Ajira za walimu wiki ijayo

paesulta

JF-Expert Member
Mar 13, 2009
227
29
Gedius Rwiza
SERIKALI inatarajia kutoa tamko
kuhusu ajira za walimu 25,015
waliohitimu mafunzo ya ngazi
mbalimbali katika vyuo vya
ualimu nchini wiki ijayo.
Kati ya hao, walimu wa
sekondari ni 13,636 wa shahada
wakiwa 6,649 na stashahada ni
6,987 na walimu wa shule za
msingi ngazi ya cheti ni 11,379.
Hatua hiyo itaondoa hofu kwa
wahitimu wa mafunzo ya ualimu
ambao wamekaa nyumbani kwa
zaidi ya miezi saba wakisubiri
ajira, kinyume cha ahadi ya
Serikali kwamba wangeajiriwa
mara tu baada ya kuhitimu
masomo yao.
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa
na Serikali za Mitaa (Tamisemi),
Kassim Majaliwa alisema jana
kuwa mwanzoni mwa wiki ijayo,
Serikali itatoa tamko la ajira hizo.
Majaliwa alisema ajira hizo ni
kwa ajili ya walimu waliohitimu
vyuo mbalimbali vya ualimu
kuanzia Mei, 2011 katika ngazi za
cheti, stashahada na shahada.
“Napenda kuwataarifu walimu
kwamba hakuna mwalimu
atakayebaki bila kupata ajira na
hatutaki mwalimu afike kituo cha
kazi akose mahitaji muhimu
kama ilivyokuwa miaka ya
nyuma, kwa hiyo mwanzoni mwa
wiki ijayo majina yatakuwa
kwenye tovuti za Wizara ya Elimu
na Tamisemi,” alisema Majaliwa.
Majaliwa alisema tayari utaratibu
wa kuwapangia vituo vya kazi
walimu hao 25,015 umekamilika
na kwamba Wizara ya Fedha
imearifiwa ili iweze kupeleka
Sh6.2 bilioni katika halmashauri
zote nchini ili walimu
watakapofika wakute fedha zao
tayari.
Alisema hakuna mwalimu
atakayebaki bila kuajiriwa kama
ilivyokuwa ikielezwa na baadhi ya
vyombo vya habari. Alisema
sababu za kuchelewesha ajira
hizo ni kutaka kukamilisha
mahitaji yote ya walimu hao.
Majaliwa alisema Serikali ina nia
njema ya kuwapatia ajira walimu
wote lakini hawataki kuona
mwalimu akifika kazini na kuanza
kuteseka kutokana na ukosefu
wa mishahara hali ambayo
imekuwa ikiwafanya walimu
wengi kukimbia vituo vya kazi.
Alisema wakurugenzi wa
halmashauri zote wameagizwa
kuwapokea na kuwapangia kazi
walimu hao watakapofika, baada
ya kuwa wamewapatia mahitaji
muhimu ili wasitoroke kutokana
na hali ngumu ya maisha.
“Hata wakurugenzi wote
tumewapa taarifa ya kuwapokea
walimu hao bila kuwabughudhi
na kuwapatia mahitaji muhimu
ya kuanzia maisha ili wawe na
moyo wa kufanya kazi kwa
ufanisi. Kwa hiyo nawaomba
walimu wawe na subira,” alisema
Majaliwa.
Baada ya kukaa mitaani kwa
takriban miezi saba tangu
wahitimu vyuo, walimu hao
wamekuwa na hofu ya kukosa
ajira ya Serikali na wamekuwa
wakiilalamikia Serikali kwa
kushindwa kuajiri kama
ilivyokuwa miaka ya nyuma
ambayo waliokuwa wakimaliza
walikuwa wakiajiriwa mara tu
baada ya mafunzo.
 
Wamebanaaa karibu wanachia,ok asante kwa taarifa sasa hofu ni moja cjui ntapangiwa wapi mie!
 
ni vigumu kuamini...tumepigika vya kutosha,kusoma sio dili siku hizi kwani ukisoma unakalishwa kitaa...
Walisema Dec mwaka jana,sijui kama watatekeleza
 
Kama walimu watapewa fedha za kujikimu mapema bila mikingamo,basi hlo litakua jambo la AJABU MNO,TUSUBIRI
 
utata co kale kapesa kakujikimu.. Ila mziki upo kwenye hela za mizigo na wategemezi hapo lazma walimu njuka wachakuchuliwe.. Watachezea Siasa za kufa m2.. By da way best of luck...
 
by da way kama kuna mwl atapangiwa cngda mjini/manispaa.. Anitafute ntampa hifadhi kipindi ambacho atakuwa anajipanga kusimama mwenyewe.. N:B. Kwa walimu masela kama mimi isije akaja mwanamama akaja shindwa kutoka
 
kama kweli umesota vya kutosha utakwenda,halafu baadae unaangalia utaratibu mwingine...kesho usije lalamika kuwa hakuna ajira
 
utata co kale kapesa kakujikimu.. Ila mziki upo kwenye hela za mizigo na wategemezi hapo lazma walimu njuka wachakuchuliwe.. Watachezea Siasa za kufa m2.. By da way best of luck...

duh hapo sasa natishika mkuu.Heb nisaidie mbinu gan itumike ili wasichakachue? Then ntajua ni kiasi gan m2 anapaswa kulipwa kama fedha ya mizigo na wategemezi? Kwel unjuka kazi nisaidien wakuu
 
Hata mm kma ningepata msaada wa kujua kiasi cha pesa tunachotakiwa kupewa ingekuwa vzr sana maana unaweza ukapewa hela kdogo alafu ukaanza kuutabika.so 2naoomben msaada wa kujua hlo kwa wale wazoefu.
 
by da way kama kuna mwl atapangiwa cngda mjini/manispaa.. Anitafute ntampa hifadhi kipindi ambacho atakuwa anajipanga kusimama mwenyewe.. N:B. Kwa walimu masela kama mimi isije akaja mwanamama akaja shindwa kutoka

pia nawakaribisha arusha,wakaka kwa wadada karibu!
 
PM aliwaamrisha waorodheshe stahiki za mwajiriwa katika barua yake ya ajira.ni bunge lililopita,km sijakosea.
 
Back
Top Bottom