Ajali ya Meli: "Taifa Msibani, Umoja wetu na Utu wetu shakani!" - Zitto Kabwe

Kila kukicha huku bara ikiwa ni pamoja na Kigoma maelfu ya watanganyika wanakufa kwenye ajali za mabasi lakini sijawahi kusikia mnataka watu waache kufanya matamasha yao!

Nakumbuka Kamadoo na Mkapa wapoliua Wapemba 27(tu?!) mwaka ule matamasha, sherehe, taarabu, mechi za ligi, etc. ziliendelea kama kawa Unguja na Bara.
 
Bosi wangu ni mtu wa nje na ndiye alikuwa wa kwanza kunijulisha juu ya tukio ilo kwani aliona kupitia sky television,basi nikamuomba tuangalie channel za Tanzania ili tulipate vizuri,tukatafuta we kila channel mara vipindi vya watoto wetu,mara Miziki ,mara daladala,mwisho tukachoka tukarudisha sky news,baada ya masaa mawili tukaangalia tena channel za bongo hakuna lolote,bosi akasema 'this country is very funny ,you dont take seriously serious things,instead you take seriously simple things' MWISHO WA KUNUKUU
 
Huu ujinga wa kuwafanya wa TZ kama NDONDOCHA kwa viongozi wanaoongoza Taasisi za Serikali kutokujali kile kinachowatokea Wananchi kwa kuwa tu wanajua hakuna anayeweza kuwawajibisha ndiyo Jadi. Hawa TBC1 si kwamba ni watu wa ajabu bali walichokifanya ni KITUKO CHA MWAKA.
m
Roho za Watanzania wenzetu zidi ya 200 zimetokomea kwa uzembe wa Waapuzi wachache waliopewa Dhamana ya kuangalia hicho kilichostahili kuangaliwa kabla Meli haijang'oa nanga Bandarini Malindi, lakini kwa hali ya kushangaza hadi sasa hujasikia kuna Kiongozi ameachia ngazi, si Mkurugenzi wa Mamlaka ya Bandari au Waziri wa Mawasiliano.

Lakini jambo la pili hawa VODA Ubinadamu ZERO wao wanachoona ni bora kushuhudia walimbwende na mikogo ya kuiga kwenye jukwaa, eti kwa kisingizio cha kupata hasara kuliko kuonyesha utu,heshima na huzuni ya pekee kwa janga hili la Taifa.Ni faida kiasi gani wametengeneza tangu walipotia mguu hapa Bongo, hao waliopoteza maisha yao wamechangia kwa kiasi kikubwa sana (kama wateja wao) hata kufikiria na hatimaye kukubali kudhamini Miss TZ.

Mimi nasema hakika MWENYEZI MUNGU hausiki na ujinga uliotokea na kusababisha balaa kubwa kiasi hiki, kwa kuwa yeye huwapenda waja wake na huwaita kwake kwa staha kubwa na kamwe si kwa njia hii ya mateso kwenye maji hadi Roho inaacha Mwili.

Sasa kwa kuwa MUNGU mwenyewe ana Mbinu zake za kuwaadhibu aliowakabidhi jukumu la kuangalia wenzao kwa kupitia Viongozi (kwa kuwa Mamlaka iliyoko Duniani ni mfano wa Mamlaka iliyoko Mbinguni)sasa nami nasali nikimuomba awapige na adhabu kali hapahapa Duniani hao wote waliojifanya hamnazo, kwa kuwa najua kwa hali ya kawaida hakuna hatua itakayochukuliwa toka kwenye mfumo waliouzoea.

MUNGU AWAPUMZISHE NDUGU ZETU WALIOTUACHA NA AWAPE NAFUU MAPEMA WOTE WALIOPATA BAHATI YA KUNUSURIKA.AMEN

Mkuu naomba kufahamishwa majukumu ya mhandaaji na mdhamini,ukinisaidia hapo nitakuwa ktk nafasi nzuri kuchangia
 
Binafsi nimesononeshwa sana na kitendo hiki cha hawa vodacom na wenzake kwa kutothanini utu wetu. Kwa kitendo hiki nikaamua kuwatosa kama walivyowatosa watanzania wenzangu. Kuanzia jana niliamua kuacha kutumia huduma zao hadi hapo watakapoomba radhi kwa kitendo hiki cha kudhalilisha watanzania.

