Ajali ya MV Skagit: Waziri Zanzibar ajiuzulu

Kertel

JF-Expert Member
May 11, 2012
5,268
4,973
Waziri wa miunombinu wa serikali ya mapinduzi ya zanzibar awasilisha barua ya kujiuzulu kwa rais wa zanzibar kufuatia ajali ya meli ya skargit na rais amekubali na kumteua waziri mwingine bwana rashid seif kutoka cuf
 
Waziri wa miunombinu wa serikali ya mapinduzi ya zanzibar awasilisha barua ya kujiuzulu kwa rais wa zanzibar kufuatia ajali ya meli ya skargit na rais amekubali na kumteua waziri mwingine bwana rashid seif kutoka cuf

Huyo mpya anauwezo wa kupambana na hizo ajali? au kwa maana nyingine alishiriki vipi kuzamisha meli hiyo? na ni kwa kiwango gani tunaamini huyu ajaye ni suluhisho? au ni maigizo / zingaombwe la mwaka?
 
Huyo mpya anauwezo wa kupambana na hizo ajali? au kwa maana nyingine alishiriki vipi kuzamisha meli hiyo? na ni kwa kiwango gani tunaamini huyu ajaye ni suluhisho? au ni maigizo / zingaombwe la mwaka?

anajua shein
 
Angeachia ngazi wakati ule wa ajali ya Spice Islander pengine (pengine) hii ajali ya pili isingetokea.
 
Wenzetu wako 'smart'. Sijaelewa hawa magamba wa uku ni magamba ya kobe au?
 
Waziri wa miunombinu wa serikali ya mapinduzi ya zanzibar awasilisha barua ya kujiuzulu kwa rais wa zanzibar kufuatia ajali ya meli ya skargit na rais amekubali na kumteua waziri mwingine bwana rashid seif kutoka cuf
Ndio maana hawa jamaa wanataka nchi yao.
 
00000000001ajiuzuluzenji.jpg
Waziri wa Mawasiliano na Miundombinu mjini Zanzibar, Hamad Masoud amejiuzulu wadhifa wake baada ya kuwepo kwa shinikizo la kuachia ngazi lilitoka kwa wananchi.

Hatua hii imekuja kufuatia madai ya wananchi kuwa ajali za meli zimekuwa zikiongezeka mjini Zanzibar bila yeye kuchukua hatua.

Kwa habari zaidi ungana nasi baadaye. http://www.mwananchi.co.tz/componen...li-ya-mv-skagit-waziri-zanzibar-ajiuzulu.html
 
hamad-masoudzenji.jpg
Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Hamad Masoud Hamad​

Salma Said na Talib Ussi, Zanzibar
Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Hamad Masoud Hamad amejiuzulu wadhifa wake jana kufutia ajali ya kuzama kwa meli ya Skagit.Taarifa ya Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Dk Abdulhamid Yahya Mzee ilisema tayari Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein amekubali ombi la kujiuzulu kwa Waziri Hamad.

“Tarehe 20 Julai, 2012 Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Mheshimiwa Hamad Masoud Hamad alimuandikia barua Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimia Dk Ali Mohammed Shein kumuomba ajiuzulu kufuatia ajali ya kuzama kwa meli ya Mv Skagit iliyotokea Julai 18,2012,” Ilisema taarifa ya Dk Mzee.

“Kufuatia kujiuzulu kwa aliyekuwa Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano, Rais amemteua Rashid Seif Suleiman kuwa Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano,” Taarifa ya Ikulu ilisema na kwamba Uteuzi wa Waziri mpya huyo umeanza Julai 23 mwaka huu.

Wakati huo huo, Dk. Ali Mohammed Shein ameunda Tume ya kuchunguza ajali ya kuzama kwa meli ya Mv Skagit ambayo itaongozwa na Mwenyekiti wake, Jaji Abdulhakim Ameir Iss.

Wajumbe wa tume hiyo ni Meja Jenerali S.S. Omar, Hassan Mussa Mzee, Kapteni Abdulla Yussuf Jumbe, Kaptein Abdulla Juma Abdulla, Salum Taoufiq, Kaptein Hatibu Katandula, Mkali Fauster Ngowo, Ali Omar Chengo na Shaaban Ramadhan Abdalla ambaye ni Katibu wa Tume.

