Ajali ya School Bus

Domo Kaya

JF-Expert Member
May 29, 2007
531
59
Nimepokea habari ya kusikitisha sasa hivi, kuna ajali imetokea pugu road School bus na roli yamegongana, dereva na baadhi ya wanafunzi wamekata roho hapo hapo.

Mwenye habari zaidi, au yupo maeneo hayo atupe habari zaidi.

Kila mtu anatembea na kifo chake. M/mungu awalaze marehemu wote mahala pema peponi, AMEN.

Kwa wale wenye watoto wanaosoma shule ya msingi Olympio jamani wajaribu kufuatilia, maana inanisumbua kichwa kujiuliza kule walikuwa wanatoka wapi na wanaenda wapi.
 
OMG jamani pole kwa wazazi wa watoto hao na familia ya dereva pia, jamani inauma kupoteza watoto. Mungu tusaidie na majanga ya ajali
 
Habari ambayo nimeipata mpk sasa ndio hiyo, mimi mwenyewe najiuliza wanatoka wapi na wanaenda wapi, au ndio wapo katika kupelekwa makwao sielewi, ila bado naendelea kufuatilia nijue zaidi, kwa wale wenye watoto shule hiyo jamani hebu jaribuni kuulizia ili tupate habari za uhakika zaidi.
 
Habari nilizozipata sasa hivi ni kwamba ni kweli ajali imetokea. Ni njia ya kuelekea Gongo la Mboto wanafunzi walikuwa wanarudishwa nyumbani toka shule. Maiti ziko Temeke Hospital. Nimeongea na mmliki wa mabasi ya King Trans anaitwa Mr Chande namba yake ni 0784490291. Yeye pia hana details za idadi ya waliokufa na kwakuwa anaelekea Temeke Hospital atatu-update tuzidi kuwasiliana naye kwa simu hiyo hapo juu
 
Back
Top Bottom