Ajali ya Meli Zanzibar; Sumatra yabebeshwa lawama

Gumzo

JF-Expert Member
Jan 2, 2012
211
7
SIKU chache baada ya serikali kutangaza kusitishwa kwa zoezi la uopoaji wa miili katika meli ya Skagit iliyozama karibu na Kisiwa cha Chumbe, baadhi ya wananchi wamerusha lawama kwa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) kwamba ina upungufu katika utendaji wao wa kazi.
Wakizungumza na gazeti hili mwishoni mwa wiki iliyopita baadhi ya wananchi walisema kumekuwa na mchanganyiko wa idadi ya abiria kila meli inapopata ajali, hali inayoonesha kwamba Sumatra hawana utaratibu mzuri wa kuelekeza wamiliki wa vyombo vya majini jinsi ya kutunza kumbukumbu za abiria wanaopanda melini.
“Hakuna utaratibu mzuri wa kutunza kumbukumbu wanaoingia katika meli na hii inachangia watu wengi kuingia katika chombo bila shaka kupita uwezo wake.” Alisema Saidi Kilopwa Saidi aliyekuwa akisafiri kwenda Zanzibar aliyekuwa bandarini Dar es Salaam.

KWA HABARI KAMILI BOFYA HAPA
GUMZO LA JIJI
 
Mwandishi aliyeandika habari hii na wananchi waliotoa maoni yao hawajui kuwa mafisadi wa zanzibar waliipiga stop SUMATRA kufanya chochote kqwenye meli za zanzzibar?!, well; nashangaa jeshi la polisi wamejaza polisi barabarani kusumbua magari ya mizigo na abiria lakini sijawahi kuwaona wakiangalia usalama wa vyombo vya majini, sijaona wakikagua kama chombo kina maboya ama life jackets za kutosha na tahadhari nyingine. Tikiti za kusafiri kwenda zanzibar zinauzwa kama njugu ama sigara mitaani no body cares. Mi naona IGP pia angejipima na kuchukua uamuzi sahihi maana geshi lake limelala.
 
Back
Top Bottom