Mapema akizungumza na waandishi wa habari mjini Unguja jana, Makamu wa Pili wa Rais wa SMZ, Balozi Seif Ali Iddi alisema lengo la kuundwa kwa tume hiyo ni kupata ushauri wa nini cha kufanya katika kuhakikisha vyombo vya abiria vinakuwa salama.

Balozi Iddi alisema kutokana na hali ya ajali zinazotokea na mbali na Tume hiyo, Serikali imeona kuwa ipo haja pia ya kupitia upya Sheria zinazohusu usafiri wa baharini na kuweka aina ya viwango vya meli zitakazoruhusiwa kuingizwa nchini na kuchukua abiria.

Alisema pia Serikali unakusudia kununua meli kwa ajili ya usafiri ipo palepale na kwamba, juhudi zinaendelea katika kufanikisha suala hilo.

"Katika hatua ya kudhibiti majanga ya aina hii, Serikali inakusudia kuzifanyia mapitio sheria zinazohusu usafiri wa bahari na kuweka viwango vya aina ya meli zitakazoruhusiwa kuingizwa nchini na kuchukua abiria,” alisema.

Kauli ya CUF
Mapema jana Mwenyekiti wa CUF, Profea Ibrahim Lipumba alisema alitumaini kuwa Hamad angechukuwa hatua kwa kuzingatia mfululizo wa ajali hizo.

Profesa Lipumba alisema waziri huyo anayetokana na Chama cha CUF, anapaswa kuwajibika ili kumsaiddia Rais na Serikali kutekeleza majukumu yake ipasavyo.

“Chama kina imani kuwa atawajibika kwa kilichotokea,” alisema Lipumba.

Alisema kimsingi waziri huyo hana kosa la kiutendaji, lakini hali halisi ya kisiasa, inamtaka kuchukua hatua za kujiuzulu au hatua nyingine kwa namna anavyoamini kuwa inafaa.

Msimamo wa CUF ulikuwa ni tofauti na ule wa Hamad ambaye mara kadhaa alishanukuliwa akisema kwamba hawezi kujiuzulu na kwamba, waliokuwa wakishinikiza suala hilo ni wasiopenda Serikali ya Umoja wa Kitaifa.

"Siwezi kujiuzulu kwa sababu kilichotokea ni mipango ya Mungu, hivi ningezuiaje upepo usitokee, ajai hii ni mipango ya Mungu, haiwezi kuzuiliwa na binadamu,” alisema waziri huyo.

Maiti tano zaopolewa
Wakati huohuo, Balozi Seif aliwaambia waandishi wa habari kwamba, maiti zaidi zimeopolewa na kufanya marehemu waliotokana na ajali hiyo kufikia 78.

Alisema miili iliyopatikana ilikimbizwa kuzikwa eneo la Kama nje kidogo ya Mji wa Zanzibar ambako kumetengwa kwa kuzikiwa maiti hizo.

Balozi Idd alisema kwamba, mpaka sasa jumla ya watu 146 wameokolewa wakiwa hai huku maiti zikifikia 78 ambazo ni pamoja na wanaume, wanawake na watoto.

Kuhusu juhudi za uokoaji, alisema meli hiyo ilikuwa na raia wa kigeni 17 na waliookolewa wakiwa hai ni 15 na mmoja ambaye ni raia wa Uholanzi alipatikana akiwa amefariki na mwingine mmoja hakupatikana hadi jana.

Wageni walinusurika kufa katika ajali hiyo wanatoka Ubelgiji, Marekani, Ujerumani, Uholanzi na Israel kwamba, Serikali iliwahudumia na tayari wameondoka kurudi kwao.

Balozi Idd aliongeza kuwa, hadi jana, kati ya majeruhi 138 waliopelekwa katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja iliyopo mjini Zanzibar kwa uchunguzi walikwisharuhusiwa kwenda kwao baada ya kupata matibabu.

Aliwataka wananchi popote watakapoona maiti wapeleke taarifa Jeshi la Polisi, wakuu wa wilaya, mikoa na masheha ili taratibu za kuichukua na kuihifadhi miili hiyo ziweze kuchukuliwa.

Kamishna wa Polisi Zanzibar, Mussa Ali Mussa alisema miongoni mwa maiti hao mmoja imetambuliwa kuwa ni Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ, Kikosi cha Bendi Zanzibar aliyetambuliwa kwa jina la Suleiman Pandu Jape.

