Ajali ya ubungo riverside; maoni ya shuhuda

Kitomai

JF-Expert Member
May 21, 2009
1,061
281
Nini kifanyike kupunguza ajari za barabarani zinazosababishwa na mwendo kasi? Jamii yetu sasa imekuwa ikishuhudia ajari ambazo zinasababisha vifo visiyo rasimi na kuwaacha maelefu wengine wakipatwa na ulemavu. Awali ya yote nikusimulieni nilichokiona katika ajari iliyotokea hapo riverside tarehe 23 Jumatano majira ya mchana.

Nikiwa nimesimama pembeni ya barabara eneo la Ubungo Riverside nasubiri nivuke upande wa pili ili nichukuwe usafiri wa daladala nikiwa naelekea Mwenge. Mara nikaona lori aina ya Mercesdes Benz tanker lenye tela lenye nambari za usajili T264BUC likija kwa kasi kama ilivyokawaida ya magari hayo kwenda mwendo kasi baada ya kuruhusiwa kutoka katika mataa ya Ubungo pamoja na kwamba hapo kuna vibao na alama elekezi zilizowekwa kwa ajili ya kuwaongoza madereva wakiwa katika eneo ilo wanapaswa mwendo gani.

Alama kama michoro ya punda milia ipo mita chache karibu na kituo cha daladala cha Riverside. Basi hilo lori likiwa katika mwendo kasi amadi dereva wa daladala akawa anaondoka kituoni na kuingia barabarani ndipo huyo dereva wa lori katika kuhofia kuwa angeweza kuingia ile Hiace kwa nyuma akapanda tuta linalotenganisha barabara.

Baada ya kulipanda tuta, lori likagonga kigingi au jiwe kubwa kisha likawagonga vijana wawili (Maaarufu kama Wamachinga) mmoja alikuwa anauza sticers na mwingine alikuwa amebeba DvD/VCD na Cd, kisha likaanza kuyagonga magari yaliyokuwa upande wa pili wa barabara moja baada ya lingine kwa haraka haraka nilivyoyahesabu yalifika sita lakini mawili aina ya Honda salon yenye nambari za usajiri T918BUC na Toyota Mark II nyeupe yenye namba za usajiri T133ADC yalikuwa yamefanywa chapati (tazama picha).

Shughuli za uokozi zikaanza kwanza kupitia raia wema baadaye polisi wakawasili kutekeleza majukumu yao. Hapa napo nilishuhudia mapungufu makubwa lakini kwa kuwa nataka kuzungumzia kinga ni bora kuliko tiba sito ongelea hilo la shughuri za uokozi Sheria za barabarani zipo lakini nani mwenye jukumu la kuzisimamia?

Nani mhusika nambari moja, namba mbili na nambari tatu? Nambari moja bila shaka ni polisi wa usalama barabarani. Swali la msingi hawa polisi wa usalama barabarani wanafanya kazi yao sawasawa? Ripoti ya Jaji Warioba imewatuhumu hawa polisi wa usalama barabarani kuwa ni wala rushwa wakubwa.

Mapendekezo yangu kazi hii wapewe MP wa JWTZ kwa sababu hivi sasa hakuna vita hivyo hawana kazi nyingi kama wakati wa vita. Wewe una maoni gani katika hii hoja ya kwamba wapewe wanajeshi tuone matokeo yatakuwa vipi.

Nawakilisha hoja.
 

