Ajira za TANROADS: Kuna Harufu ya Ubaguzi na Upendeleo

Hawa Tanroads kwa sasa hawatofautiani sana na mtu ambaye anaingia kwenye chumba cha mtihani huku majibu anayo tayari mkononi. Haya matangazo ni muendelezo tu wa udanganyifu katika kutafuta mbinu za kuhalalisha vitendo vyao vya kibaguzi, hila na upendeleo...
 
Ajira nyingi za taasisi za umma na serikali, hasa kwa kazi zile ambazo zina watu wengi walio na sifa, zimejaa mizengwe, kujuana na ubabaishaji.
 
Mkuu Mwita Maranya.Huo umri jamaa walioutoa ni wazi kuwa wana malengo ya ku retain watu wa ndani wanaotaka hama nafasi.Na hii ni maalumu ili kulinda mitandao yao ya kibaguzi na wizi kwa umma.

Watu wa umri huo na wenye elimu watakuwa na kazi nyingine na mazingira ya interview yatakuwa magumu. Tanzania kuna wenda wazimu mwingi sana.Kuna kazi za uzoefu na kuna kazi zinazohitaji mtu kuwa energetic na well motivated.Kwa uzoefu wangu vijana wengi hu-perform vyema wakiwa supervisors ktk kazi ambazo ni challenging, na watendaji wazoefu waachiwe wafanye hizo kazi.Hapa pako tricky ila ndipo panapohitaji optimization.HUyu kijana akipewa ukaguzi na shift za usiku atafanya kazi,ila anahitaji kupewa time frame ajue kufanya ili aweze chukua nafasi ya utendaji kama ilivyopaswa.


NI kwa vile hatujafikia utendaji wa kuona kwamba kutenda tuu hakutoshi tena,ila kutenda kwa ufanisi ndiko kunapotakiwa,basi ndipo hizi tabia za kibaguzi na uzembe zitaanza tokomea.Taani ifikie mahali daktari ajisikie fahari watu wangapi kawaponya katika mazingira ya hatari, wafikie mahali si tuu kuwa wamefanya operation salama bali wamefanya salama na yenye kuacha mwili wa mgonjwa ukiwa na umbile la kupendeza.Hawa jamaa tanroads na TRA wafikie mahalai pa si tuu kuwa wapeta wafanyakazi wenye vyeti bali wenye uelewa wa kutosha maliza sheria na procedures zote na hivyo kufikia mahali pa kuweza ona mapungufu na hivyo kuleta mbinu mbadala.
 
Dah.. Tayari? Siku zinaenda kasi eeh? Lol. This will be best discussed via pm... Karibu Speaker. Pamoja saana.

Yaani,it's 3months now mtaani.
Hata JF sija ichangia na nimetoka kwenye u-premium.
So sad.
Ngoja nihamie upande wa pili.
 
We nawe, ndo mana jina lako ni kiroba..LOL
Keshasema na wengine, sasa ulitaka ataje wana JF wote....!

Na kiroba anaalikwa kuchangia mada hii.... haya changia sasa maana nimekutaja kwa jina lako

Hakuna cha kusema na wengine maana hapa JF kila mada inayowekwa inajulikana ni ya wote, sasa yeye alitaja baadhi ya watu ili iwe nini. Kwani hao aliowataja hawafai kuwa na wengine? Kubali kataa hii thread inaubaguzi ndani yake....
 
Hata hii habari uliotoa ina harufu ya ubaguzi mkubwa. Binafsi siwezi nikachangia kabisa kwa kuwa umewalenga rafiki zako unaowajua na umewakopi kwa kuonyesha msisitizo. Hali hii ni mbaya sana kwa maendeleo na ustawi wa taifa letu. Napinga kwa sauti kuu huu ubaguzi ulioufanya. Kama umeufanya kwa makusudi basi mungu akuhukumu kwa dhambi ya ubaguzi, na kama ni bila kufahamu basi mungu akusamehe kwa kuwa hujui ulitendalo.
umenichekesha kweli-kweli
 
mkuu hujaeleza hizo kazi zimetoka lini na mwisho wa kuomba ni lini;usipende kulaumu sana waachie wenye sifa waombe.Tupe link ya kazi hizo tafadhali.
 
