Ajira za upendeleo toka kwa mawakala wa kazi

kisugujira

JF-Expert Member
Aug 13, 2012
774
196
Kutokana na uhaba wa ajira uliopo sasa hivi nchini, vijana tunaotafuta ajira tunatakiwa kuwa makini na taasisi za nje zinazotoa matangazo ya kuwepo nafasi za kazi kwa niaba ya makampuni yanayotaka au tayari yanafanya kazi hapa nchini.

Vijana wengi tusio na ajira tumekuwa tukituma maombi ya kazi kwenye makampuni mbalimbali kupitia taasisi hizi bila mafanikio yoyote! Taasisi hizo au mawakala hao wa kazi toka nje kama My Jobs Eye na Prime Time Personnel Africa ya nchini Kenya yanafanya kazi kibaguzi. Wanatoa matangazo ya nafasi za ajira kwa watanzania lakini wanaopata kazi ni wakenya!

Mara nyingi utakuta wanataka mtu awe na elimu ya sekondari ya KCSE yenye C tupu (with C plain), kibali cha kufanyia kazi,pasipoti,leseni ya gari daraja BCDE na kadhalika. Kwa hiyo utaona mahitaji yote hayo huwa ni kwa mtu asiye raia wa hapa nchini. Wanakuwa wameisha waandaa watu wao toka Kenya kuja kufanya kazi hapa nchini.

WanaJF nini kifanyike kuondoa ukilitimba huu?

Nawakilisha.
 
bora hata hao wana watu wao amabao huwalipa vizuri japo kwa upendeleo,je haya makampuni ya kwetu umeshajua kiwango na jinsi wanavyotoa ajira kwa upendeleo?
 
Ngoja siku moja panuke ndo tutaheshimiana inasikitisha mtoto wa mkulima umesoma kwa shida tena ada zilipatikana kwa kuuza shamba na kumega kipisi cha kiwanja upande wa choo alafu unakosa ajira.Ndo maana shehe Mponda anawafuasi wengi wanaotaka kutibua amani coz watu wana njaa wengi mno.
 
Back
Top Bottom