Ajali za mabasi Tanzania yazua gumzo Canada!

Chanzo Kikubwa cha ajali ni sisi Wenyewe!! Unaweza Kuamua kumkomalia dereva ili apunguze Overtaking za kizembe ila raia (Wasafiri wengine) wanakuona kama zuzu au Mshamba au Unapenda sana kuishi!! Shida kubwa ni serekali kuwa na blabla nyingi!! Haijui hata inasimamia nini? Ukichukua Tathimini halisi unaweza kukuta ajali za Mabasi kwa mwaka husababisha vifo vya watu 700; Ila Usafiri wa pikipiki kwa kipindi Hichohicho utakuta wamekufa watu 1,400!! Huoni kwa hali hii ni kuwa serekali imepoteza mwelekeo na Haijui Inachosimamia!!!
 
Mtapiga kelele lakini hakuna atakayewasikiliza. Hivi mtu mzima ambaye ana familia anapoamua kuwapa Majembe Auctions jukumu la usalama kwenye barabara zetu wakati hiyo kampuni hawaelewi hata chembe kuhusu usalama barabarani mnategemea nini?

Hakuna chombo ambacho kipo makini kusimamia, wenzetu wanasema Highway Code, dereva anaua tena kwa makusudi unamkuta kesho yupo barabarani anaendesha. Dereva anakunywa pombe au kutumia unga unamkuta yupo barabarani. Hakuna chombo huru ambacho kinasimamia maslahi ya watanzania. Chama Cha Majambazi ambacho kiliiba kura kitaendelea kuua Watanzania hadi pale watakapozinduka kutoka kwenye usingizi wa pono. Si mmesikia watu walivyouawa kule Songea, si tayari hakuna kesi itakuwa ajali sisi tuendelee tu kuwashadidia makahaba waendeleze libeneke lao.
 
Wana JF leo nilikuwa katika mmoja ya Mikutano nchini Canada. Katika kujadili masuala ya husuyo Tanzania na bila kufahamu kama walikuwemo wa-TZ ndani ya Mkutano ule uliokuwa unazungumzia Utalii Afrika, mzungu mmoja kutoka USA akaamka na kusema wazi mbele ya kikao kuwa .. jamani muendapo Tanzania msipande mabasi yatokayo Arusha/Moshi kwenda Dar... mtakufa na mtakuja kusahauliwa na familia zenu. Ametoa ushuhuda alivyosafiri na basi toka Arusha kwenda Dar bila kutaja basi ya Kampuni ipi na kusikitika alivyozomewa na abiria waliokuwemo ndani ya basi hilo. Abiria walimtaka ashuke kama yeye anaogopa kufa na walimwambia wao wanaharaka na wanataka kufika Dar mapema. Mzungu anasema ilibidi anywe wine/POMBE ili alewe na asijue kinachoendelea hadi alipofika Ubungo na kuashwa na Girlfriend wake.

Alitoa takwimu za ajali Tanzania na inavyo claim maisha ya watu huko TZ.

Nilijaribu kuomba nafasi nikapata na nikatoa blaa blaa ninazozijua ili angalau kutetea nchi yangu.Maswali yalikuja kama nyuki...

USHAURI: Kwanza ni aibu kwa Taifa kushindwa kupunguza ajali zisizo za lazima kama hizi za barabarani.Pili, pato kubwa la Taifa linatokana na utalii, mambo kama haya yatachangia kupunguza mapato ya Serikali..

Sitaki kuzungumza mambo mengi lakini mnaweza changia nini kifanyike, wafukunyungu watazipeleka kwa JK.

Thanks.

