Ajali ya Meli: Waokoaji toka SA washindwa kuifikia, wasitisha rasmi zoezi

Dah! Inauma sanawatanzania hatuna wa kutusaidia, tunakufa na maiti zinaliwa na samaki, haya bana!

Inauma sana ,samaki watakula miili ya binadamu wenzetu na baadae tutawavua na kuwala; hivyo ndivyo dunia inavyozunguka!!

Sasa tufanyeje. Wataalam wameshindwa kuifikia... Ndio kaburi lao.
Ukifikiria kwa undani inauma sana.
ITV NEWS

Yale yale ya Mwanza,uzuri huwa sili samaki wa baharini.Kipindi kile 1996 watu tulikula kamongo,sangala,sato,gogogo kwa kwenda mbele

Hapo kwa maoni yangu mh.seif idd amekosea,angejaribu kutumia kauli ingine ya kistaarabu kidogo,watu bado tuna machungu ya msiba.

Mheshimiwa Seif Iddi amelewa madaraka na fedha za misaada yaani kitendo cha kusema meli itakuwa kaburi lao huku akiwa anachekelea ni kibaya na lugha yake haijavaa Condomu kabisa. wafanye sensa ya maiti zilizopotea.

Mheshimiwa Seif Iddi amelewa madaraka na fedha za misaada yaani kitendo cha kusema meli itakuwa kaburi lao huku akiwa anachekelea ni kibaya na lugha yake haijavaa Condomu kabisa. wafanye sensa ya maiti zilizopotea.

kaburi lao, kina nani, na ni wangapi? Ajaribu kuwa mstaarabu basi

Serikali yakiri kuwa wazamiaji kutoka S.Afrika hawawezi kufika umbali ilikofika hiyo meli (kina cha maji),imewaomba waliofiwa na ndugu zao na hawajawaona wakubali meli ile iwe kaburi la ndugu zao!(ajari nyingine) AJARI YA BASI YAUA WATU KUMI BAGAMOYO,KIKWETE ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KWA MKUU WA MKOA WA PWANI! Source Radio one,taarifa ya habari.

Kwa hiyo ni wangapi wamepotea na meli huko chini ya bahari kwenye huo mkondo wa nungwi! Mungu tujaze hekima.

mita 340 ni ishu? Watu/maiti zaidi ya 500 hawajulikani walipo. Ni wazi kuwa wapo huko majini na serikali (ya zanzibar) inaona aibu kuzamia. Ishu si kuitoa meli bali miili. Funika kombe na chozi la mamba. Hofu yangu ni kwa hiyo misaada inayomiminika huko tu

Kuna post moja humu inasema kuwa Serikali imesimamisha makusudi utafutaji wa maiti katika meli iliyozama kwa "sababu ya kuficha aibu, na uzembe wao".

Kwa kiasi kikubwa ninakubaliana na hoja hii kwa sababu, ikiwa S.Afrika haina uwezo, nchi nyengine zenye uwezo zipo na kama wakiomba msaada wanaweza kufanya. Kuna nyamizi nyingi tu ulimwenguni zilizama na maiti au waliokuwemo kuokolewa.

Kwa kusema tu kuwa imeshindikana haitoshi kwani hawajachukua juhudi zote. Maiti zinaweza zisipatikane, lakini kumbukumbu za waliopoteza watu wao zitabaki milele, hasa wakielewa kuwa kuna uzembe umepita.

Ni kweli mkuu ila haya yanayofanywa na serikali hii legelege yanamwisho na kama nijuavyo mwisho wa ubaya aibu

Back
Top Bottom