Kwa sasa situmii tena sim card ya vodacom. Na pia situmii tena huduma yao ya M-Pesa. Ni bora nikose hizo huduma lakini nibaki na utu wangu na heshima ya nchi yangu.Sipo tayari kushirikiana na watu wasiotambua mchango wangu kwao.

Nashauri hata viongozi wa serikali ambao ni wazalendo na wenye kujali utu wakatae kabisa kuendelea kutumia huu mtandao wa vodacom kwa kuwa umetudharau sana.Hapa siongelei watu kama akina makamba kwa sababu wanafaidika na huu mtandao.

Watanzania wenzangu nawaomba tushirikiane kwa pamoja kuwaadhibu hawa vodacom ili washike adabu wasirudie tena utovu huu wa kutokuwa na utu.

Mungu walaani vodacom ili biashara zake ziyumbe hadi wakurudie wewe muumba mbingu na ardhi.

Amina!!!!!!!
 
Acheni siasa uchwara(zitto $ jussa)kuna matukio mengi yameshatokea na hatujaona hata hao wa nchi ya zanzibar(rejea mazungumzo ya maalim seif jana tbc)wakisimamisha shughuli zao zote za uzalishaji eti kwa ajiri ya kuomboleza,namuona jussa kaa mhuni tu na zitto anafuta upepo asiojua.

Jiulize kwanza budget ya TBC ikoje kabla ya lawama kuiwewzesha kufanya coverage ya live ndio uanze kuilinganisha na cnn,bbc,aljazira etc,acheni vodacom wafanye kazi yao ya uwekezaji ili walipe kodi ambayo inafujwa na serilkali, kuna majanga mengi yameshatokea na hatuwaoni kina jussa wakiongea mf.kuna tofauti gani ya vifo hivo na mauaji ya wana cdm arusha?? Gongolamboto????

Mbagalla? MV bkb?? ajali ya tren dom???watoto kwenye idd tabora??? nk TUPAMBANE KUJENGA MFUMO CIO HIZO SIASA UCHWARA ZA KIPEMBA!!!!!!!
 
Mimi nadhani hasira zetu hazijaelekezwa mahali sahihi. Maana walipokufa watu Gongo la Mboto, Mbagala, watoto 21 pale Tabora tena siku ya Idi ni wachache wetu tuliona jambo hili. Miss Tanzania wangeacha kufanya show kungetufanya tujisikie vizuri kidogo lakini kusingeondoa ukweli kuwa tatizo ni serikali na mfumo wake uliopo. Wanaotakiwa kukatyaliwa na kuadhibiwa ni serikali ya CCM na watendaji wake.

Hivi serikali ilitangaza saa ngapi kuwa taifa limeanza maombolezo ya siku tatu maana wengine wamehesabu siku za maombolezo kuanzia leo Jumapili na siyo jana Jumamosi.

Ni kweli kabisa unayosema! wanaotakiwa kuwajibika ni Serikali na CCM a,mbao walizindua kampeni wakati taifa limegubikwa na simanzi. Siungi mkono sana kuwashutumu Vodacom, kwani wao ni sponsor tu na waandaaji ni watu wengine ambao kama si serikali kupitia wizara ya utamaduni na michezo kusitisha mashindano hayo, basi muandaaji alipaswa kufanya hivyo. Mfadhili yeye alishakabidhi fedha/zawadi kwa kamatiya miss TZ. lakini tangu lini tuna utamaduni wa kuwajibishana??? God forbid!
 
Inasikitisha sana kuwasoma watu mnaojiita Watanzania mkitoa mifano kuhalalisha tamasha la Miss Tanzania na maswala mengine yote. Jamani, jamani Miss Tanzania ni sherehe ya Kitaifa ambayo tunatafuta wawakilishi wetu ktk mashindano ya dunia, leo mnakuja hapa kutetea upuuzi ulofanyika kwa kutoa mifano ambayo haihusiani kabisa..