Attachments

  • askali 1.jpg
    askali 1.jpg
    35.9 KB · Views: 178
  • Honda.jpg
    Honda.jpg
    43.1 KB · Views: 173
  • honda  1.jpg
    honda 1.jpg
    36.9 KB · Views: 148
  • IMG00227-20111123-1400.jpg
    IMG00227-20111123-1400.jpg
    38.9 KB · Views: 146
  • IMG00228-20111123-1400.jpg
    IMG00228-20111123-1400.jpg
    42.9 KB · Views: 149
  • IMG00230-20111123-1402.jpg
    IMG00230-20111123-1402.jpg
    39.2 KB · Views: 132
  • IMG00232-20111123-1437.jpg
    IMG00232-20111123-1437.jpg
    42.8 KB · Views: 132
  • mark II.jpg
    mark II.jpg
    37.8 KB · Views: 151
  • IMG00252-20111123-1513.jpg
    IMG00252-20111123-1513.jpg
    34.1 KB · Views: 130
  • umati2.jpg
    umati2.jpg
    40.4 KB · Views: 127
  • IMG00242-20111123-1446.jpg
    IMG00242-20111123-1446.jpg
    45.1 KB · Views: 138
  • IMG00233-20111123-1439.jpg
    IMG00233-20111123-1439.jpg
    37.7 KB · Views: 127
  • IMG00235-20111123-1443.jpg
    IMG00235-20111123-1443.jpg
    46.3 KB · Views: 146
Du mkuu awali ya yote nawapa pole wale wote waliofikwa na ajali hiyo, pili tunakushukuru ndg Kitomai kwa kutupa habari kwa muda(latest/current) yenye maelezo ya kina yasiyoacha shaka. Hawa madereva sijui wanakuwa wamelewa kweli ubungu ni seheme ya kukimbiza gari mpaka likushinde?
 
Ajali nyingi sana utakuta Daladala linahusika au gali la abiria ya kwenda mkoa yamehusika. Hivi ni kwanini hawa wanaobeba roho za binadamu wengi ndo haohao wanaosababisha ajari.
 
Nini kifanyike kupunguza ajari za barabarani zinazosababishwa na mwendo kasi? Jamii yetu sasa imekuwa ikishuhudia ajari ambazo zinasababisha vifo visiyo rasimi na kuwaacha maelefu wengine wakipatwa na ulemavu. Awali ya yote nikusimulieni nilichokiona katika ajari iliyotokea hapo riverside tarehe 23 Jumatano majira ya mchana.

Nikiwa nimesimama pembeni ya barabara eneo la Ubungo Riverside nasubiri nivuke upande wa pili ili nichukuwe usafiri wa daladala nikiwa naelekea Mwenge. Mara nikaona lori aina ya Mercesdes Benz tanker lenye tela lenye nambari za usajili T264BUC likija kwa kasi kama ilivyokawaida ya magari hayo kwenda mwendo kasi baada ya kuruhusiwa kutoka katika mataa ya Ubungo pamoja na kwamba hapo kuna vibao na alama elekezi zilizowekwa kwa ajiri ya kuwaongoza madereva wakiwa katika eneo ilo wanapaswa mwendo gani. Alama kama michoro ya punda milia ipo mita chache karibu na kituo cha daladala cha Riverside.

Basi hilo lori likiwa katika mwendo kasi amadi dereva wa daladala akawa anaodoka kituoni na kuingia barabarani ndipo huyo dereva wa lori katika kuhofia kuwa angeweza kuingia ile Hiace kwa nyuma akapanda tuta linalotenganisha barabara. Baada ya kulipanda tuta, lori likagonga kigingi au jiwe kubwa kisha likawagonga vijana wawili (Maaarufu kama Wamachinga) mmoja alikuwa anauza sticers na mwingine alikuwa amebeba DvD/VCD na Cd, kisha likaanza kuyagonga magari yaliyokuwa upande wa pili wa barabara moja baada ya lingine kwa haraka haraka nilivyoyahesabu yalifika sita lakini mawili aina ya Honda salon yenye nambari za usajiri T918BUC na Toyota Mark II nyeupe yenye namba za usajiri T133ADC yalikuwa yamefanywa chapati (tazama picha).

Shughuli za uokozi zikaanza kwanza kupitia raia wema baadaye polisi wakawasili kutekeleza majukumu yao. Hapa napo nilishuhudia mapungufu makubwa lakini kwa kuwa nataka kuzungumzia kinga ni bora kuliko tiba sito ongelea hilo la shughuri za uokozi Sheria za barabarani zipo lakini nani mwenye jukumu la kuzisimamia? Nani mhusika nambari moja, namba mbili na nambari tatu?

