Ajali ya MV Bukoba: Makosa yamerekebishwa?


Hizi ni baadhi ya picha za ajari ya MV Bukoba,
No 1 Meri ikiwa kichwa chini miguu juu, ndani kuna abiria wako hai
,, 2 Mnara wa kumbukumbu ya ajari kwa mbari[/SIZE]
,, 3 Mnara wa kumbukumbu kwa karibu
,, 4 Meri ya mv Bukoba kabla ya kuzama (enzi za uhai wake)

mkuu reekebisha kwanza humo kisha tuje kuisoma maana.
 
Watanzania wezangu,

Kama mnavyokumbuka, miaka kumi na nne iliyopita usiku wa leo kuamkia tarehe 21 May, 1996, Tanzania ilipatwa na janga la pekee kwa kupoteza uhai wa zaidi ya watu 1500 wasio na hatia katika ajali ya MV Bukoba ambayo ilisababishwa na uzembe wa watu wachache. Idadi kamili ya waliokufa haijawahi kutolewa na badala yake kulikuwa na jitihada za makusudi za kutaka kuficha idadi hiyo mara tu baada ya ajali; inawezekana kabisa kuwa watu waliokufa katika ajali ile ni wengi kuliko wale waliokufa kwenye ajali ya TITANIC iliyotokea April 15, 1912 na kuua watu 1516 kamili.


  1. Ninafahamu kuwa serikali imewajengea wahenga wetu wale mnara wa kumbukumbu. Jambo ambalo sijaelewa ni namna gani ndugu na jamaa wa marehemu wale walivyofidiwa. Kwa vile ajali ile ilitokana na uzembe wa shirika la reli, ninategema kuwa shirika lilichukua jukumu la kutoa fidia kwa walioathirka na ajali ile. Je ni kweli hilo lilitokea?
  2. Baada ya kuwa na ajali mbaya namna ile nadhani serikali iliahidi kusimamia na kuboresha usalama katika njia zetu za usafari. Je ahadi ile ilifika wapi? Imekuwa jambo la kawaida kusikia ajari za ajabu sana siku hizi hasa zile za barabarani zikihusisha watu wengi wasio na hatia ambao huwa ni abiria tu. Je serikali bado inakumbukua wale ndugu zetu wa MV. Bukoba kweli?
  3. Katika kukumbuka ndugu zetu wa walioangamia na MV Bukoba, ninaomba wana JF tusimame kimya kwa dakika mbili popote pale tulipo.
 
Hiyo ajali ilikuwa kuboko,niliwapoteza ndugu zangu sita hapo na siyo siri sina hakika kama serikali imefanya jambo lolote kubwa walizoahidi. May The Souls of the departed brothers and sisters be granted eternal peaceful rest. Amen!
 
Hiyo ajali ilikuwa kuboko,niliwapoteza ndugu zangu sita hapo na siyo siri sina hakika kama serikali imefanya jambo lolote kubwa walizoahidi. May The Souls of the departed brothers and sisters be granted eternal peaceful rest. Amen!
pole sana mkuu,ndugu sita kwa mpigo si mchezo.lakini ndio ilivyo serikali yetu ndio kwanza itakuletea ripoti ya uchunguzi kurasa kibao ili uone uvivu kusoma kisha imekula kwako,wakati wewe umepoteza ndugu zako.:angry:
 
Nakumbuka maskini ndugu na jamaa zangu watu karibia 25 nimewapoteza na kibaya zaidi tulipata mwili mmoja tu RIP
 
Nilikuwa Tanzania kwa likizo fupi ya summer lakini nadhani likizo yangu yote iliharibiwa kabisa na ajali ile hasa pale zilipoanza kutolewa taarifa kuwa miili ya victims imeharibika kiasi kuwa haitaweza kuopolewa tena, itabidi ibakie huko huko majini na mabaki ya meli ile ndiyo itakayokuwa kaburi lao!!
 