Mkuu hayo unayoyasema ni yakweli, swali linakuja Je Tanzania kuna Serikali? na Jibu Hakuna Serikali bali kuna genge la Wahuni ndio wanaoongoza nchi kwa mabavu. Kama kungekuwa na Serikali Tanzania Mifumko ya bei ya Vyakula, Mafuta kuchakachuliwa, Ajali za barabarani, matatizo ya Wananchi waliyokuwa nayo, Ufisadi, Wizi wa mali za umma na matatizo mengine yanayosumbua taifa Yangedhibitiwa na sheria zingefuatwa bila ya kujali cheo au kiongozi wote tungebanana kwenye sheria. Tatizo kubwa Tanzania haina Serikali bali kuna wahuni wanaendesha nchi kihunihuni na sisi Walalahoi ndio wakulaumiwa kwa ujinga na upumbavu wa kuwaogopa wahuni kwa kuto kuwatoa au kuwafukuza kinguvu.
 
Chanzo halisi cha ajali Tanzania ni Mirungi, Bangi, TRAFFIC POLICE, Valeur, Ufinyu wa barabara na usimamizi mbovu wa sekta ya usafiri

Uko sawa kabisa; Kuna rafiki yangu ni dreva wa magari, alikuwa habwii ugoro, kuba, alijiriwa kuendesha mabasi hiyo tabia ikaanzia huko.
Anadai asilimia kubwa ya madereva wa mabus hawezi endesha bus bila kuwa n a kileo kichwani wapo wanavuta bangi wanywa gogo kubwia mirungi kuba n.k
yeye anabwia ugoro sababu kuba ni aghari na adimu.
Basi kila stand ya mabus Kuna police traffic, wapowapo tu, wapewe kipima pombe
na drugs, sidhani km Kuna driver atakunywa pombe kabla ya safari.
 
Issue iko kwako na kwangu je dont we contribute kutokea kwa izo ajali.
Uko kwa gari na dreva anamiss behave unakaa kimyaa.
Kuna dreva wa NEW FORCE alimis behave nikampigia mmiliki dreva alishika discipline ingawa kutukomoa akaanza endesha kama kinyonga.
Naona kazi tunayo
 
Labda ingewekwa time limit ya basi kutoka point A mpaka B.
Pia kuwe na check points barabarani ku check muda.
Mabasi ya railways yalikuwa na system hizo na ajali zilikuwa ndogo.
Mfano upo iringa unataka kwenda mbeya unajua basil litafika saa ngapi kutoka Dar.
Madereva wakiwahi kufika wanapata matatizo.
 
Sana sana hiyo utawaongezea ma Traffic police bakshish basi, hamna lolote watakuwa wanachukua hela kwa kila basi halafu wanajidai hawaoni.
 
Kuna mzungu mmoja aliniambia nchini kwao wakati mtu anasafiri kuja afrika anapewa briefing ya nchi hatari sana kiusalama katika afrika ambazo ziko lebelled red,ya kwanza ikiwa Somalia ikfuatiwa na Nigeria na Tanzania aliniambia inatajwa nchi ya nane,nilimuuliza ni vigezo gani wanatumia kwani nchi yetu ni kati ya nchi salama kabisa Afrika,alinjibu ni kwa sababu ya ajali za barabarani kwamba inaongoza Afrika kwa vifo vya ajali.Kweli nilielezwa ilo about three years ago lakini hadi leo bado nalitafakari.
 
Mkuu JAPUONY nadhani hauna uzoefu wa kusafiri ktk njia ya Arsh-Moshi-Dsm maana ungeweza toa maelezo ambayo kwa kiwango fulani yangesaidia wajumbe wa kikao. Wenzangu wameeleza matatizo mengi yanayoikabili sekta ya usafirishaji ktk Tanzania. Na mimi nakubaliana nao. Nyongeza ni kwamba kwa wasafiri wazoefu wanafahamu mabasi ya makampuni gani yanakimbizwa mwendo kasi na kusababisha ajali kila siku. Ni jukumu la mawakala wa Kampuni za Utalii na Serikali kuweka matangazo ya tahadhari kwa wageni/watalii wanapoingia ingia nchini. Kwa hiyo wengi upanda mabasi hayo kwasababu hawana taarifa yoyote. Pili wazungu wengi wanaotoka Arusha na Moshi kwenda Dsm huwa wanataka kuwahi boti za Zanzibar. Kwa hiyo unakuta wenyeji wao wanawakatia tiketi za mabasi ya mwendo wa kufa mtu!
 