Nambari moja bila shaka ni polisi wa usalama barabarani. Swali la msingi hawa polisi wa usalama barabarani wanafanya kazi yao sawasawa? Ripoti ya Jaji walioba imewatuhumu hawa polisi wa usalama barabarani kuwa ni wala rushwa wakubwa. Mapendekezo yangu kazi hii wapewe MP wa JWTZ kwa sababu hivi sasa hakuna vita hivyo hawana kazi nyingi kama wakati wa vita. Wewe una maoni gani katika hii hoja ya kwamba wapewe wanajeshi tuone matokeo yatakuwa vipi. Nawakilisha hoja.
Umeeleza vizuri juu ya kilichotokea, swala la lori kuwa kwenye mwendo kasi si chanzo cha hiyo ajali kwa maelezo yako, (Hujui wala hajui kuwa RPM ya lori ilikuwa inasoma ngapi wakati daladala inaingia barabarani kwa ghafla).

Mimi ni dereva mzuri tu, na jana wakati imeletwa hii taarifa ya humu JF mimi nilijua nyuma ya hii ajali lazima kuwe na msaada mkubwa wa dereva wa daladala, maeneo ya ubungo mataa hadi eneo la Hostel ni maeneo ambayo binafsi naamin madereva wa daladala wanavibari halali vya kusabaisha ajali ambavyo ama kwa kufahamu au kutofahamu vimetolewa na Jeshi letu la Polisi (Trafic).

Hakika ni moja ya maeneo ambayo madereva wa daladala wanafanya uvunjaji wa sheria za usalama barabarani kwa uwazi na uhuru kabisa,Imefikia mahala madereva wa njia hiyo wanageuza magari ubungo mataa (wakitokea riverside hufanya UTURN kwenye mataa), ni ujasiri wa namna gani huo kama sio kibali cha kufanya hivyo.

Kuna maeneo mawili ambayo binafsi nikisikia ajali najua ni mipango ya Jeshi la polisi,moja ya maeneo hayo ni Ubungo toka njia panda ya CHUO,ubungo Mataa pande zote mbili toka chuo na kuelekea riverside. Eneo jingine ni kimara mwisho,haya maeneo uhuru wa daladala kuvunja sheria ni mkubwa mno na kama kuna mtu asiyejua atakuwa hataki kujua tu,kimara mwisho kituo cha polisi kipo umbali kwa makadirio ni mita 150 toka eneo ambapo fujo na uvunjaji wa sheria unafanyika.

Mtazamo wangu ni kwamba,hizi ajali zitapunguzwa pale tu ajira ya polisi itapotegemea uwezo wa mtu kichwani na si kuajiri wale waliofail sekondari ndiyo wawe mapolisi,matokeo yake jeshi la polisi hali mbinu hata za kukomesha makosa ya wazi ambayo husababishwa na uvunjanji wa sheria za usalama.
 
Lakin mkuu huo daladala na lori wote walisababisha ajali...lori kwa mwendo kasi sehemu zisizoruhusu kuendesha mwendo kasi uliopendekezwa na daladala kwa kuingia barabarani bila kuhakikisha inamruhusu kuingia.

Kutokana na maelezo ya shuhuda ni wazi daladala alichomekea kwa kujidanganya angeweza kwenda mwendo kasi kuliko mwendo wa lori ambalo tayari lilikuwa barabarani kwa mwendo kasi. ki msingi hapa wote wana makosa. sio lori tu peke yake hata daladala.
huyo dereva wa hilo lori ameshakamatwa?nasikia kampuni inayomiliki hilo lori (DALBIT) ni ya kigogo
 
Acha unazi mkuu, kwa lori lililokuwa kwenye mwendo mdogo lisingeweza panda tuta halafu kwenda huo umbali na kusababisha madhara kama aliyoyaelezea shuhuda. Ni wazi hilo lori lilikuwa mwendo kasi usio wa kawaida na pia hiyo daladala nayo inaweza ikawa ilifanya kosa vilevile
 
Sikubaliani na hoja ya kuwapa JWTZ majukumu ya usalama barabarani wala shughuli yoyote ya usalama
wa ndani wa raia. hawa ndio watasababisha madhara makubwa zaidi.

Kumbuka kwamba JWTZ hawafundishwi sheria za uraia, hivyo hawawezi kusimamia sheria yoyote kwa
uelewa na busara.

Hawa Jamaa wamefundishwa kuua adui, sasa unataka waje kuua wavunja sheria??