AshaDii,
Nimekuelewa lakin bado nina doubts! Vipi kuhu range hiyo ya miaka mitano..Kwani wangetuamia tu sera ya serikali inayosema ajira kwenye Public Service (kwa permanent and pensionable terms) maximum age ni 45 wangekosa watu wenye sifa hizo? I.e nina swali kwanini wasiseme 35-45? Na kama ni uzoefu mara nyingi inatakiwa iwe katika similar au related position na kwenye taasisi inayofanana au kukaribiana kwa kesi ya TANROADS maana yake kwenye Government Agencies zingine au taasisi nyingine za serikali. Mimi nahisi labda kuna mambo mawili
1. Wanataka ku recruit from within i.e kuna watu wenye sifa hizo ndani ya Tanroads pengine kuna watu walikuwa wanafanya kwa contracts au kwa kujitolea, au
2.Kuna watu wao waliondaliwa na wenye sifa kama hizo

Naomba niwe wazi na niseme mawazo yangu hapa ni vile tu ambavyo nafikiria na sio kwamba kuwa definetly najua iko hivo. Nijuavyo ni kuwa kuna kazi age ya mtu ina matter sana regardless ya kusema kuwa kustaafu ni early 50s. Kuna kazi inahitaji mtu ambaye ni kijana na yupo fit... Kama unavyoelewa kuwa from 45 kuendelea kasi ya kazi sio sawa na chini ya hapo.

Nikija kwenye hio kwa nini not to 45, assumption yangu ni kuwa wanapo ajiri hio nafasi wanataka mtu ambae maybe kwa makadirio awafanyie kazi walau hata miaka sio chii ya 10 na akiwa katika hali ambayo ni ya kudai tokana na demand ya kazi ambayo inatakiwa kufanya. Kwa hio akiwa waruhusu 45 inakuwa kama inakula kwao... Lol.

Nakubaliana na hizo assumption zako, kuna possibility kubwa kuwa yawezekana...
 
mkuu hujaeleza hizo kazi zimetoka lini na mwisho wa kuomba ni lini;usipende kulaumu sana waachie wenye sifa waombe.Tupe link ya kazi hizo tafadhali.


hahaha! Mwita Mazegezege anaomba link... Lol. Imenifurahisha saana hii post. Maadam kazi zinam favour basi poa tu...
 
Kaka nikupongeze kwanza maana we unaona mbali, sijui nikuite kiona mbali? huu ni ubaguzi kabisa pia inaonekana kama ni planned process. naona kuna watu wameshapangwa kwa hizo nafas, hata mimi nimeziona na nimejaribu kuomba Mwanza na Kibaha, ila nimemwachia Mungu kama nitapata au lah! ila kigezo cha umri sikua nacho.
 
Mwita Maranya, Nguruvi3, Mchambuzi,

..nakubaliana na hoja ya Nguruvi3, pamoja na Mchambuzi.

..suala la umri halikutakiwa kuwekwa kwasababu linakwenda kinyume na kanuni ya USAWA KTK AJIRA.

..kanuni hiyo inakataza ubaguzi ktk masuala ya jinsia, kabila,imani, umri, etc etc.

..binafsi sielewi TANROADS walikuwa wanalenga nini kwa kuweka kigezo cha umri wa miaka 35 to 45. kama walikuwa wanataka watu wenye uzoefu basi wangeweka kipengele cha UZOEFU wa kazi.
 
mdau umetoa la moyoni,na limetoka,nami tabia hii siipendi

umri una nafasi sana hasa katika nafasi ya kufanya maamuzi na uadilifu,graduate mwenye miaka 23 si rahisi kuogopa rushwa ukilinganisha na mtu mwenye miaka 37 ambaye tayari anategemewa na familia.n uwazi kuwa hii kazi ina majaribu,na wakati mwingine sehemu za rushwa hata watu wa juu yako wanakulazimisha kupokea rushwa ili na wao walinde maslah ya wakuu mbalimbali. Hii kazi kweli inahitaji watu strong sana na wenye uzalendo wa kweli m nimefuatilia sana kujua hali halisi
 
Back
Top Bottom