Na hizi chuki zenu za kufikiria Ubara na visiwani, Uislaam na Ukristu ndizo zinawaponza kiasi kwamba mnashindwa kutazama uzito wa maafa haya dhidi ya tamasha la Miss Tanzania ambaye keshoi atabeba bendera yetu ya Taifa kutuwakilisha. Au kwa sababu Miss Tanzania ni Miss Tanganyika?..Zitto asiseme kitu mkakitazama kwa jicho la Utaifa isipokuwa kasema Zitto mziyempenda kwa mapenzi yetu ya kipuuzi mnakuja tetea vitu kisha ati mnafikiria mtaweza kupambana na matatizo ya utawala ktk nchi yetu?.
Napinga zaidi hata wale wanaowapa pole Wazanzibar, kama vile hili janga halituhusu Bara!... mbona maafa ya Mv Bokoba hamkusema poleni Wahaya na Wasukuma?.

Wakuu zangu nawaomba sana vitu kama hivi vinapotokea ni wakati wa kujitazama upya na kuitafuta haki, ni wakati wa kuomba viongozi wote wanaohusika na tukio la maafa haya iwe direct au indirect wajiuzulu haraka, sheria kali iwekwe na kama alivyosema Obama ya kwamba pigo hili (ktk 9/11) litupe nasi ari na nguvu zaidi ya kuweza kukabiliana na UFISADI (uzembe) kama huu. Ni wakati wa kuitaka serikali iwe responsible na accountable kwa sababu imekuwa mazoea na visingizio vya matakwa ya Mungu ktk uzembe mkubwa unaofanyika ktk ngazi zote za kiutawala..

Nilitegemea sana kuwasomeni mkitaka maelezo ya kina kutoka kwa rais, mawaziri na wabunge wetu kuweka sheria kali inayohaklikisha Usalama (safety) ktk sehemu zote za usafiri toka hizo Meli, Ferryboat, treni, mabus na hata ndege haiondoki bila kukaguliwa na hakuna chombo chochote cha usafiri kinapewa kibali cha kupakia abiria pasipo kuwa na safety check inayofanyika kila baada ya miezi sita au mwaka. Pia wananchi wenyewe tuchukue jukumu la kukataa au kuzuia chombo cha usafiri kuondoka ikiwa kuna mashaka ya usalama wa wananchi.

Haya maswala la kutafuta mchawi sijui hulka hii itakwisha lini kwa sababu inatisha sana kuwasoma Watanzania wakiandika kaa wenye imani za kichawi zaidi ya elimu ya sayansi waliyosoma darasani. na pengine ndio maana tunashindwa kukabili matatizo yetu kisayansi badala yake tunakwenda kwa waganga..
 
Zitto ameandika akiwa na uchungu wakati wa tukio kama mtanzania,hata mm ninge react hivyo hivyo.kuna matukio ya kitaifa kipindi cha msibwa mkubwa hivi yanatia aibu.wote aliowataja zitto including waziri Nchimbi wawajibike
 
Mkandara, umesema vyema kweli kweli.

a. Msiba huu kwanza kabisa unagusa watu wa Zanzibar japo ni wa kitaifa. Hili la kuwa msiba ni wamahali kwanza si jambo geni. Yaliyotokea New York marekani Sept 11 ilikuwa ni msiba kwa Wamarekani wote pote duniani lakini kwa namna ya pekee ulikuwa ni msiba wa New Yorkers. Hivyo, watu waliposema wanawapa pole watu wa New York si kwa sababu haukuwa msiba kwa watu wa Michigan au LA. Hili ni kweli hata ilipotokea Mv. Bukoba kwani msiba kwanza kabisa ulikuwa kwa wale watu wa Mwanza. Hivyo, kwa namna ya pekee msiba ni kwa watu wa Nungwi pale na kwa Zanzibar japo ni msiba wetu sote. Wanaoleta hisia ya ukanda na ukabila ni wale walioingiza mambo ya "muungano" kwenye msiba huu. Mmoja anasema "angalieni tv yenu" inaonesha nini na wengine wanasema "upande mmoja wa muungano". Really? Huu ni msiba wa Watanzania na sisi sote tumeguswa nao. Of course, hatuwezi kuwakosa watu ambao wameona huu msiba ni wa "Zanzibari" au si "watanganyika" kwa saababu ya hisia zao za utaifa (nationalistic attitudes). Hawa hatuna jinsi ya kuwasaidia kwani hakuna lolote litakalotokea upande wowote wa Muungano ambalo wao wataliona ni lao; litakuwa ni la "wale" au la "kwetu".

