Ajinyonga kwa kuchoshwa na vipigo vya mkewe

[h=4]Comments [/h]

0 #1 harrid 2011-08-08 06:21 dah tamwa wanahitajika kuchukua au kuchukuliwa atua.manake kidume kujiua si mchezo, ustawi wa jamii mpoooooo.hii ishu si ya kitoto na si ya kawaida,kweli jamaa alionewa.

WanaJF pateni huu uhondo;

MKAZI mmoja katika Mtaa wa NHC katika Mji wa Mugumu wilaya ya Serengeti wilayani Mara, Samson Kitoshi (32) amejinyonga hadi kufariki dunia kwa kamba chumbani kwake kwa kile alichodai kuwa: “Amechoka kupigwa na mkewe kila wakati.”

Tukio hilo lililovuta umati mkubwa wa watu, linadaiwa kutokea jana saa tano asubuhi. Akisimulia mkasa huo, mtoto wa marehemu (Jina tunalihifadhi) alisema kabla ya kutokea kwa tukio hilo, mama yao alimpa Sh 1,000 akanunue sukari na vitafunio, lakini asimpe baba yao chai... "Mama aliaga kuwa anakwenda Hospitali DDH kwa kuwa anaumwa. Baba akasema hatakunywa chai hiyo na kutuambia kuwa hatutamwona tena anatuaga na tusiingie ndani."

Marehemu baada ya kuingia chumbani kwake anadaiwa kuwa alifunga kamba juu ya dari na kujining'iniza hadi alipokata roho.Mtoto huyo wa darasa la tatu ambaye ana umri wa miaka 10 alisema hawakuweza kuingia ndani kama walivyoambiwa na baba yao, lakini baadaye aliamua kumwamsha akidhani kuwa amelala ili anywe chai ndipo alipokuta amening'inia. Alipiga kelele kuomba msaada.

"Baba alikuwa amevua shati akawa amening'inia chini kuna meza nikaweka stuli ili nifungue kamba sikuweza nikapiga yowe majirani wakafika wakasema ameshakufa," alisema.

Kuhusu migogoro ya ndani, mtoto huyo alisema kumekuwa na ugomvi wa mara kwa mara hasa ukisababishwa na mama yao ambaye anauza pombe ya kienyeji ya wanzuki anaporudi akiwa amelewa kwani humfanyia vurugu baba yao.

"Hivi karibuni baba alifikia hatua ya kumtaka mama aondoke amechoka na mateso anayomfanyia, lakini mama alikataa kuwa hawezi kutoka na kudai yeye ndiye atakayetoka," alisema.Ndugu wa Kitoshi ambaye anaishi katika Kijiji cha Morotonga alisema kuwa marehemu aliyekuwa akifanya kazi ya kusaga nafaka alikuwa akilalamika kupigwa na mkewe mara kwa mara.

"Huyu ni ndugu yangu hata leo amefika kwangu na akanikosa na kurudi nadhani alitaka kuniambia kitu. Baada ya muda nikapigiwa simu kuwa amekufa kwa kujinyonga, amechoshwa na kupigwa," alisema.

Kamanda wa Polisi Wilaya ya Serengeti, Paulo Mng'ong'o alijaribu kumtafuta mwanamke huyo kwa simu lakini mara baada ya kujitambulisha kuwa yeye ni OCD, mama huyo alikata simu.

Baada ya muda mama huyo alifika nyumbani na kumkuta mume wake akining'inia kwenye kamba. Huko alipokewa kwa maneno makali kutoka kwa wanawake wenzake waliokuwa na hasira baadhi wakisema: “Ulitaka afe ujitawale sasa amekufa tanua... unadanganya ulikuwa hospitali mbona umelewa..."

Maneno hayo makali yalimwingia mwanamke huyo kwani alikaa chini kisha akalala chali na kupoteza fahamu. Hakuweza kunyanyuka hadi alipopakiwa kwenye gari la polisi pamoja na mwili wa mumewe na kupelekwa hospitali.

Akizungumzia tukio hilo, Kamanda Mng'ong'o alisema polisi inalifanyia uchunguzi na kwamba itatoa taarifa kwa umma. Alisema wangefanya mahojiano na mke huyo wa marehemu baada ya kuzinduka kujua chanzo cha kifo hicho.Mwenyekiti wa Mtaa wa NHC, Elias Nyamraba alisema kuwa wanasubiri ndugu wa marehemu kwa ajili ya hatua nyingine ikiwemo ya mipango ya mazishi akisema Kitoshi ni mzaliwa wa Kijiji cha Issenye.

Source: Mwananchi

Shughuli, nayeye si angehama tu nyumbani mpaka ajitoe uhai ?! Na mke mlevi ana nguvu ya kupiga mume ?! Mwe!

MKAZI mmoja katika Mtaa wa NHC katika Mji
wa Mugumu wilaya ya Serengeti wilayani
Mara, Samson Kitoshi (32) amejinyonga hadi
kufariki dunia kwa kamba chumbani kwake
kwa kile alichodai kuwa: “Amechoka
kupigwa na mkewe kila wakati.”
Tukio hilo lililovuta umati mkubwa wa watu,
linadaiwa kutokea jana saa tano asubuhi.
Akisimulia mkasa huo, mtoto wa marehemu
(Jina tunalihifadhi) alisema kabla ya kutokea
kwa tukio hilo, mama yao alimpa Sh 1,000
akanunue sukari na vitafunio, lakini asimpe
baba yao chai... "Mama aliaga kuwa
anakwenda Hospitali DDH kwa kuwa
anaumwa. Baba akasema hatakunywa chai
hiyo na kutuambia kuwa hatutamwona tena
anatuaga na tusiingie ndani."
Marehemu baada ya kuingia chumbani
kwake anadaiwa kuwa alifunga kamba juu
ya dari na kujining'iniza hadi alipokata
roho.Mtoto huyo wa darasa la tatu ambaye
ana umri wa miaka 10 alisema hawakuweza
kuingia ndani kama walivyoambiwa na baba
yao, lakini baadaye aliamua kumwamsha
akidhani kuwa amelala ili anywe chai ndipo
alipokuta amening'inia. Alipiga kelele
kuomba msaada.
"Baba alikuwa amevua shati akawa
amening'inia chini kuna meza nikaweka
stuli ili nifungue kamba sikuweza nikapiga
yowe majirani wakafika wakasema
ameshakufa," alisema.
Kuhusu migogoro ya ndani, mtoto huyo
alisema kumekuwa na ugomvi wa mara kwa
mara hasa ukisababishwa na mama yao
ambaye anauza pombe ya kienyeji ya
wanzuki anaporudi akiwa amelewa kwani
humfanyia vurugu baba yao.
"Hivi karibuni baba alifikia hatua ya kumtaka
mama aondoke amechoka na mateso
anayomfanyia, lakini mama alikataa kuwa
hawezi kutoka na kudai yeye ndiye
atakayetoka," alisema.Ndugu wa Kitoshi
ambaye anaishi katika Kijiji cha Morotonga
alisema kuwa marehemu aliyekuwa akifanya
kazi ya kusaga nafaka alikuwa akilalamika
kupigwa na mkewe mara kwa mara.
"Huyu ni ndugu yangu hata leo amefika
kwangu na akanikosa na kurudi nadhani
alitaka kuniambia kitu. Baada ya muda
nikapigiwa simu kuwa amekufa kwa
kujinyonga, amechoshwa na kupigwa,"
alisema.
Kamanda wa Polisi Wilaya ya Serengeti,
Paulo Mng'ong'o alijaribu kumtafuta
mwanamke huyo kwa simu lakini mara
baada ya kujitambulisha kuwa yeye ni OCD,
mama huyo alikata simu.
Baada ya muda mama huyo alifika nyumbani
na kumkuta mume wake akining'inia
kwenye kamba. Huko alipokewa kwa
maneno makali kutoka kwa wanawake
wenzake waliokuwa na hasira baadhi
wakisema: “Ulitaka afe ujitawale sasa
amekufa tanua... unadanganya ulikuwa
hospitali mbona umelewa..."
Maneno hayo makali yalimwingia
mwanamke huyo kwani alikaa chini kisha
akalala chali na kupoteza fahamu. Hakuweza
kunyanyuka hadi alipopakiwa kwenye gari
la polisi pamoja na mwili wa mumewe na
kupelekwa hospitali.
Akizungumzia tukio hilo, Kamanda
Mng'ong'o alisema polisi inalifanyia
uchunguzi na kwamba itatoa taarifa kwa
umma. Alisema wangefanya mahojiano na
mke huyo wa marehemu baada ya
kuzinduka kujua chanzo cha kifo
hicho.Mwenyekiti wa Mtaa wa NHC, Elias
Nyamraba alisema kuwa wanasubiri ndugu
wa marehemu kwa ajili ya hatua nyingine
ikiwemo ya mipango ya mazishi akisema
Kitoshi ni mzaliwa wa Kijiji cha Issenye.

Mimi huwa najiuliza sana,inakuwaje unajiua kwa sababu ya mtu?This is insane!Huwezi kumwona mtu ambae umekutana nae ukubwani tena labda miaka mitano tu iliyopita na ulikua humfaham kabla ya hapo,unamuona bora kuliko maisha na uhai wako!!Wehu huu!!

Wakurya bwana.....
Wanaume ni balaaa......
Wanawake ni kasheshe.........
Dawa ni kuwaacha waoane wenyewe kwa wenyewe ili wapigane mapanga hiyo ndio raha yao.

mi zamani kujiua ni kwa ajili ya Mkwawa na watu wake tu, kumbe nlikuwa nimeingia choo cha watoto, huko nikakuta mapoti tu.

Dawa ya mwanamke mkorofi kama huyo ni kumtelekeza tu. Unatafuta kimwana mwingine then nduki.

ndio madhara ya kutafutiwa mchumba hayo, matokeo yake unaparamia miana mke ambayo inabeba vyuma na kuvuta bangi

Wakurya bwana.....
Wanaume ni balaaa......
Wanawake ni kasheshe.........
Dawa ni kuwaacha waoane wenyewe kwa wenyewe ili wapigane mapanga hiyo ndio raha yao.

Ugomvi ni wa kabila gani?
na ni kabila gani lisilokua na "tatizo " kwa mtazamo wako?
naona mnge discuss topic kama tukio na sio topic kama ukabila,....
kila kabila tunasikia mambo yao kibao ila tu basi hatuoni umuhim
wa kuyatilia maanani maana ni upuuuzi ku-discuss kwamba kabila flan ni hovyo kwa
haya na haya,.......

Taja kabila lako hapa uone lilivo safi mkuu

Mwanamke gani huyo anaenda kunywa pombe halafu anasinhgizia kuwa eti alikuwa hospitalini?

RIP mbaba uliyejinyonga!... Daaah! Upendo ulizidi kwa mkewe!.. Attachment ilkuwa kali akashindwa kumwacha aokoe roho yake... Haya sasa amejinyonga, mwezie kabaki!

Ugomvi ni wa kabila gani?

na ni kabila gani lisilokua na "tatizo " kwa mtazamo wako?

naona mnge discuss topic kama tukio na sio topic kama ukabila,....

kila kabila tunasikia mambo yao kibao ila tu basi hatuoni umuhim

wa kuyatilia maanani maana ni upuuuzi ku-discuss kwamba kabila flan ni hovyo kwa

haya na haya,.......

Taja kabila lako hapa uone lilivo safi mkuu

well said :)

Back
Top Bottom