Ajari ya Mtoto Mdogo Nchini China Ni Anguko la Ujamaa wa Kichina Kwishey

DSN

JF-Expert Member
Feb 2, 2011
2,837
1,674
Ajari ya kugongwa kwa Mtoto Mdogo Nchini China ni moja ya dalili ya kuanguka kwa Ujamaa wa china ambao uliwafanya kuishi kama jamii moaja.Mtoto huyo Mdogo aliyegongwa na Magari Mawili na kupitwa na wapita njia watano pasipo kati yao wote hao kutoa msaada ni moja ya picha ya anguko la ujamaa wa kikomunist wa china na kuzalisha watu wakatili hata kwa watoto wadogo.

Tizama picha hiyo inayotia simanzi vibaya nina hakika jambo hilo lingetokea kwenye ardhi ya Marekani au Uingereza haya yasingeonekana kuwa mtoto aliyegongwa kupitwa na magari kadha na watembea kwa miguu bila msaada.Pamoja na kuwa Mataifa hayo watu wake hawakulelewa kwenye mazingira ya ujamaa lakini wanajali kwenye jumuhiya zao.

Jamani hiyo ndiyo China Ya Leo.[video=metacafe;yt-wo0_Yup17yc/tragic_accident_at_foshan_guangdong/]http://www.metacafe.com/watch/yt-wo0_Yup17yc/tragic_accident_at_foshan_guangdong/[/video]
 
Tabia au hulka za mtu hazihusiani na mfumo wa nchi wa uchumi.

Kwanini Nyerere watanzania wanataka aigwe tabia zake?Kwanini kiongozi anakumbwa na kashfa binafsi uko ulaya anafukuzwa au anajiuzuru?
 
Kwa hiyo tabia za Nyerere zilibadilika alipoamua kuachia ngazi? Kama hazikubadilika si angeendelea tu? Tabia binafsi za hao viongozi wa Ulaya zinahusiana vipi na mfumo wao wa uchumi?
 
Dah! aise.. inasikitisha kwa kweli.
Hiyo ndiyo china ya sasa ambayo utu kwao si deal tena kila mtu kivyake vyake,Ukomnisti ni mfumo ambao unawalakini.
 
Ajari ya kugongwa kwa Mtoto Mdogo Nchini China ni moja ya dalili ya kuanguka kwa Ujamaa wa china ambao uliwafanya kuishi kama jamii moaja.Mtoto huyo Mdogo aliyegongwa na Magari Mawili na kupitwa na wapita njia watano pasipo kati yao wote hao kutoa msaada ni moja ya picha ya anguko la ujamaa wa kikomunist wa china na kuzalisha watu wakatili hata kwa watoto wadogo.

Tizama picha hiyo inayotia simanzi vibaya nina hakika jambo hilo lingetokea kwenye ardhi ya Marekani au Uingereza haya yasingeonekana kuwa mtoto aliyegongwa kupitwa na magari kadha na watembea kwa miguu bila msaada.Pamoja na kuwa Mataifa hayo watu wake hawakulelewa kwenye mazingira ya ujamaa lakini wanajali kwenye jumuhiya zao.

Jamani hiyo ndiyo China Ya Leo.[video=metacafe;yt-wo0_Yup17yc/tragic_accident_at_foshan_guangdong/]http://www.metacafe.com/watch/yt-wo0_Yup17yc/tragic_accident_at_foshan_guangdong/[/video]

Tusisingizie Ucommunist, hiyo ni tabia mbaya tuu, ambayo inamfanya binadamu kuwa kama shetani, !! Kwani hata siwezi kumlinganisha na mnyama , maana hata ng'ombe angepita hapo akikuta damu ya ng'ombe mwenzake huwa anapiga kelele sana!! na kuchimbua ardhi. Kama huamini mpitishe ng'ombe machinjioni utasikia kilio chake. Nafikiri Hiyo tabia imepita kiwango cha UTU wala Unyama. MUngu amponye huyo mtoto.
 
Kwa hiyo tabia za Nyerere zilibadilika alipoamua kuachia ngazi? Kama hazikubadilika si angeendelea tu? Tabia binafsi za hao viongozi wa Ulaya zinahusiana vipi na mfumo wao wa uchumi?