2. Sakata la Miss Tanzania kulaaniwa watu wanaona si haki kwa sababu ukilinganisha kati ya Miss Tanzania (tukio la kibiashara) na Kampeni za CCM - tukio la kiutawala ni hili la pili linagusa zaidi. Miss Tanzania ni onesho kama la mpira - ambalo linatafuta mshindi. Toka mwanzo kabisa nilitarajia asubuhi ya Jumamosi baada ya ajali serikali ingetoa kauli ya mara moja kuwa taifa limeingia kwenye maombolezo na "mikutano yote ya sherehe na burudani imeahirishwa ukiondoa labda harusi n.k). Lakini serikali haikufanya hivyo. Isingeweza kufanya hivyo kwa sababu tayari walikuwa wamejiandaa na uzinduzi wa Igunga kwa gharama kubwa. Sasa bila kuwa na kauli ya wazi ya maombolezo yameanza lini kila taasisi ilikuwa huru kuendelea na shughuli zake. Zanzibar wenyewe walitangaza maombolezo yanaanza Jumapili! Sasa kama serikali zenyewe hazikujua zinaanza kuomboleza lini hawa wengine wangefanya nini?

Lakini kuna jingine kwenye Vodacom na wengine wamelionesha - Vodacom siyo waandaji wa mashindano hayo; watu waliotakiwa kususiwa ni kina Lundenga - kama kuna mtu wa kususiwa. Lakini baadhi yetu hatutaki kuangalia juu ya Vodacom. Binafsi Vodacom nilishaweka pembeni kwani nina matatizo nao makubwa zaidi kwa muda mrefu na wala sina sababu ya kuwatetea. Ninachokiona ni kuwa watu hawataki kuwa wa wazi kusema kuwa kina Lundenga wangekuwa sensitive na kuahirisha hayo mashindano. Ni kweli yangeleta usumbufu kidogo kwa watu lakin ingekuwa nzuri kwao. Lakini si ndio matatizo ya tamaa za fedha pia?

3. Mazoea mabaya. Tayari tumeanza kuweka mazoea mabaya kiasi kwamba maombolezo hayana maana kwa baadhi ya watu. Nakumbuka kuna watu walinikoromea sana niliposhangaza na kitendo cha Rais Kikwete kwenda kwenye mechi ya mpira uwanja wa taifa wakati taifa liko kwenye maombolezo ya kifo cha Mzee Kawawa. Tena tulikuwa katika siku nzito na hotuba alitoa yeye mwenyewe Kikwete kutuambia juu ya kifo cha Kawawa. Sasa kama wao wenyewe wameshaanza kupoteza maana ya maombolezo kwa kuendelea na burudani sisi wengine inakuwaje? Na kuonesha kuwa hawana msimamo katika hili jana mechi ya ligi ya TFF imeendelea kama kawaida na kuna watu waliendelea kushangilia tena wakati huu tayari taifa liko kwenye maombolezo. Sasa kati ya Vodacom kuendelea na mashindano ya Miss Tanzania kabla ya maombolezo rasmi kuanza na Azam na wengine kucheza mpira wakati maombolezo rasmi yameanza ni yupi anatakiwa kususiwa kwa kutoonesha kujali utu? Napendekeza ni TFF!

4. Kama unakumbuka miaka kama miine iliyopita ilitokea ajali ya watoto 21 kufa kwenye ukumbi wa NSSF Tabora. Tena ilitokea Oktoba 1 siku ya Idi. Mimi na labda wachache wetu wengi tulikasirishwa sana na jinsi ajali ile ilivyotokea na tukapiga kelele watu wawajibishwe. Kaka leo mwaka wa ngapi? Hivi ripoti yao imewahi kujadiliwa Bungeni? Hivi ni ofisa gani wa NSSF aliwajibishwa? Badala yake tukaambiwa tunawashambulia watu tu kwa sababu ni NSSF. Lakini hatukutuhumiwa udini kwa sababu watoto wengi waliokufa walikuwa wanasherehekea sikukuu ya Idi! Leo kwa upande mwingine wamekufa watoto wengi na watu wazima wengi ambao nao baadhi yao walikuwa wanatoka kula Idi. Tunataka watu wahusika wawajibishwe lakini badala yake tunaambiwa ni Vodacom! Kwamba hadi rambirambi za Vodacom zinakataliwa! really? Kwamba kosa la Vodacom ni kubwa mno kuliko kosa la wazembe na mafisadi wanaondelea kuachilia ajali kama hizi kutokea?

5. Kwa miaka karibu mitano sasa nimekuwa nikiandika kuhusu suala la kujiandaa na majanga. Kwamba taifa letu halijajiandaa kwa majanga na mapendekezo ya mabadiliko ya sheria nimeyatoa na bila ya shaka wengine nao wamefanya hivyo. Kwa muda wote huo tena tumeenda mbali kabisa na kuelezea kujiandaa kwa ajali hizi za majini na barabarani na ajali za moto. Leo hii Manzese ikishika moto au Msasani kuna watu watasimama na kutuambia ni bahati mbaya na Mapenzi ya Mungu. Kaka viongozi wetu wameahalalisha kustahili kwao marupurupu na posho kibao lakini kwenye suala la usalama wa wananchi wa kawaida hakuna mastahili ya maisha yao.

Tumekubali kujenga jumba la bilioni 3 kwa ajili ya Gavana wa benki kuu kwa sababu anastahili; kiasi hicho kaka kingeweza kununua boti kadhaa ziwe mpya au zilizotumika kwa ajili ya patrol baharini au kwa ajili ya kusearch and rescue. Kaka, tumetenga zaidi ya shilingi bilioni 900 kwa ajili ya posho za watendaji mbalimbali serikalini kama "mastahili yao". Kaka kiasi cha dola milioni 133 kilikombwa kwenye wizi wa EPA kama unavyojua. Kwa miaka kumi iliyopita tumepoteza zaidi ya dola bilioni 10 kwenye corruption! Sasa leo tunakosa hata meli za kuokolea watu, hatuna helikopta hata moja ya search and rescue! Dar-es-Salaam yenyewe inategemea vikosi vya "fire" vya binafsi kwa ajili ya majanga! Sasa haya yote watu hawataki kuyaona kuwa yanahusiana na walioko madarakani. Mimi na wewe tunatambua wazi kabisa kuwa madhara ya majanga kama haya yangeweza kupunguzwa kweli kama tungekuwa na uongozi na utawala mzuri wenye kusimamia sheria (law enforcement).

Ninaelewa frustrations za watu kutoka kwenye upande wa hisia kuhusiana na suala la Vodacom. Kwamba katika mpangilio wa vitu mashindano ya urembo yangekuwa chini kweli kulinganisha na suala la kuokoa maisha ya watu. Ninaelewa kabisa kuwa hisia za watu zimeumizwa kwani ni kana kwamba Miss Tanzania haikujali. Kama hili ni kweli basi watu waende mbele zaidi. Wawatake wale wote waliumizwa na CCM kuendelea na kampeni Igunga tena kwa kutumia vikundi vya Burudani kurudisha kadi zao za CCM kama kweli wamechukizwa; na wale wote ambao wamechukizwa na kitendo cha TFF kuendelea na mechi wakati taifa liko kwenye maombolezo wagome japo kwenda mechi moja kupinga. Kupinga Vodacom peke yake - ni very selective.

Unless.. kama wengine walivyoashiria ni kuwa "mashindano ya vichupi". Kwamba kilichowakwaza watu zaidi ni kuwa hayo ni mashindano ya ulimbwende ambayo kwa kweli kabisa labda kwenye imani na hisia za watu wengine hayakutakiwa kabisa kufanyika. Ikumbukwe kuwa Zanzibar hakuna mashindano kama hayo. Sasa kama hili ni kweli basi isemwe kuwa ni hivyo lakini kama watu wa Zanzibar hawayatambui mashindano haya kwa sababu za kimaadili, inakuwaje wangependa yaahirishwe kwa muda wakati hawayatambui?

Kwa sisi wengine Vodacom ni tatizo na si kwenye kufadhili tu wengine tumekuwa nao kwenye matatizo kwa muda tu. Laiti wengine wangeona haya mapema.
 
Nitakujibu kwa kifupi sana..
1. Tukio la 9/11 halijawahi kuwa swala la New York na wala sijawahi kusikia pole zikitolewa kwa wakazi wa New York isipokuwa ni swala la Marekani nzima na duniani kwa sababu lilitugusa sote..Isipokuwa utawasikia wale wanaoshabikia upanbde wa pili ndio wakiweka madai haya aisdha ni janga la New York na Marekani. Vile vile haikuwa ktk janga na Mv Bukoba wala haiswihi kusema lile janga ni la Kikanda..Kitika ukaaji wako Marekani nadhani unafahamu vizuri sana serikali inapotangaza janga la kikanda na lile la Kitaifa. Na kwa kukujibu swali moja uliuliza huko nyuma, maafa ya meli hii yalifahamika Jumamosi asubuhi na mapema, tena naweza kwambia waandalizi wa Miss Tanzania walikuwa na taarifa hizo mapema. Mkuu wangu utamaduni wetu siku zote umetufundisha kwamba msiba wajirani yako ni msiba wako haya sii maneno matupu..

2. Kwa vile CCM wameendesha kampeni zao haiwezi kuhalalisha Voda ktk uwakilishi wao. CCM wanajulikana na tunawalaani kila siku ya Mungu iendayo na hakika kama mtu angeweka mada hapa inayowahusu CCM na ufunguzi wao wa kampeni za Igunga tungewaliza vile vile..Sasa isije mkafikiri kwamba tunapowashutumu Voda, upande mwingine tunawapongeza CCM la hasha siwapendi na kila nitakalo andika juu yao itaonekana chuki zangu binafsi dhidi yao au nafanya siasa za majitaka..Kosa la CCM haliwezi kuhalalisha ya Voda hata kidogo wao walitakiwa kujua umuhimu wa Miss tanzania kwa nchi yetu na sii umuhimu wake ktk biashara zao. CCM on the otherhand sishangai kwa lolote wanalolifanya, nimewachoka kama Wamisri na Mubarak!!

3. Tunachokijenga hapa JF ni tabia tofauti na ile ya JK au kiongozi mwingine yeyote. Tunatakiwa kuonyesha upeo wetu ktk kuelewa maswala muhimu ktk jamii ambayo ndiyo hutengeneza uhalali na haki stahiki ktk kuunda muungano wa nchi zetu.. Mimi na wewe tuna upeo mpana sana ktk maswala kama haya ambayo nina hakika kwa Watanzania wengi hawafahamu uzito wake. Na yawezekana hata hao waandaaji wa Miss Tanzania walijua ni janga dogo sana ambalo halina umuhimu kuliko maandalizi za Miss Tanzania. Sisi tunawapelekea ujumbe tofauti kabisa na wanatakiwa kuwa makiini na watumie elimu zao kuendesha mashirika haya nchini na sii uhuni uhuni mtupu.

4. Nakumbuka vizuri sana ajali ya Tabora lakini haikuzuia watu kupiga kelele na kusema halikuwa janga. Na kupuuzia kule kule kulikofanyika miaka hiyo ndiko leo kunakoendelea hapa JF. Na hizi sababu za kutetea vitu tusivyovijua ndiko hupelekea watu kuamini hakuna makosa yoyote yayliyofanyika isipokuwa ahadi yao imefika. Halafu basi uliposemna NSSF wawajibike ndivyo watu hawakukuelewa wewe (kama tusivyoeleweka sisi) kuwahusisha wao na usalama wa jengo wakati zipo taasisi zinazotoa kibali pasipo kwanza kulikagua jengo kaa linafaa kwa matumizi kama yale...Yet again, makosa yalifanyika na hayawezi kuhalalishwa kwa njia yeyote ile..

5. Mkuu wangu chochote kinachohusiana na CCM leo hii kwangu mimi nitakipiga vita wakati wowote kwa sababu viongozi wetu wameshindwa kufikiria ama ndio wamefikia kikomo cha wao kufikiria hivyo yote hayo ulozungumza hapo juu, ndio hunisukuma kuamini kwamba CCM has to go, tuanze mwanzo mpya pengine tutaweza kurekebishika yale yanayowezekana kwa wakati. Taratibu nasi tutarudi ktk Utu na Ubinadamu maanake sasa hivi hatuna tofauti na wanyama na hapa JF kuna mifano mingi sana inayobainisha ukweli huu.
 
Mkuu Mwanakiji na Mkandara,

Hebu tuwe wakweli hivi ni nani mbaguzi kati ya Mzanzibzri na Mtanzania Bara? Hawa watu (Wazanzibari) popote duniani kutana nao wanajitambulisha wao ni Wazanzibar na ukitaka ugomvi mwite mtanzania, sasa leo mnapiga kelele wao kuitwamsiba wa wazanibari?