It has been 14 years now since I last saw my mother's smile. Every 21st of May is a difficult day for me. Even though time does heal the soul and the pain dulls, the sense of loss is ever present. The day my mother died, 3 days of national mourning was declared, not because she was so singularly important but because her death was one of the nearly one thousand (1,000) deaths that occurred that day on Lake Victoria.
Next to my mother, was my beloved cousin who also perished with my mother. For Tanzanians, the name MV Bukoba says it all, but for non Tanzanians it says nothing. May 21st 1996 MV Bukoba – a steamboat that carried hundreds of passengers across Lake Victoria from Bukoba to Mwanza sank and nearly one thousand people died.
Why and how it sank and who is to blame, is something that the media has chewed over again and again every year but not as much attention has been given lately to the loss that ordinary Tanzanians have suffered.
My family was not special that day because we mourned with thousands of Tanzanians who lost their loved ones.
This is the first time that I have publicly opened up about my loss and it has not been easy. But I feel that sharing this loss with people especially with Tanzanians might help those ones who suffered similar losses on that day, to re-live it in a more public manner and to know that we are not alone. Since I received the news and followed the tragedy unfold on radio on that fateful day, I know I changed. I came to realize how fragile we all are and how important it is to use every minute and hour in the present, because time fleets by. And I try to live every minute and second of my life to the fullest.We all changed that day and the one who came out the strongest was my father. He had to overcome his grief of losing his wife, and he raised us as a single parent. He is our father and our mother rolled in one, he is our anchor, our support, our hope.
My Dad means the world to me and to my siblings. Looking back I know that I can never truly know how difficult it was for him, yet he remained patient, gentle and loving with us, he was never bitter or desperate but held us all together and gave us strength to move on. His love for us is exemplary and his courage is heroic.They say that with time our memories of past loved ones fade and their faces blur, but my mother's smile and face is seared in my mind.
To me, she is still with me even if not in body. I know that every step I make she watches over me, and she lifts me up when I stumble and fall in my life. Her love nourishes me to date and has propelled me to where I am today. Even if for a brief while, I had you, Mama, and I am thankful to God that you were in my life and you continue to be with me.
- Flaviana
http://globalgrind.com/channel/news/content/1590359/exclusive-blog-by-flaviana-matata-gone-too-soon/
http://twitter.com/FlavianaMatata/status/14399174600
 
Kaitaba please usinitoneshe kidonda ambacho kilishaanza kukauka.
Nilipoteza watu wangu wa karibu sana katika ajali hiyo.
Ni vizuri tukawa tunaadhimisha kila inapofikia tarehe hiyo kwa kuwaombea waliotutoka.
Ni vizuri tukaadhimisha.

Tarehe uliyoitaja inawezekana ndiyo tarehe aliyofika Ben Mkapa pale uwanja wa Nyamagana kusitisha zoezi la kuwatafuta ndugu zetu baada hata ya wataalamu kutoka South kuchemsha na kuondoka na siri moyoni kwa kile walichokishuhudia chini ya maji.

Umenikumbusha mbali,,,,,kwani ile ripoti ya uchunguzi wa ajali ilisha toka?
KUMBUKUMBU ZINANIONYESHA Mv BUKOBA ILIZAMA USIKU WA KUAMKIA TAREHE 21/MAY/199,kuna lipi jipya la kutufanya tuadhimishe tarehe 25?hata hayo maadhimisho yenu sipendi kuyasikia.





K

Ni tarehe 21 sio 25, samahani kwa hilo, ila hizi hoja mbili tuchague moja na tuielekeze serikali cha kufanya
 
MV Bukoba ilizama 21/05/1995 maadhimisho 25/05/2010?

The best thing tungefanya kama kumbukumbu ni kuimarisha usafiri wa majini nchi nzima... haya mengine ni ubatili mtupu na kujilisha upepo

BTW: Kwa waliokuwa UDSM (Hill) hiyo tarehe kulikuwa na MGOMO wa wanafunzi ambao nadhani haujawahi kutokea tena! Maeneo ya Wizara ya Sayansi (enzi hizo). Kitu ambacho nakikumbuka sana ni nguvu ya askari wa FFU iliyotumika!
 
mkuu reekebisha kwanza humo kisha tuje kuisoma maana.

