Ajinyonga kwa kukataliwa na mke wa mtu

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
266
HAMISI TUMBUKA [25] Mkazi wa Kibamba, amekutwa amejinyonga kutokana na sababu za kimapenzi baada ya kukataliwa na mke wa mtu ambaye alikuwa akimpenda kupita kiasi
Marehehemu huyo alikutwa amekufa akining’inia juu ya mti na kuacha ujumbe mzito ambapo alibainisha sababu cha kifo chake na kumtaja mwanamke ambaye alikuwa akimsumbua akili na kumuandika jina lake lililofahamika kama Ashura

Mbali na kuacha ujumbe pia alitoa maagizo kwenye ujumbe huo kuwa azikwe kiiislamu na aliomba msichana huyo aliyemtaja kwa jina la Ashura ashuhudie mazishi yake kwa kuwa alisababisha kifo hicho

Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela alisema kuwa, tukio hilo lilitokea juzi , majira ya saa 2 asubuhi, huko Kibamba ambapo polisi walikuta mwili wake ukining’inia kwenye mti.

Kamanda Kenyela amesema kuwa marehemu huyo alitumia kamba ya katani kujinyonge na kukutwa na ujumbe uliosema

“Naomba Waislamu wanizike hapa hapa na Ashura ashuhudie ninavyozikwa..., Ashura nakupenda uishi salama na mumeo.” Ulimaliza ujumbe huo

Polisi mkoani Kinondoni wameuhifadhi mwili huo katika Hospitali ya Tumbi Kibaha kwa uchunguzi zaidi.
 
Sir god anamsubili "****** huyo"kwa ma2,
1-kamtamani mkee wa mtu
2-kaua nafsi yake,
****** huyo.
 
Sasa police watafanya uchunguzi gani?
Ama wanataka kumjua huyo Ashura aliyesababisha kifo!
 
Mkuu LIVERPOOL FC nadhani umesahau utaratibu wao,
Huwa wanasema hv(uchunguzi bado haujakamilika)na kawaida huwa unakamilika after a lot of years
 
Habari kama inatolewa na jamaa hawa bado si ya kuaminika. ona bosi wao alivyotoa habari ya ajabu kuhusu Mwakyembe kulishwa sumu au la.
 
Huyo jamaa kaamua tu kumsingizia ashura lazima alikuwa na yake mambo akaamua kupakaza ili tu amharibie ashura! watu wengine virus kichizi
 
Asa alivyojinyonga ndo kampata au kamuachia mwenzie afaidi
kwa nafasi.
Mwanaume jitume, tumia ulichonacho kupata unachokitaka.
 
pengine ashura *alipima na kujikuta na ukimwi na ikawa *sabb ya kumkatalia
:lol:
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom