Maria Roza
JF-Expert Member
- Apr 1, 2009
- 6,797
- 1,567
MWANAFUNZI Simon Joseph (15), aliyechaguliwa katika awamu ya pili kujiunga na kidato cha kwanza katika Shule ya Sekondari ya Kata ya Iyela, amejinyonga hadi kufa akipinga mama yake kuikimbia familia na kwenda kuolewa na mwanamume mwingine.
Inadaiwa mwanafunzi huyo alifikia uamuzi huo akipinga mama yake kuolewa na mwanamume mwingine na yeye kuchoshwa na kubeba mzigo wa kuwahudumia wadogo zake, ambao alikuwa akiwapikia pamoja na huduma nyingine za kawaida za nyumbani.
Akizungumzia tukio hilo, Diwani wa Kata ya Iyela katika Halmashauri ya Jiji la Mbeya, Ambakisye Mwasumbi alisema tukio hilo lilitokea juzi saa tano asubuhi nyumbani kwa familia ya mwanafunzi huyo eneo la Airport.
Alisema inadaiwa kabla ya kujinyonga, Simoni aliwaambia wadogo zake kuwa amechoshwa na adha ya kuwalea baada ya mama yao Esther Yona kuwakimbia na kuolewa na mwanamume mwingine; akidaiwa alisema ni afadhali afe.
Alisema inadaiwa wadogo zake watatu walijaribu kumzuia na kumshauri asitimize azma hiyo, lakini aliwatisha kuwachoma kwa kisu alichokuwa amekishika, ndipo baada ya kutishiwa walikimbia na kumwacha peke yake.
Aidha, Mwasumbi alidai kuwa baada ya wadogo zake kukimbia na kumwacha peke yake, kijana huyo alitoka nje na kupanda juu ya mwembe uliopo nyumbani kwao na kujinyonga kwa kutumia waya wa simu za TTCL.
Diwani huyo alidai wadogo zake walimuona alipopanda kwenye mwembe na kujirusha, ambapo walipiga kelele za kuomba msaada, lakini hadi watu wanafika kutoa msaada alikuwa amekwishafariki.
Mume wa Esther aliyetambuliwa kwa jina moja la Joseph, alishindwa kuzungumza lolote ambapo inadaiwa tangu akimbiwe na mkewe ni miezi miwili imepita na kwamba alikwishatoa taarifa kwenye uongozi wa Serikali ya Mtaa.
Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Advocate Nyombi hakupatikana kuthibitisha tukio hilo, ambapo ilidaiwa na Katibu Muhtasi wake kuwa yupo kwenye kikao cha siku nzima na hivyo hawezi kuonana na waandishi wa habari.
Simon alikuwa aanze masomo ya kidato cha kwanza Machi 15, mwaka huu katika Shule ya Sekondari ya Kata ya Iyela ambapo inadaiwa baba yake alikuwa tayari ameshamfanyia maandalizi yote ya shule
http://bongoyetu.com/the-news/468-ajinyonga-kupinga-mama-yake-kuolewa-kwingine.html