Ajinusurisha polisi kwa kujeruhi mke kwa wivu wa kimapenzi

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
54,363
58,385
Ajinusurisha polisi kwa kujeruhi mke kwa wivu wa kimapenzi
5530470.jpg

Friday, March 18, 2011 10:38 AM
KIJANA mmoja jina kapuni [34] mkazi wa Yombo amejinusurisha kituo cha polisi baada ya kumjeruhi mke wake kutokana na sababu za wivu wa kimapenzi.Chanzo cha habari hii kilidai kuwa, kijana huyo alimjeruhi mke wake baada ya kumuhisi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwenye nyumba wao.

Ilidaiwa kuwa, jana majira ya saa 2 usiku mume huyo alikuwa akianza kumfokoe mke wake na hatma yake alijikuta kumpiga na kumjeruhi maeneo yake ya usoni kutokana na jazba na hasira ya kuhisi kuibiwa mke wake.

Ilidaiwa kuwa, mara baada ya kuona amejeruhi kijana huyo alichomoka ndani kwake na kukimbilia kituo cha polisi kilichokuwa karibu nao kuripoti tukio hilo.

Majirani waliokuwa karibu nao walikimbilia ndani humo na ndipo mwanamke huyo alibainisha kuwa alikuwa amempigwa na chupa ya soda kutokana na hasira za kuhisiwa anatoka nje ya ndoa.

Mwanamke huyo alibainisha kuwa “mume wangu ananihisi kuwa nina mahusiano na baba mwenye nyumba, kutokana na kutukuta mara kwa mara tukiongea na kuchangamkiana ndipo alikuwa akidhani kuwa ni mpenzi wangu”

Ilidaiwa kuwa mwanamke huyo alifafanua kuwa alikuwa na ukaribu na mwenye nyumba hiyo kwa kuwa alikuwa ni kabila moja na alikuwa akimuona kama kaka yake kutokana na kuongea lugha moja.
 
Duh Hii kali, hicho kikwao jamaa alikuwa hakielewi nini?
 
Back
Top Bottom