Ajiua kwa kudaiwa shoga

minda

JF-Expert Member
Oct 2, 2009
1,068
65



Tuesday, 28 September 2010 04:42
Na Benjamin Masese

13.JPG

MWANAMUME mmoja aliyefahamika kwa jina la Deogratius Paul (39), mkazi wa Kinondoni amekutwa amekufa chumbani kwake akiwa na ujumbe mfupi wa maandishi kuwa 'mimi si shoga kama inavyodaiwa nina familia na mtoto, Mungu shahidi yangu'.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Bw. Elias Kalinga alisema kuwa tukio lilitokea juzi saa 12 alfajiri baada ya mwili wa marehemu kukutwa ukining'inia kwenye shuka iliyotundikwa kwenye dari.

Bw. Kalinga alisema chanzo cha kifo hicho bado hakifahamika lakini kwa mujibu wa ujumbe huo inadaniwa kuwa amejiua.

Maiti imehifadhiwa katika Hospitali ya Mwananyamala na upelelezi unaendelea.


Source: Majira
 
Kama unasingiziwa kwanini ujiue halafu useme MUNGU anajua :mad2::mad2::mad2:huo sio uamuzi sahihi na wala sijaafiki kuna jambo zaidi limejificha ndani yake
 
Back
Top Bottom