinishika kiuno na sio kawaida yake?
wanajamii hebu nisaidieni
 
Amewambia wewe ndo kaka yake mkubwa, yan ndo wa kwanza nyumbani 'kwenu'! so akawaonesha makea 'yenu' si ulisema kwao wanajiweza,so ndo aliwaonesha 'uzungu' wa hom 'kwenu':lol:
 
Ukiona Manyoya Ujue ameshaliwa huyo, na yeye ni mmoja wa wale wanaowashobokea hivyo jifunge mkanda.
 
wakati tunaelekea huko akaniambia wale jamaa wana gari na huwa wanawatokeaga madem weng,na madem huwa wanashobokaga na gari lao,

sasa mtu kuwa na kigari tu, wasichana wanashobokea nini? anyway, kwa ufupi wewe piga kitu tu ulale mbele coz mko wengi mnaopitia hapo
 
sijui hata niseme nini hapa kwa kifupi kuna mmoja anatoka na binti au wako mbioni kuanza kudate
Inakuwaje akose confidence mpaka aombe kuondoka ???
 
Baba ukusijia paa ujue imekulamba nikawaida ya ya ingin ikisha gonwa lazma iogope ilichokigongwa daa itakua amewatel we cousin wake mmekutanba bahat mbaya!
 
kuna kitu kuhusu wasichana wa ki tz na magari....
sijui ni nini hasa...
kuna mtu anayaita 'hirizi ya mjapan' lol......
kweli hirizi ya mjapan. Nakumbuka niliwahi ambia 'huna gari utakuwaje na mimi' ndo nikakukumbuka kuwa na mazoea ya kuazima magari inasaidia kwa watu kama hao.
 
unakuta mtu kiwanja hana,lakini ana magari mawili ya mkopo..
watu bana lol

Hehehehe kwasababu yanaonekana kirahisi. Akiwa na nyumba watu wasiomfahamu hawawezi kujua anayo mpaka awaambie, wakati gari hata machinga naona "dah, yule mshkaji anatembelea tairi aisee." Wabongo kwa sifa hawawezekani!!
 
Huyo demu wako anatembea na huyo jamaa aliyeenda chooni na ndio maana alitetemeka sana na kuanza kusmile, pia ulipompa ruhusa ya kwenda kuwasabahi alienda kuua soo kwa kudanganya ya kuwa wewe ni ndugu wa karibu/mjombake/kakake.
Pia yawezekana yeye ni mmoja wa kuzimikia gari la huyo jamaa.
:eyebrows:
 
Hivi mshkaji mpaka leo unaamini kuna dem wa peke yako? Wakati hata mawaif tunashea ktk ulimwengu wa leo!
 
alikosa confidence,sababu yeye ni mwanamke haswaaa mwenye haya za kike,aibu kula starehe na mwanaume wako mbele ya watu unaowafahamu.....

pili ingekuwa ametoka na mmojawapo asingekushika kiuno,amekushika kuwaonyesha she is taken/proud of you,.......kaka kosa ni kumkuta/kumfumania na mtu kitandani mengine yote yanasameheka/yanaongeleka sababu mapenzi ni imani tu..................................
 
Back
Top Bottom