Nadhani tatizo kubwa sana liko kwenye usimamizi wa sheria na taratibu tulizojiwekea, uwezo
wa kusimamia sheria na taratibu umevunjika kabisa katika nchi yetu, na sio katika sekta
ya ulinzi na usalama wa raia pekee bali mpaka bungeni kutokana na serikali yetu kukumbatia
rushwa.

Serikali ya CCM imechekacheka na rushwa na sasa imekuwa ni mazalia makubwa sana
ya tatizo hili, rushwa imeharibu kabisa mfumo mzima wa maisha yetu.

Naomba tusisahau hata mara moja kwamba CCM ndio tatizo letu, tuunganishe nguvu
kuwaondoa madarakani.
 
kwa mtazamo wangu kwa mujibu wa ushuhuda huu, chanzo cvha ajali ni daladala iliyoingia barabarani ikitokea kitunoni pasi kuangalia kama kuna gari inakuja toka nyuma. tunawajua daladala hizi huwa zao sana. ingekuwa ni gari ndogo inakuja nyuma labda ingeweza kusimama haraka bila kusababisha madhara makubwa.

kwa upande wa lori, yes itaonekana kuwa alikuwa mwendo wa kasi ndio maana alishindwa kulidhibiti lori lake. bila shaka asingekuwa kwenye mwendo huo wa kasi madhara yangekuwa madogo kuliko ambavyo yamekuwa. ila bado madhara yangetokea kwa aidha kuligonga daladala au kusimama ghafla na labda lenyewe kugongwa kwa nyuma nk.

kwa namna yoyote ile ulitazamavyo hilki suala, kumlaumu dereva wa lori ni katika kuangalia kama madhara yaliyotokea yangeweza kupunguzwa. wa kulaumiwa kabisa kwa kusababisha yote haya ni dereva wa daladala. kama angekuwa makini na kutazama kwenye vioo vyake, ajali hii isingetokea asilani na wala huu mjadala usingekuwepo leo hapa. cha kushangaza, wala dereva wa daladala hazungumziwi kama alikamatwa au yeye ndo alisepa kwa amani ya bwana!
 
Mwendo kasi unaweza kuonekana kwa macho pia. Siyo lazima uwe na kifaa cha kupimia mwendo kasi kujua huu ni mwendo kasi. Unaweza kutumia common sense kujua huu ni mwendo hatarishi au siyo. Na kwa taarifa yako kuna jiwe lilofanyika kama kigingi baada ilo jiwe kugongwa kasi ya hilo gari ilipungua na laiti mwendo usingepunguzwa na hicho kigingi bila shaka madhara yangekuwa makubwa kuliko yalivyokuwa. Lori limeharibu magari saba wewe unasema lilikuwa linatembea mwendo wa pole mwendo wa arusi! Ungekuwepo katika tukio ungeandika kitu tofauti. Kuhusu polisi kufanya vibaya kwa sababu wanaoajiliwa wamefeli fomu 4 hoja hiyo naye ni nyeupe. Angalia safu ya uongozi wa nchi hii jinsi iloivyosheheni wasomi wa vyuo vikuu, madaktari, maprofesa n.pamoja na kusheheni wasomi katika safu ya uongozi hali halisi ya uchumi na huduma za jamii zipo taabani, kuanzia afya, elimu.makaazi,kilimo na ufugaji, rushwa, ufisadi,madini na nishati,nguvu kazi ya taifa vijana ipo under-utilized, sheria na katiba,ni dhahili kabisa hiyo elimu waliyoipata haisadii kupambana na mazingira maana kwangu mimi maana ya elimu ni UWEZO WA KUPAMBANA NA MAZINGIRA au capacity to meet life situations. Kwani kwako nene elimu lina maana gani?
 
Hii barabara ina ajali kuliko maelezo last two months nikiwa kituo cha daladala Gereji (kituo kinachofuata baada ya External ukielekea buguruni) ilikuja daladala la kichina likagonga daladala nyingine mbili! It was terrible, siwezi ku-list idadi ya ajali nilizoshuhudia kwene hii barabara achilia mbali mtu ambaye aligongwa na gari ya polisi pale kati ya Riverside na Ubungo akiwa (Polisi_) kwene wrong side! so hii barabara inatisha!!!!! Nothing more
 
Umeeleza vizuri juu ya kilichotokea, swala la lori kuwa kwenye mwendo kasi si chanzo cha hiyo ajali kwa maelezo yako, (Hujui wala hajui kuwa RPM ya lori ilikuwa inasoma ngapi wakati daladala inaingia barabarani kwa ghafla).

