Tatizo la ajira kwa watumishi katika mwaka tajwa inaonekana ni mfupa ulioishinda serikali ya JPM.Hakuna kiongozi hata mmoja wa serikali iwe Mh.Rais mwenyewe au wasaidizi wake mwenye jibu la uhakika kuhusu swala hili...Mh.Rais mbele ya umma wa watanzania alisema ajira zipo lakini anasitisha kutoa vibali ili kuhakiki watumishi hewa ambalo ni jambo zuri..lakini ni zaidi ya miezi miwili sasa sio mawaziri,Rais mwenyewe hata waandishi wa habari ambao wamekwisha hoji juu ya kauli mwwndelezo ya hili swala baada ya muda aliousema mtufuku Rais kupita..mimi naamini serikali hii ina watu makini itoe majibu ya uhakika juu ya swla hili ili kama vijana waliomaliza katika fani tofauti waamue ni uelekeo upi wachukue juu ya hatma ya maisha yao..tena itoe specific day ya kutoka kwa ajira hizi kama zipo kuliko kutoa majibu kama ya kina Jaffo na Kairuki eti mda wowote kwanzia sasa..mi sijawahi kuuona huo muda wowote...Wana jukwaa hili swala ni letu sote..ndugu zetu wana msongo wa mawazo juu ya swala hili..hata sekta binafsi zinashindwa kuwa ajiri watanzania hawa kwa kuhofia kua mda ambao haujulikano serikali itatoa ajira hvyo watumishi waliokua wamewachukua kulamizika kuondoka kwenye vituo vya kazi...naiomba serikali yangu sikivu itoe jibu lenye mwafaka sasa kwa Taifa letu..kama ajira zipo zinatoka lini na kama hazipo waombe radhi kwa kuwapotezea muda na kuwa hadaa watanzania..