Ajira za watanzania kuchukuliwa na wageni, serikali ipo?

Ally Musa

New Member
Jul 8, 2011
4
1
KUMEKUWA NA WIMBI LA WAGENI HASA WAHINDI AMBAO WANAINGIA NCHINI KWA KISINGIZIO KWAMBA NI WATAALAM (EXPATRIATE), LAKINI KAZI WANAZOKUJA KUFANYA NI ZILE AMBAZO VIJANA WAKITANZANIA WANAWEZA KUZIFANYA VIZURI SANA. KWA MFANO KATIKA KAMPUNI YA NOKIA SIEMENS, KUNA MHINDI MMOJA ETI ANAITWA EXCEL SPECIALIST. KAMPUNI INADAI IMEMLETA KWA AJILI YA KU-COMPILE REPORT KWA KUTUMIA EXCEL, JE WATANZANIA NI WAJINGA KIASI HICHO? KAMPUNI HII YA NOKIA SIEMENS INAZAIDI YA EXPATRIATE 12, JE UTARATIBU WA NCHI UNASEMAJE KUHUSU WAGENI? KAMPUNI YA KINGSWAY INTERNATIONAL (american garden) INA WAFILIPINO AMBAO KAZI YAO NI MAUZO, YAANI SALESMAN. JE WATANZANIA HATUWEZI HATA KUUZA? PALE MOVENPICK HOTEL KUNA MKENYA MMOJA YEYE KAZI YAKE NI ROOMS ALLOCATION. JE WATANZANIA HATUWEZI KUFANYA KAZI YA ROOMS ALLOCATION? KAMA NI HIVYO BASI SISI WATANZANIA NI WAJINAGA, AU TUNAVIONGOZI WAJINGA. WANAJUKWAA MNASEMAJE KUHUSU HILIJAMBO?
 
Nimesoma website ya AIRTEL,unachosema ni kweli.Ukiangali management ,ni almost all foreigners!
Sijui tunakwenda wapi
 
Watanzania ni wajinga ndio na pia tuna viongozi wajinga, hii hali haijaanza leo na wala haitaisha leo, kuna mianya ambayo wanaitumia hawa wageni ambayo huwezi kuziba. Watanzania nao waende nje kuchukua kazi, thats exactly what I am doing.
 
Tatizo lipo serikalini hasa Wizara ya Mambo ya Ndani, sijui wanatoa vigezo gani mpaka kumpa mgeni WORK PERMIT Najua wapo Watanzania wengi ambao wana uwezo wa kufanya hizo kazi ila Immigration ndio tatizo kubwa kwetu wanatoa vibali bila ya kujali kama kuna ndugu zao ambao wanao uwezo wa kuzifanya hizo Kazi. CCM inatupeleka pabaya kila aliyeipigia kura CCM sasa wanaanza kujuta, tunajichimbia kaburi wenyewe
 
Tatizo la nchi yetu ni kwamba wengi wanajali maslahi yao binafsi,kwani sheria ipo kabisa ya kuwataka wageni waajaliwe tu wale ambao hakuna mtanzania mwenye ujuzi huo,lakini hakuna utekelezaji wa sheria hiyo.viongozi wa kitanzania rushwa imewazidi.
 
Watanzania ambao unataka wafanye hizo kazi wako bize wanashinda JF na kulalamika

Mbona mna mbunge raia wa Burundi na hamlalamiki?
 
Hili li inchi linakera sana, mtu ni msomi, ana wadhifa mkubwa , mshahara mkubwa, gari zuri kifupi hana shida, lakini anapewa rushwa ya Tsh 200,00 tu anatoa maamuzi ambayo yanaathiri jamii nzima. Wanatoa hivyo vibali ni corrupt sana pale mambo ya ndani, Leba, na Uhamiaji panahitaji kusafishwa sana.