Nashukuru, bahati mbaya sikusomea arts, nimesomea sayansi, unisamehe bure, sijui nirekebishe nini, pamoja na hayo kuna wengine wanajaribu kuchangia,hivyo hivyo na wewe jaribu mimi nitakuelewa tu ndugu yangu uwe na amani ya BWANA.
 
Nashukuru, bahati mbaya sikusomea arts, nimesomea sayansi, unisamehe bure, sijui nirekebishe nini, pamoja na hayo kuna wengine wanajaribu kuchangia,hivyo hivyo na wewe jaribu mimi nitakuelewa tu ndugu yangu uwe na amani ya BWANA.

sio suala la arts wala sayansi shemeji yangu ni zaidi ya hilo.....nakumbuka kwa wakwe zangu kashozi kashekulo
 
sio suala la arts wala sayansi shemeji yangu ni zaidi ya hilo.....nakumbuka kwa wakwe zangu kashozi kashekulo


Wanaojua maana ya hapo pekundu watusaidie, pamoja na hayo mada bado haijapata jibu bado.
 
Hiyo picha ya mwisho sio ya MV Bukoba ni MV Victoria ambayo ipo mpaka keo!

Maadhimisho ni muhimu, ila yanatakiwa yawe kwa namna tofauti! Inatakiwa siku ya maadhimisho kila mwaka, serikali iseme imechukua hatua gani kuhakikisha ajali kama hii haitokei tena na hatua itazochukua incase ajali kama hii imetokea.
Hii inatakiwa kila mwaka waseme wamefikia wapi kiutelezaji na sio kutuonesha yaliyotokea MV MV Bukoba. Hayo wanaweza kutuonesha kila baada ya miaka mi5 au kumi!
 
Naikumbuka sana siku hii,kipindi hicho ni mwanafunzi pale Pamba sekondari,nakumbuka kukatishwa kwa masomo na vingora vya magari ya wagonjwa yaliyokuwa yakipeleka wale waliokuwa wamebahatika kuokolewa wakingali hai katika hospitali ya bugando.Mpaka leo hii sijajua ni kwa nini sikuweza kwenda katika uwanja wa NYamagana kuangalia maiti za watanzania wenzetu,LAKINI PIA HILI NI MOJA YA MATUKIO YALIYOSABABISHA NIAMINI KWELI KUSAHAU NI MOJA YA NEEMA TULIZOPEWA NA MUUMBA KWANI LAITI TUNGEKUWA HATUSAHAU SIJUI TUNGEWEZA VIPI KUISHI HUKU TUKIO HILI LIKIJIRUDIA KILA MARA KATIKA AKILI ZETU.kWA WALIENDA NYAMAGANA NA WALIOPOTEZA NDUGU NA MARAFIKI WATAKUWA WANAJUA NAMAANISHA NINI.
 
Kuna tulilojifunza kutokana na ajali ile kweli?................au ndio business as usual..............sio ziwani tu hata barabarani.............
 
Kuna tulilojifunza kutokana na ajali ile kweli?................au ndio business as usual..............sio ziwani tu hata barabarani.............

Mafunzo makubwa ni kuwa hatuna kitengo cha dharura chenye uwezo wa kukabiliana na majanga. Na kudharau sheria na taratibu za uendeshaji wa vyombo vya usafiri kwa ku-overload

Nilipoteza watu watano niliokuwa nawafahamu fika kwa takriban miaka sita ya kuwa pamoja nao katika pilikapilika za maisha.

Kama tungekuwa na kitengo imara na chenye watu wanaofikiria kisayansi basi tungepoteza watu wachache sana. Kitendo cha kila mtu Polisi, wanasiasa kujifanya wahandisi na kufikia maamuzi ya kutoboa tundu na ku-release hewa iliyokuwa imehifadhiwa ndani na kuifanya meli izame, wakati tungeweza kuivuta kwanza kwa kutumia panton mpaka maji mafupi na kuanza uokoaji.

mv+mnara
 
Tulipoteza nguvu kazi kubwa kutokana na hii ajali..Tujifunze kutokana na hii ajali.
 
Back
Top Bottom