Mimi ni dereva mzuri tu, na jana wakati imeletwa hii taarifa ya humu JF mimi nilijua nyuma ya hii ajali lazima kuwe na msaada mkubwa wa dereva wa daladala, maeneo ya ubungo mataa hadi eneo la Hostel ni maeneo ambayo binafsi naamin madereva wa daladala wanavibari halali vya kusabaisha ajali ambavyo ama kwa kufahamu au kutofahamu vimetolewa na Jeshi letu la Polisi (Trafic).

Bila shaka leseni yako uliletewa nyumbani. Ina maana mtu akitaka kujua kama gari linakwenda mwendo wa kasi ni lazima aangalie RPM yake?? Kama hilo lori lingekuwa kwenye mwendo wa wastani basi lisingeweza kungoa kigingi na kuparamia magari saba kulingana na maelezo ya mtoa taarifa.
 
Bila shaka leseni yako uliletewa nyumbani. Ina maana mtu akitaka kujua kama gari linakwenda mwendo wa kasi ni lazima aangalie RPM yake?? Kama hilo lori lingekuwa kwenye mwendo wa wastani basi lisingeweza kungoa kigingi na kuparamia magari saba kulingana na maelezo ya mtoa taarifa.

Mtu akisoma bila kutafakari andiko lako atagonga thenkis kama mimi, mwendo kasi ni kawaida ya gari,gari haliruki kama chura,si kweli kwamba kugonga magari saba ndiyo maana ya kuwa kwenye mwendo kasi lah,yaweza kuwa kughafirika kwa dereva kukamfanya ashindwe kuweka mguu kati,kwa vile ni lori kubwa 'Kumbuka MOMEMTUM' hata kwa kasi ya kawaida kama dereva amesahau pedali ya break ilipo inaweza gonga hata magari 10.Naamini kama hilo benzi lingekuwa kwenye overdrive maafa yangekuwa ni makubwa mno,kitendo cha kuchomekewa kwenye udereva mara nyingi hakina ushujaa,kichwa kinakuwa kwenye mfadhaiko na mahangaiko ya jambo gani lifanyike kwanza kati ya break,kukwepa au kusonga mbele na kugonga,mara nyingi uamuzi wa haraka kichwani hua ni kukwepa au break,hivi vyote vinamadhara makubwa kwa malori makubwa hasa yanapokuwa kwenye spidi ya kawaida sana ya 60kms/hrs.Hamna kitu kibaya kwa dereva barabarani kama kuchomekewa wakati unaendesha comfortably ukiamini kila gari unaloliona kuwa linaendeshwa na binadam na ni dereva,dereva kwa maana ya kwamba kila tendo hulifanya baada ya kuyatafakari mazingira ya gari yake,barabara na watumiaji wengine.
Nakataa na nitazidi kupinga haya mambo ya kukimbilia spidi eti ndiyo imesababisha ajali,kwa hitimisho la namna hiyo kamwe hatuwezi kutengeneza mazingira ya udereva salama, swala ni MATUMIZI SAHIHI YA BARABARA NA UDEREVA KWA TAFAKARI.

KUHUSU LESENI SIJUI KAMA KUNA LESENI ZA KULETEWA NYUMBANI. Ukweli utatuweka HURU
 
Acha unazi mkuu, kwa lori lililokuwa kwenye mwendo mdogo lisingeweza panda tuta halafu kwenda huo umbali na kusababisha madhara kama aliyoyaelezea shuhuda. Ni wazi hilo lori lilikuwa mwendo kasi usio wa kawaida na pia hiyo daladala nayo inaweza ikawa ilifanya kosa vilevile

kama ni unazi wewe nakutunuku nishani,lori lenye gear zaid ya sita high na low liwe kwenye overdrive(speed kubwa) ndani ya mita 500 tufanye,ajabu.tofautisha lori na saloon car mkuu, 50 km/hrs ya lori ni tofauti sana na 50km/hrs kwa impact kama ni ajali...
chanzo si mwendo kasi,bali ni matumizi mabaya ya barabara yafanywayo na madereva wa daladala...