ili kupunguza kama si kuondoa kabisa janga hili, yatupasa tufanye yafuatayo:
  • kupanua barabara kuu
  • kujenga barabara mbili mbili, ya kwenda na kurudi.
  • kuangalia sheria za barabarani ikiwamo utoaji leseni, bima kwa wafanyabiashara za usafiri wa abiria, adhabu kwa wanaosababisha ajali, adhabu kwa kampuni. Kama inakidhi hali halisi iliyopo.
  • kuangalia upya biashara nzima ya usafirishaji, nafikiri kampuni ya usafirishaji yoyote isiwe ya mtu mmoja, bali iwe ni ya watu kadhaa wenye hisa, na yenye bodi ya wakurugenzi ambao wanakuwa na majukumu ya kusimamia uendeshaji wa kampuni, hii itasaidia kuweka uwajibikaji. Hapa tuanahitaji kutunga sheria ambayo itaanisha vigezo hivi vya kamuni ya usafirishaji. Pendekezo hili ni gumu kufanyika, lakini mimi naamini kuwa itasaidia sana katika kudhibiti uzembe, kuboresha maamuzi na uwajibikaji. Kwa mfumu uliopo sasa wa kuwa mtu anaweza kumiliki kampuni yake, naona unashusha uwajibikaji na inaongeza uzembe. Ofcourse, uchumi wetu ni wa kibepari lakini naona linapokuja suala la uhai wetu, tusifungwe na kanuni hizi za kiuchumi.
  • abiria wenyewe tutoe ushirikiano katika kudhibiti ukiukwaji wa sheria barabarani, mf. Kama gari limejaa kwanini ulazimishe kupanda? Dereva anaenda mwendo wa kawaida, kwanini umshurutishe awahi, ama anaenda kasi kwanini usitoe onyo?
  • tuendeleze njia mbadala za usafiri, njia kubwa ya usafiri ni reli, tutandaze mtandao wa reli nchi nzima, nchi nyingi zilizoendelea, na zinazoendelea mf china, wanatumia reli kama njia kuu ya usafiri, kwa siku kunaweza kuwa na treni 10 zinaenda mji mmoja. Kama tukiboresha njia hizi mbadala, tutawezesha ushindani wa kibiashara, jambo ambalo litahamasisha uboreshaji wa huduma, ikiwapo pamboja na usalama wa abiria.
  • mwisho, si kwa umuhimu, jeshi la polisi liwe na uzalendo, askari unaona basi lina tairi kipara, lakini unaliacha liende na safari, au umegundua lina kasoro fulani, unatoza faini halafu unaliacha liendee na safari, mi naona bora abiria wakwame na safari kuliko kuchinjwa. Jeshi la polisi lijirekebishe, ili kurudisha imani ya jamii kwao.

inahitaji uwezo wa ziada wa dereva kuendeshe kwenye barabara hizi
 
Elimu ya usalama barabarani itolewe zaidi na zaidi na wajibu na haki ya wasafiri/abiria zifundishwe pia. Mfano:, mabas yana seat belts,je ni abiria wangapi huwa wanafunga wakiwa safarini!? Ofkoz hii iliwahi nishangaza siku moja nlipo mpa trafik polis mmoja liftj,nlipomwambia "afande funga mkanda" yeye alijibu "AAAH..,MIMI TENA? NANI ATANIKAMATA?" Hapa kuna tatizo na tusitegemee hao tunaowategemea kuwa ndo wataliondoa manake kumbe hata wao hawajui nini wanafanya.niliwahisoma maneno ya Marcus Moziah Garvey akisema ; "where there is poverty there is no respect of law,authority or human life". Pengine umaskin wetu ndo unatufanya tuwe wajinga kias hiki.., au pengine ni ujinga wetu?
 
