Ajinyonga kwa kutumia Mtandio Baada ya Kugombana na Mumewe

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,316
33,125
MWANAMKE mmoja aliyetambulika kwa jina la Pendo Kimaro [21] amejinyonga kwa kutumia kitambaa cha kujitanda kichwani [mtandio] baada ya hasira ya kugombana na mumewe. Akitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari jijini Dar es SaLaam, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova amesema kuwa, tukio hilo lilitokea jana majira ya saa 4 asubuhi huko Kurasini jijini Dar es SaLaam.

Kova amesema kuwa, polisi wamepata taarifa kutokana na mume wa dada huyo aliyetambulika kwa jina la Shija Kabaho [25] kuja kutoa taarifa katika kituo cha polisi.

Amesema kuwa mume huyo aliieleza polisi kuwa kulitokea mfarakano kati ya wana ndoa hao na kusema kuwa wakati alipotoka kwenda kwenye shughuli zake aliporudi alimkuta mke wake huyo ameshafariki.

Amesema kuwa aliporudi nyumbani alimkuta mkewe huyo amekufa na kugundua kuwa alijitundika kwa kutumia mtandio wake ambao ulikuwa umefungwa kwenye dali ya nyumba hiyo.

Amesema mwili huo umechukuliwa na kwenda kuhifadhiwa hospitali ya Temeke na uchunguzi wa kina unaendelea kubaini chanzo halisi cha kifo hicho.
http://nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsId=2578702&&Cat=1
 
Back
Top Bottom