KAMA WEWE NI DEREVA FANYA EXPERIMENT YA NAMNA UTAVYOAMUA UKICHOMEKEWA GHAFLA HATA UKIWA SPIDI YA 50/HRS
 
Mwendo kasi unaweza kuonekana kwa macho pia. Siyo lazima uwe na kifaa cha kupimia mwendo kasi kujua huu ni mwendo kasi. Unaweza kutumia common sense kujua huu ni mwendo hatarishi au siyo. Na kwa taarifa yako kuna jiwe lilofanyika kama kigingi baada ilo jiwe kugongwa kasi ya hilo gari ilipungua na laiti mwendo usingepunguzwa na hicho kigingi bila shaka madhara yangekuwa makubwa kuliko yalivyokuwa. Lori limeharibu magari saba wewe unasema lilikuwa linatembea mwendo wa pole mwendo wa arusi! Ungekuwepo katika tukio ungeandika kitu tofauti. Kuhusu polisi kufanya vibaya kwa sababu wanaoajiliwa wamefeli fomu 4 hoja hiyo naye ni nyeupe. Angalia safu ya uongozi wa nchi hii jinsi iloivyosheheni wasomi wa vyuo vikuu, madaktari, maprofesa n.pamoja na kusheheni wasomi katika safu ya uongozi hali halisi ya uchumi na huduma za jamii zipo taabani, kuanzia afya, elimu.makaazi,kilimo na ufugaji, rushwa, ufisadi,madini na nishati,nguvu kazi ya taifa vijana ipo under-utilized, sheria na katiba,ni dhahili kabisa hiyo elimu waliyoipata haisadii kupambana na mazingira maana kwangu mimi maana ya elimu ni UWEZO WA KUPAMBANA NA MAZINGIRA au capacity to meet life situations. Kwani kwako nene elimu lina maana gani?

Anyway kuna mambo mengi ya kuangalia kabla ya mtu kufikia hitimisho la kuwa lori lilikuwa mwendo usio wa kawaida au lah,aina ya barabara ni jambo la msingi sana,Je ? ni barabara ya mtaani au ni highway,je kama ni highway minimum na maximum speed ya gari ni ngapi,na je wakati gari ilipokuwa inapata ajali kadilio la spidi ni ngapi mara nyingi kuangaliwa alama za mserereko wa break kama dereva alikumbuka kuweka mguu kati. Kwa vile wewe ulishuhudia ajali na macho yako yanajua kukadilia spidi japo hata katika andiko lako umeshindwa kusema hisia zako kwenye kile unachosema overspid ni kiasi gani,nasisitiza kama daladala asingefanya fujo barabarani ajali hiyo isingekuwapo.
swala la Elimu (Tofautisha Elimu na Uwezo mzuri wa Kutafakari) Mtu anaye fail naamini kuna tatizo katika mchakato uliomfikisha kufail, usichanganye Elimu na Failure,fail haimaanishi kuwa hana elimu,lah,amekwenda shule,kapewa mtihani kashindwa,japokuwa wapo walioshindwa si kwa kuwa upstairs ni kubovu bali ni mazingira,lakini wengi wa wanaoshindwa upstairs ni kubovu.uchumi na Huduma za jamii unamaanisha nini,kinachoitwa uchumi ni mapato ya wananchi katika ubinafsi wao ndiyo mjumuisho wake hupima uchumi wa nchi,Kwa uvivu wetu watz unategemea maprof.walete uchumi mzuri,Uvivu umetulemea japo wanasiasa kwa kukosa uzalendo hawalisemi hili wamebaki kuhubiri umasikini kwa kuwa umasikini wenu unawanufaisha.
Kama Ekufaulu si kigezo kwanini kuna mitihani,anafeli mtuhani anapelekwa trafic unataka afanye maajabu,bado naamini uwezo mzuri wa kufikiri ni kichocheo cha utendaji uliotukuka,failure wanaenda polisi then tunatarajia maajabu yatendwe ,mfumo mbovu maisha mabovu,matukio mabovu.
 
Back
Top Bottom