Mbali na hayo yote yaliyochangiwa, pia tunapashwa kujikabidhi mikononi mwa Mungu kila tunapoanza safari zetu. Tukumbuke pia kuna mambo mengi sana njiani mbali na yaliyo yanasababisha ajali pia.

Nakubali madereva wengi ni wazembe na walevi ila si vibaya pia kila mtu akawa anamwomba Mungu kwa imani yake ili roho za ajali zituepuke.
 
Nikweli sina uzoefu wa njia ya Arsha - Dar lakini ndg yangu nilipata AIBU kujitangaza kuwa mie Mtanzania. Nadhani ningekuwa Mtumishi wa Serikali ningekuja niandike ripoti mbaya sana kwa wakubwa zangu ambayo najua wasingefanyia kazi ila ujumbe ungefika. Kweli ni aibu, tushindwe kuzuia UKIMWI na hata ajali za barabarani...!!!!!!!!
 
Hapa waongea ujinga wazungu Wanapenda bure na rahisi na Ndo kitu kinachowaponza acha ukenge.

QUOTE=JAPUONY;3422924]Wana JF leo nilikuwa katika mmoja ya Mikutano nchini Canada. Katika kujadili masuala ya husuyo Tanzania na bila kufahamu kama walikuwemo wa-TZ ndani ya Mkutano ule uliokuwa unazungumzia Utalii Afrika, mzungu mmoja kutoka USA akaamka na kusema wazi mbele ya kikao kuwa .. jamani muendapo Tanzania msipande mabasi yatokayo Arusha/Moshi kwenda Dar... mtakufa na mtakuja kusahauliwa na familia zenu. Ametoa ushuhuda alivyosafiri na basi toka Arusha kwenda Dar bila kutaja basi ya Kampuni ipi na kusikitika alivyozomewa na abiria waliokuwemo ndani ya basi hilo. Abiria walimtaka ashuke kama yeye anaogopa kufa na walimwambia wao wanaharaka na wanataka kufika Dar mapema. Mzungu anasema ilibidi anywe wine/POMBE ili alewe na asijue kinachoendelea hadi alipofika Ubungo na kuashwa na Girlfriend wake.

Alitoa takwimu za ajali Tanzania na inavyo claim maisha ya watu huko TZ.

Nilijaribu kuomba nafasi nikapata na nikatoa blaa blaa ninazozijua ili angalau kutetea nchi yangu.Maswali yalikuja kama nyuki...

USHAURI: Kwanza ni aibu kwa Taifa kushindwa kupunguza ajali zisizo za lazima kama hizi za barabarani.Pili, pato kubwa la Taifa linatokana na utalii, mambo kama haya yatachangia kupunguza mapato ya Serikali..

Sitaki kuzungumza mambo mengi lakini mnaweza changia nini kifanyike, wafukunyungu watazipeleka kwa JK.

Thanks.[/QUOTE]
 
Takwimu zinaonesha ajali safari zinaua zaidi ya ukimwi, nyuma ya malaria.
ni mada sensitive sana. lakini inapozungumziwa maisha ya watu Tz, nobody anajali. Sijui why,ila naona uhai hauthaminiwi kabisa bongo as if tuna 2nd chance.Tunajua vifo vingi vinavyosababishwa na mwendo kasi,utajiuliza wapi speed gavanor? mbona hatusikii zikikaguliwa tena? utajiuliza kwanini zisiwekwe camera barabarani,je ni expensive kuliko uhai wetu? police anakamata gari linaenda kasi au bovu au dereva hana leseni,anamuachia kwa rushwa ya 5000tsh,je uhai wetu hauna thamani kiasi hicho? Ujinga wetu pia unasababisha hayo,kama huyo mzugu alivyosema,watanzania wanashangilia mwendo kasi,wanataka kuwahi ikitokea ajali ndio wanamlaumu dereva.Tuchukue hatua,hakuna haja ya kufanya utafiti au kuwasilisha mapendekezo serikalini.sisi tukatae madereva au magari yanayohatarisha uhai wetu
 
The only people can change the systems is us... We need to act now and not to wait for the un known Government which can't act...