Kwa kifupi huu msiba sasa ndo unaonyesha nyufa za katiba, hilo si siri nafikiri sote tumeliona. Ukija kuhuhsu kufunga shughuli zote, naomba kwanza mtafakari kauri zenu, msiba umetyokea Pemba yaani biashara zote hata Kigoma zisimame, watu watakula nini? hivi hamjua asilia 65% ya watanzania kula yao inategemea kama ametoka akafanya kazi? sasa watalipwaje hao? mtawalisha nyinyi?
 
Nitakujibu kwa kifupi sana..
1. Tukio la 9/11 halijawahi kuwa swala la New York na wala sijawahi kusikia pole zikitolewa kwa wakazi wa New York isipokuwa ni swala la Marekani nzima na duniani kwa sababu lilitugusa sote..Isipokuwa utawasikia wale wanaoshabikia upanbde wa pili ndio wakiweka madai haya aisdha ni janga la New York na Marekani. Vile vile haikuwa ktk janga na Mv Bukoba wala haiswihi kusema lile janga ni la Kikanda..Kitika ukaaji wako Marekani nadhani unafahamu vizuri sana serikali inapotangaza janga la kikanda na lile la Kitaifa. Na kwa kukujibu swali moja uliuliza huko nyuma, maafa ya meli hii yalifahamika Jumamosi asubuhi na mapema, tena naweza kwambia waandalizi wa Miss Tanzania walikuwa na taarifa hizo mapema. Mkuu wangu utamaduni wetu siku zote umetufundisha kwamba msiba wajirani yako ni msiba wako haya sii maneno matupu..

2. Kwa vile CCM wameendesha kampeni zao haiwezi kuhalalisha Voda ktk uwakilishi wao. CCM wanajulikana na tunawalaani kila siku ya Mungu iendayo na hakika kama mtu angeweka mada hapa inayowahusu CCM na ufunguzi wao wa kampeni za Igunga tungewaliza vile vile..Sasa isije mkafikiri kwamba tunapowashutumu Voda, upande mwingine tunawapongeza CCM la hasha siwapendi na kila nitakalo andika juu yao itaonekana chuki zangu binafsi dhidi yao au nafanya siasa za majitaka..Kosa la CCM haliwezi kuhalalisha ya Voda hata kidogo wao walitakiwa kujua umuhimu wa Miss tanzania kwa nchi yetu na sii umuhimu wake ktk biashara zao. CCM on the otherhand sishangai kwa lolote wanalolifanya, nimewachoka kama Wamisri na Mubarak!!

3. Tunachokijenga hapa JF ni tabia tofauti na ile ya JK au kiongozi mwingine yeyote. Tunatakiwa kuonyesha upeo wetu ktk kuelewa maswala muhimu ktk jamii ambayo ndiyo hutengeneza uhalali na haki stahiki ktk kuunda muungano wa nchi zetu.. Mimi na wewe tuna upeo mpana sana ktk maswala kama haya ambayo nina hakika kwa Watanzania wengi hawafahamu uzito wake. Na yawezekana hata hao waandaaji wa Miss Tanzania walijua ni janga dogo sana ambalo halina umuhimu kuliko maandalizi za Miss Tanzania. Sisi tunawapelekea ujumbe tofauti kabisa na wanatakiwa kuwa makiini na watumie elimu zao kuendesha mashirika haya nchini na sii uhuni uhuni mtupu.

4. Nakumbuka vizuri sana ajali ya Tabora lakini haikuzuia watu kupiga kelele na kusema halikuwa janga. Na kupuuzia kule kule kulikofanyika miaka hiyo ndiko leo kunakoendelea hapa JF. Na hizi sababu za kutetea vitu tusivyovijua ndiko hupelekea watu kuamini hakuna makosa yoyote yayliyofanyika isipokuwa ahadi yao imefika. Halafu basi uliposemna NSSF wawajibike ndivyo watu hawakukuelewa wewe (kama tusivyoeleweka sisi) kuwahusisha wao na usalama wa jengo wakati zipo taasisi zinazotoa kibali pasipo kwanza kulikagua jengo kaa linafaa kwa matumizi kama yale...Yet again, makosa yalifanyika na hayawezi kuhalalishwa kwa njia yeyote ile..