Meneja wa MV Skagit

Makachero wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, wamemsafirisha kwenda Zanzibar
Meneja wa Meli ya Skagit, Omari Hassan Mnkonje (50) ili kuunganishwa na watuhumiwa wengine wanaohojiwa na Polisi visiwani humo kuhusiana na meli hiyo.

Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi Zanzibar ACP, Yusuf Ilembo, alisema meneja huyo wa ambaye ofisi zake zipo Jijini Dar es Salaam ameunganishwa na watuhumiwa wengine katika kesi hiyo.

Katika hatua nyingine, Kamanda Ilembo amesema kuwa watuhumiwa watatu kati ya sita waliokuwa wakihojiwa kuhusiana na tukio hili wameachiwa baada ya kuonekana kuwa hawahusiki katika tukio hilo.

Taarifa za nyongeza na Mohammed Mhina, Polisi Zanzibar na Joseph Zablon, Dar es Salaam Ajali MV Skagit yamg
 
Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano wa Zanzibar, Hamad Masoud Hamad amejiuzulu wadhifa wake leo jioni imeelezwa. Kwa mujibu wa taarifa ya Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Dk. Abdulhamid Yahya Mzee ilisema tayari Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk. Ali Mohammed Shein amekubali ombi la Waziri Hamad Masoud kujiuzulu.

Zaidi hapa ZanziNews Blog

 
Kwenye ZanziNews Blog, Mheshimiwa huyu Mkubwa sana alinukuliwa akisema haya:
[h=2]Saturday, July 21, 2012[/h][h=3]Waziri Masoud: Sioni sababu ya kujiuzulu[/h]


Asema Dhoruba Ilizamidha Mv Skagit


Na Waandishi wetu
WAZIRI wa Miundombinu na Mawasiliano, Hamad Masoud Hamad, amesema haoni sababu ya kujiuzulu nafasi yake, kufuatia janga la kuzama kwa meli ya MV.Skagit iliyopoteza maisha ya zaidi ya watu 60.
Waziri Masoud alisema meli hiyo ilizama kutokana na janga la kimaumbile, kufuatia upepo mkali uliosababisha mawimbi na hatimaye kuzama kwa boti hiyo.


Alisema haoni sababu ya msingi ya kujiuzulu kufuatia ajali ya kuzama kwa meli hiyo licha ya kutokea ndani ya kipindi cha mwaka mmoja tangu kuzama kwa meli ya MV. Spice Islander.


Alikiri kuwepo kwa maoni ya watu kumtaka ajiuzulu na kuwaeleza watu wa aina hiyo kuwa hakuna mtu anayeweza kuzuia majanga ya kimaumbile kama upepo yasitokezee.
"Kumekuwa na watu wanaotoa maoni juu ya suala la kujiuzulu, lakini bado hakuna mtu anayeweza kuzuiya upepo usitokee kwani hauko katika mamlaka yake",alisema waziri huyo.


"Kuna wengine wanasema tumemkosa kule sasa watanipatia kwa hili, nimeshapata taarifa kuwa kuna ‘private member' watapeleka hoja katika Baraza la Wawakilishi ya kujiuzulu, nimeshasikia na wimbo huu unaimbwa tena na natumiwa meseji kuulizwa nitajiuzulu wakifa wangapi kwani mimi napenda kuua", alisema..






Lakini ukiangalia hapa:
"Tarehe 20 Julai, 2012 Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Mheshimiwa Hamad Masoud Hamad alimuandikia barua Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimia Dk Ali Mohammed Shein kumuomba ajiuzulu kufuatia ajali ya kuzama kwa meli ya Mv Skagit iliyotokea Julai 18,2012," Ilisema taarifa ya Dk Mzee.
, utaona kuwa wakati anasema kuwa hatajiuzulu NG'O tarehe 21 Julai, kumbe tarehe 20 Julai alikwisha muandikia Raisi barua ya kujiuzulu. Ukweli uko wapi?
 
kwanza alitamka, "sijiuzulu ng'o! kwani mimi ndio nilivumisha upepo baharini? haya ni mapenzi ya Mungu." huo ushujaa nimpe wa kazi gani sasa

ningempongeza kama angejiuzulu pale bandarini alipokwenda kusaidia uokoaji.
 
Back
Top Bottom