I agree with you 100%. Yes we have rough and reckless drivers, what is the role of passengers whose lives are in danger? Keeping silence and wait for the accidents to occur and be witness........ (if they are lack enough to be alive).
 
ni mada sensitive sana. lakini inapozungumziwa maisha ya watu Tz, nobody anajali. Sijui why,ila naona uhai hauthaminiwi kabisa bongo as if tuna 2nd chance.Tunajua vifo vingi vinavyosababishwa na mwendo kasi,utajiuliza wapi speed gavanor? mbona hatusikii zikikaguliwa tena? utajiuliza kwanini zisiwekwe camera barabarani,je ni expensive kuliko uhai wetu? police anakamata gari linaenda kasi au bovu au dereva hana leseni,anamuachia kwa rushwa ya 5000tsh,je uhai wetu hauna thamani kiasi hicho? Ujinga wetu pia unasababisha hayo,kama huyo mzugu alivyosema,watanzania wanashangilia mwendo kasi,wanataka kuwahi ikitokea ajali ndio wanamlaumu dereva.Tuchukue hatua,hakuna haja ya kufanya utafiti au kuwasilisha mapendekezo serikalini.sisi tukatae madereva au magari yanayohatarisha uhai wetu

ajali ya train iliyotokea Mpwapwa na kuua more than 800 people, nilikuwa a mwanafunzi nje ya Tanzania. Sikujua kama kuna ajli kama hiyo. Prof wangu alinifuata na kuniuliza: hivi viongozi wa Africa wanajali maisha ya raia wao? Nikamuuliza why? akanionyesha gazeti lilioandikwa ile habari. Nilibaki mdomo wazi, sikuwa na la kumjibu.:A S embarassed::shock:
 
Wana JF leo nilikuwa katika mmoja ya Mikutano nchini Canada. Katika kujadili masuala ya husuyo Tanzania na bila kufahamu kama walikuwemo wa-TZ ndani ya Mkutano ule uliokuwa unazungumzia Utalii Afrika, mzungu mmoja kutoka USA akaamka na kusema wazi mbele ya kikao kuwa .. jamani muendapo Tanzania msipande mabasi yatokayo Arusha/Moshi kwenda Dar... mtakufa na mtakuja kusahauliwa na familia zenu. Ametoa ushuhuda alivyosafiri na basi toka Arusha kwenda Dar bila kutaja basi ya Kampuni ipi na kusikitika alivyozomewa na abiria waliokuwemo ndani ya basi hilo. Abiria walimtaka ashuke kama yeye anaogopa kufa na walimwambia wao wanaharaka na wanataka kufika Dar mapema. Mzungu anasema ilibidi anywe wine/POMBE ili alewe na asijue kinachoendelea hadi alipofika Ubungo na kuashwa na Girlfriend wake.

Alitoa takwimu za ajali Tanzania na inavyo claim maisha ya watu huko TZ.

Nilijaribu kuomba nafasi nikapata na nikatoa blaa blaa ninazozijua ili angalau kutetea nchi yangu.Maswali yalikuja kama nyuki...

USHAURI: Kwanza ni aibu kwa Taifa kushindwa kupunguza ajali zisizo za lazima kama hizi za barabarani.Pili, pato kubwa la Taifa linatokana na utalii, mambo kama haya yatachangia kupunguza mapato ya Serikali..

Sitaki kuzungumza mambo mengi lakini mnaweza changia nini kifanyike, wafukunyungu watazipeleka kwa JK.

Thanks.

Miundombinu ya mkoloni haiwezi kidhi mahitaji ya sasa ya usafiri.
 
Barabara hizo hazijengwa na Mkoloni, zimejengwa na wa TZ!Mabasi tumenunua sisi siyo wakoloni.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom