GM7
JF-Expert Member
- Jun 26, 2009
- 492
- 24
Kwa mujibu wa TBC taifa treni ya abiria iliyokuwa ikisafiri kutoka Dar es Salaam kwenda Kigoma imeanguka usiku wa kuamkia leo nje kidogo ya mji wa Morogoro ambapo imejeruhi watu kadhaa. Mmoja wa wafanyakazi wa TRL amesema treni hiyo ilipita Morogoro saa 6:15 usiku. Imeelezwa kuwa takribani mabehewa 6 yameanguka na chanzo cha ajali hiyo bado hakijafahamika.
Taarifa kamili ya ajali hiyo itaendelea kutolewa ktk taarifa za habari zijazo.
Taarifa kamili ya ajali hiyo itaendelea kutolewa ktk taarifa za habari zijazo.