Leo hii unalia na taifa lako kuwa limekuwa maskini kumbe nini kama sio tabia za viongozi wako kujilimbikizioa mali kisha kuwaacha nyie maskini.Ndio maana kuna kuwa na maadili ya Viongozi na maadili ya Umma.Utakuwaje na Kanuni za Maadili ya Viongozi au Umma kama una swala la Tabia.Maana ya kuwa na Maadili ni kitu kinachohusu tabia.Ludi Class Mkuu.
 
Tusisingizie Ucommunist, hiyo ni tabia mbaya tuu, ambayo inamfanya binadamu kuwa kama shetani, !! Kwani hata siwezi kumlinganisha na mnyama , maana hata ng'ombe angepita hapo akikuta damu ya ng'ombe mwenzake huwa anapiga kelele sana!! na kuchimbua ardhi. Kama huamini mpitishe ng'ombe machinjioni utasikia kilio chake. Nafikiri Hiyo tabia imepita kiwango cha UTU wala Unyama. MUngu amponye huyo mtoto.

Mkuu china ni noma kweli,Nchi zote zilizokuwa za kikomunist leo hii Nchi hizo watu wake ni wakatili kinoma fuatilia misuko suko ya Waromania au Warusi jamaa hao ni watata kwenye jamii si kidogo.Mtu aliye lelewa kuwa anawajali wengine ukimuondolea maadili uwa anaendekeza unyama mara mbili ya mtu mwingine.Ndio maaana mtu kutoka shamba akiingia mjini anakuwa much know kinoma.Hii iko wazi.
 
Leo hii unalia na taifa lako kuwa limekuwa maskini kumbe nini kama sio tabia za viongozi wako kujilimbikizioa mali kisha kuwaacha nyie maskini.Ndio maana kuna kuwa na maadili ya Viongozi na maadili ya Umma.Utakuwaje na Kanuni za Maadikli ya Viongozi au Umma kama una swala la Tabia.Maana ya kuwa na Maadili ni kitu kinachohusu tabia.Ludi Class Mkuu.
Mtaalam nadhani kuna mahala hatujaelewana. Katika maelezo yako kwenye thread umeonyesha kuwa kitendo cha hao Wachina kumpita huyo mtoto bila msaada kimetokana na ujamaa kuisha na kwa maana hiyo unamaanisha kitendo kile pengine kimetokana na ubepari. Hapo hapo unawasifu mabepari (Wamarekani na Waingereza) kuwa kama ingekuwa wao wangemfanyia yule mtoto utu. Tayari hapo kuna contradiction.
Nilichosema mimi nilimaanisha kuwa bila kujali ujamaa au ubepari tabia za watu ni aidha nzuri au mbaya. Hapa nazungumzia "morals" na "manners" kati ya binadamu na binadamu. Hizi hazijengwi na mifumo ya uchumi. Kama ungezungumzia kwa minajili ya dini au imani pengine mada ingekuwa tofauti. Sina ugomvi na wewe, tunaeleweshana tu ingawa umenihimiza nirudi shule.
 
Mkuu naona ujaweza kutambua kuwa Tiafa linajengwa kupita tabia,Wachina leo sio mabepari na wala sio wakomunisti bali wapo wapo tu sio ndege wala sio popo wameacha ukomunist wamedandia kutaka kuwa mabepari lakini kumbe ubepari ni mfumo ambao nao una kanuni zake hivyo kuzidandia pasipo kujenga misingi unaunda unyangau.China leo watu wanaona imeendelea kwa kwa kuwa ilipewa teknolojia kiduchu na mmarekani sasa mmrekani kafunga teknolojia anasema viwanda vyote vya wamarekani vilivyokuwa nje ya marekani viluid Nchi Marekani kauri ya Obama [Obama's Job Speech 2011] tayari kizaaza kimeanza mara ghafla uchumi wa Chiana umeeanza kuyamba na toka speech hiyo ni miezi miwli tu.

Kuacha asili ni kupotea ni kama sisi tumeacha asili leo hii sisi si wajamaa wa kiaafrika na wala si Mabepari tupo tupo.
 
Back
Top Bottom