Ajira

zema21

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
619
251
Ajira ni tatizo kubwa linaloikabili dunia na nchi yetu pia!! Viongozi mbali mbali wakiwemo wabunge na viongozi wengineo kadhaa walisikika wakikiri ya kuwa ukosefu wa ajira kwa vijana ni bomu ambalo litalipuka muda wowote! ingawaje hakuna mwenye takwimu wahitimu wengi wa vyuo wapo mitaani wakitembea huku na kule kutafuta ajira, tempo na hata wengine wanatafuta pa kufanya internship pasipo mafanikio....

Wapo wanaoshauri kuwa vijana wajiajiri pasipo kuangalia suala la ukosefu wa mitaji kwa vijana hao..(kujiajiri panahitaji kuwa na mtaji wa vitendea kazi ikiwamo pango jengo la ofisi, vitendea kazi na fedha za kujiendesha mpaka pale business itakapo stabilize, marketing ikiwamo matangazo ya bidhaa/products ukiachilia mbali elimu ya ujasiria mali ambayo vijana wengi wanaikosa!!!

Serikali kupitia wizara ya kazi na maendeleo ya vijana inatoa fedha kwa kila halmashauri kwa ajili ya makundi ya vijana ambao wanataka kujiajiri! lakini tatizo ni kuwa ili upate fedha hizo lazima uwe umejiunga kwenye saccoss ambapo unatakiwa uweke 1/3 halafu ndipo upate mkopo kwa ajili ya mtaji! mathalani unataka kukopa milioni tatu lazima uweke kwanza milioni moja(Jambo ambalo ni gumu saana kwa vijana wanaohitimu vyuoni ikizingatiwa wengi wanatoka katika familia za kawaida na za chini)

hebu tujaribu kufikiria kwa pamoja kama wewe ungepewa nafasi ya kuwa Mkuu wa nchi ungekuja na sera/mipango gani ambayo ingewawezesha vijana wetu waondokane na tatizo hili.. Na waweze kujiajiri/kuajiriwa!!!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom