Ajinyonga kwa kunyimwa unyumba

Tume iundwe mara moja na watakaoteuliwa kwenye hii tume
wawe wanalipwa mil. kwa siku ili ufanisi wao uwe juu
na ripoti itolewe baada ya wiki mbili tu.
watu wengi inaelekea wananyimwa unyumba ila hawataki kujiua
kwani watakua wanachakachua nje .
 
Hahahaaaaa....eti imechacha...!!!Yap,km vp una m'sms......siku hz kuna BBM,WHATSAPP na vitu kede kede!!!!!!

Tatizo issue hii imetokea huko maeneo ambayo cidhani kama hata mchina wanayo.. Kimjini mjini mbona rahisi kabisa kwa kutumia hizo apps ulizozitaja hapo huu.. Wengine wanatumiana mpaka picha za mnato na video za hiyo mambo ya kikubwa..
 
MKAZI wa Mtaa wa Mpanda Hotel, Wilaya ya Mpanda mkoani Katavi, Nzego Vicent (33), amejiua kwa kujinyonga na kamba baada ya mkewe kumnyima tendo la ndoa.Tukio hilo limetokea hapo juzi majira ya saa 7:30 usiku jirani na nyumba waliyokuwa wakiishi wanandoa hao.Mke wa marehemu huyo aitwaye Agnes Nicodemu, alisema siku ya tukio mumewe ambaye alikuwa ametoka kwenye pombe za kienyeji, alifika nyumbani kwake majira ya saa 6:20 usiku na kumtaka ampe tendo la ndoa

Kwa nini asiseme amelewa tu mpaka aseme ameleweshwa na nini? Polisi waanzie kuchunguza hili.....huenda kanyongwa huyu member wetu
 
kwakisa hiki lzma tukubali ukizidisha sana pombe nihatari kwani utakosa busara yakufanya maamuzi!lkn kama hyo mama naye ndio ulikuwa ni utaratibu wake wakumnyima ushilikiano mume wake basi hafai kwani alifuata nini kwenye ndoa...raha ya ndoa nikupeana ushilikiano na kuweka mipango ya maendeleo!
hapo sio unyumba ni kumbaka yaani ufanye mapenzi na mlevi raha iko wapi hapo kweli! ndio sababu mama akahairisha zoezi
 
Jamani bongo kuna mambo! Hii imetokeo huko Subawanga, nimeikuta HabariLeo.

Mume Ajinyonga Kwa Kunyimwa Unyumba
Imeandikwa tarehe 09 oktoba 2012
Na Peti Siyame, Sumbawanga

MKAZI wa Mtaa wa Mpanda Hotel wilayani Mpanda katika Mkoa wa Katavi, Nzego Vicent (33) amejinyonga hadi kufa kwa kutumia kamba ya katani huku akimlalamikia mkewe kwa kumnyima unyumba kwa siku tatu mfululizo bila kupewa sababu zilizomridhisha.
Mashuhuda wakiwemo baadhi ya majirani wa wandoa hao kwa masharti ya kutoandikwa majina yao gazetini, walidai kabla ya kujinyonga, Vicent ambaye alikuwa ametoka kunywa pombe za kienyeji, alifika nyumbani kwake saa 6:20 usiku na kumtaka mkewe ampe unyumba.
Majirani hao walidai kuwa mke wa marehemu, Agnes Nicodemu alilalamikia mumewe kuwa hakuwa tayari kumpatia unyumba kutokana na shughuli alizokuwa amezifanya mchana kutwa na kumsihi avumilie hadi siku itakayofuata kwa kuwa alikuwa amechoka sana.
“Siku mbili mfululizo mama huyo kutokana na kuelemewa na kazi nzito za shamba na nyumbani kwake ambazo alikuwa akizifanya kuanzia alfajiri hadi usiku wa manane, aliendelea kumsihi mumewe ambaye alikuwa akirudi nyumbani usiku kuwa amechoka,“ alidai mama mmoja jirani na wanandoa hao.
Inadaiwa kuwa baada ya Vicent kujibiwa hivyo kwa siku tatu mfululizo hakuridhika na madai hayo ya mkewe ndipo alipoanza kumshutumu kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na wanaume wengine.
Inadaiwa siku ya tatu, Vicent alimshambulia mkewe huyo kwa kumpiga sehemu mbalimbali za mwili wake huku akimtolea maneno ya kumtisha kuwa lazima atamuua kwa mapanga iwapo ataendelea kuwa mkaidi katika unyumba.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari, baada ya kuona kipigo kimezidi mwanamke huyo alikimbia nje ili kukwepa kipigo na mumewe naye alitoka nje ya nyumba yao akiwa ameshikilia mashoka mawili na kwenda kusikojuliakana na kuiacha nyumba ikiwa wazi.
Ilipotimu saa 12:30 alfajiri, mwanamke huyo alifuatwa na majirani waliomweleza kuwa mumewe amejinyonga kwa katani jirani na nyumba waliyokuwa wakiishi ndipo alipoandamana nao hadi eneo hilo na kumuona akiwa amening’inia juu ya mti
 
Hii ni hatari,sasa unakubali vipi kuolewa halafu unakataa kutoa haki ya ndoa?Nadhani kulikuwa na zaidi ya kunyimwa unyumba ndio maana jamaa kaamua kujitundika.
Hivi mtu akijitundika nae tunasema Mungu amlaze mahali pema peponi au?
 
Hii ni hatari,sasa unakubali vipi kuolewa halafu unakataa kutoa haki ya ndoa?Nadhani kulikuwa na zaidi ya kunyimwa unyumba ndio maana jamaa kaamua kujitundika.
Hivi mtu akijitundika nae tunasema Mungu amlaze mahali pema peponi au?[/QUOTE]

Wanaojiua wengi wanapatwa na ugonjwa fulani wa akili unaosababisha wachukue hatua hiyo. Hivyo ni vema tu kuwaombea mema.
 
Hii Topic nilishaweka hapa juzi! tafuta topic mpya! Ni ushauri tuu.
 
Hii ni hatari,sasa unakubali vipi kuolewa halafu unakataa kutoa haki ya ndoa?Nadhani kulikuwa na zaidi ya kunyimwa unyumba ndio maana jamaa kaamua kujitundika.
Hivi mtu akijitundika nae tunasema Mungu amlaze mahali pema peponi au?[/QUOTE]

Wanaojiua wengi wanapatwa na ugonjwa fulani wa akili unaosababisha wachukue hatua hiyo. Hivyo ni vema tu kuwaombea mema.
Ewe mwenyezi Mungu naomba uilaze roho ya marehemu aliyejiua kwa kujinyonga mahali pema peponi.Amina.
 
huu uonevu mtu anashinda vilabuni hafanyi kazi afu akifika hata hampi pole ya kazi huyo kibarua wake wa shambani afu anajinyonga.
 



MKAZI wa Mtaa wa Mpanda Hotel wilayani Mpanda katika Mkoa wa Katavi, Nzego Vicent (33) amejinyonga hadi kufa kwa kutumia kamba ya katani huku akimlalamikia mkewe kwa kumnyima unyumba kwa siku tatu mfululizo bila kupewa sababu zilizomridhisha.Mashuhuda wakiwemo baadhi ya majirani wa wandoa hao kwa masharti ya kutoandikwa majina yao gazetini, walidai kabla ya kujinyonga, Vicent ambaye alikuwa ametoka kunywa pombe za kienyeji, alifika nyumbani kwake saa 6:20 usiku na kumtaka mkewe ampe unyumba.Majirani hao walidai kuwa mke wa marehemu, Agnes Nicodemu alilalamikia mumewe kuwa hakuwa tayari kumpatia unyumba kutokana na shughuli alizokuwa amezifanya mchana kutwa na kumsihi avumilie hadi siku itakayofuata kwa kuwa alikuwa amechoka sana.“Siku mbili mfululizo mama huyo kutokana na kuelemewa na kazi nzito za shamba na nyumbani kwake ambazo alikuwa akizifanya kuanzia alfajiri hadi usiku wa manane, aliendelea kumsihi mumewe ambaye alikuwa akirudi nyumbani usiku kuwa amechoka,“ alidai mama mmoja jirani na wanandoa hao.Inadaiwa kuwa baada ya Vicent kujibiwa hivyo kwa siku tatu mfululizo hakuridhika na madai hayo ya mkewe ndipo alipoanza kumshutumu kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na wanaume wengine.Inadaiwa siku ya tatu, Vicent alimshambulia mkewe huyo kwa kumpiga sehemu mbalimbali za mwili wake huku akimtolea maneno ya kumtisha kuwa lazima atamuua kwa mapanga iwapo ataendelea kuwa mkaidi katika unyumba.Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari, baada ya kuona kipigo kimezidi mwanamke huyo alikimbia nje ili kukwepa kipigo na mumewe naye alitoka nje ya nyumba yao akiwa ameshikilia mashoka mawili na kwenda kusikojuliakana na kuiacha nyumba ikiwa wazi.Ilipotimu saa 12:30 alfajiri, mwanamke huyo alifuatwa na majirani waliomweleza kuwa mumewe amejinyonga kwa katani jirani na nyumba waliyokuwa wakiishi ndipo alipoandamana nao hadi eneo hilo na kumuona akiwa amening’inia juu ya mti
 
huyu mume ijapokuwa analewa lakini nimuaminifu kwa ndoa. wewe mke jamani hata kamoja tu umeshindwa kumpa
 
Back
Top Bottom