Mwezi huu January nilipewa uhamisho kwenda Kenya na Shirika ninalofanya kazi ambalo lipo nchi kadhaa Afrika. Serikali ya Kenya walininyima kibali vile walisema kazi unayoletwa kufanya yaweza kufanywa na Wakenya wengi tu pengine kwa ubora kuliko wewe. Lakini ajabu shirika hilo hilo lina Wakenya hapa TZ na hata nchi zingine kwa kazi ile ile niliyokuwa niende kufanya huko. Usiulize mambo ya elimu, uzoefu na uzeefu mimi ni bora zaidi kuliko wao waliopo hapa nchini
 
Nakubaliana nawe kuhusu hawa wahindi na pia wageni wengine kupewa kazi ambazo watanzania wangeziweza kabisa. Makampuni kama metl group, azam group, azania, mecb, lake group nimetaja makampuni chache tu!! Kwa mahesabu ya upesi nadhani kutakuwa na wageni zaidi ya laki tano hapa nchini mwetu na wengi wao wanafanya kazi ambazo mtanzania anaziweza.
Je watanzania hawezi kuwa salesman, warehouse keeper, hotel floor manager, supermarket supervisor, supermarket warehouse receiving head, accounts assistant, data collector, invoicing clerk au hata secretary???
Jamani watanzania wanazidi kuwa maskini wakati hawa wageni wanachota tu!!
Hawa matajiri wa tanzania hawatujali sisi watanzania wanasema watanzania ni wezi na lazy!!
Dawa yao ni kuongeza ada ya work permit maradufu ili hawa matajiri wakome!!!
 
Nenda viwanda vya wahindi, wahindi wamejazana huko. Wanalala hukohuko. Sahivi hadi wachina wanauza karanga unategemea nin?? Tanzania is a failed state, hakuna sekta hata moja inayofanya vizuri. Hata moja.

Taasisi ya urais ndo imeua hii nchi!!!
 
Mkuu sasa kwenye Mashule ya Private ndo shida yaani walimu wapishi na manesi wanatoka nje zaidi Uganda na hawana work na residential permit kabisa ila uhamiji wanaogwa tu. Hii nchi aina uongozi kabisa.
 
Nusu ya mtoa mada na wachangiaji ni kweli nusu kuna taarifa zisizo sahihi. Ni kweli hakuna nchi humu duniani inaruhusu watu wasio raia kufanya kazi kiholela. Kuna masharti magumu ya kupata kazi kwenye nchi ya kigeni. Ila tukumbuke soko huria la ajira unapoenda kuomba kazi ya room hotel reception ya international hotel quality ya reception ya new york inapaswa kuwa sawa na Dar. Hivyo kama unatakiwa kufahamu lugha 3 za kimataifa basi wote huwa hivyo. Tz wachache kwenye fani hiyo huongea lugha 3 kwa ufasaha. Unadhani huko uingereza hamna wachezaji mpira? Lakini kwa viwango wanavyotaka ndio maana unaona akinq Yahaya wanacheza huko. Pili ni suala la uhusiano wa kimataifa ukiwafukuza bila utaratibu au ukinyima vibali bila utaratibu nchi husika hulipiza kisasi kwa kufukuza raia wenu huko kwao. Sina hakika na India vs Tanzania lakini hilo liliwahi kuongelewa kuhusu China na Tanzania. Cha muhimu wafuate utaratibu na sie tuusimamie ipasavyo. Loopholes tuzifunge sisi wenyewe na sio kulalamika. Tatu baadhi ya miradi ni ya uwekezaji wenyewe wanataka kulinda mali zao kiuchumi unaangalia kiwanda kinaajiri watanzania 100 na wageni 8 au kuwakatalia na kiwanda kisiwepo na watanzania 100 wakakosa kazi? Tuliangalia kwa upana wake. Msumbuji wao wapo clear wageni hapaswi kuzidi asilimia 5 ya wafanyakazi wote na hawajali kada hata kama ni wafagizi. Ndio maana nasema tuliangalie kwa mapana yake
 
Back
Top Bottom