5. Mkuu wangu chochote kinachohusiana na CCM leo hii kwangu mimi nitakipiga vita wakati wowote kwa sababu viongozi wetu wameshindwa kufikiria ama ndio wamefikia kikomo cha wao kufikiria hivyo yote hayo ulozungumza hapo juu, ndio hunisukuma kuamini kwamba CCM has to go, tuanze mwanzo mpya pengine tutaweza kurekebishika yale yanayowezekana kwa wakati. Taratibu nasi tutarudi ktk Utu na Ubinadamu maanake sasa hivi hatuna tofauti na wanyama na hapa JF kuna mifano mingi sana inayobainisha ukweli huu.

Mkandara,

Mie huwa nafikiria saa zengine bora ningelizaliwa nchi nyengine na sio Tanzania maana unajua thinking capacity ya watanzania wengine huwa inanifanya nichoke kama sio kujisikia kutapika kabisa. Hakuna mtu anataka Vodacom wasifanye biashara bali walitakiwa wawe sensible particularly katika jambo kama hili ambalo linagusa jamii ya watanzania.

Mkandara umetolea mfano wa 9/11 mie natoa mfano BP Oil spill in Gulf of Mexico mwaka jana na nilishuhudia CEO akipoteza kazi na mshahara mnono simple kwa kukosa kuwa sensible katika kipindi kile cha Oil spill. Aliropoka majibu ya ovyo katika TV na kama haitoshi akaenda zake kula bata katika boti. Kilichofuatia BP walipigwa fine bab kubwa kutokana hasira from wamarekani wakiongozwa na rais wao na CEO wake alitimuliwa. Tukumbuke Oil spill in USA wamekufa bata mzinga, samaki na viumbe wengine bahari hakuna mwanadamu hata mmoja alipoteza maisha lakini CEO wa BP USA alipoteza kazi.

Vodacom wanatakiwa wafahamu hii ni jamii ya watanzania na hivyo kama walivyokuja kuwekeza nchi kwania ya kuleta maendeleo na vile vile tuwe nao pamoja katika msiba wa kitaifa kama huu. Wakumbuke vodacom ina wateja wasiopungua milioni 5 ambao wateja hao ndio wanaowaingizia faida. Sasa kama wateja wakipata msiba Voda watasherehekea??? Voda hawana tofauti na muuza duka ambaye inapotokea msiba mtaani kwake hufunga duka lake na kwenda kushiriki msiba na wenye mtaa. Sasa ukiwatukana wanamtaa kwa kupiga mziki watakuja kweli kwenye duka lako?

Perhaps, labda niwasaidie Voda kitendo chako cha kukosa hekima na kuamua kuendelea kusponsor na kushiriki katika miss Tanzania kimetusikitisha watanzania kwasababu kuu mbili kwanza kukosekana utu wa kutambua kuwa baadhi ya watanzania wamepatwa na msiba mzito kama huu. Pili kudharau wateja wake ambao ni sisi watanzania. Ingelikuwa nchi zilizoendelea CEO wa Vodacom sasa angelikuwa amekalia kuti kavu kwani wenzetu hawana mzaha na mambo haya. Hiyo inatokana na kwamba kama CEO ameshindwa kumudu jambo dogo kama hili la kufanya maamuzi muhimu je anaweza kumudu maamuzi ya kuendesha kampuni.

Ni jambo la kushangaza sana baadhi yenu mnaowasupport Vodacom na maamuzi ya kuendelea na Miss Tanzania huku mkijua kabisa moyoni mwenu wamechemka. Ndio maana nasema ningelikuwa Vodacom sasa ningelianza kufanya damage limitation kurepair image ya Vodacom na ningeliwatimua PR department yao na Director wao kwani wanaonekana hawana maamuzi ya busara.
 
Zitto hujaanza leo

Zitto,

Ni bora jambo hilo umelisema wewe mwenyewe, kwa ulivyoandika ni kwamba Vodacom na TBC1 sio tu wameonyesha kutojali bali ni kama usaliti fulani mkubwa sana kwa kutojiunga na watz wengine katika janga/msiba/tukio kama hilo.

Nataka kukuambia kipimo hicho cha usaliti na uchungu unaousikia ndio ambao Watz na CDM wanaopata pindi ambapo CDM kinakuwa katika tukio/janga/ issue fulani halafu wewe unaonyesha kutojali na unaendelea na mambo yako(mifano ipo mingi).

Sio kwamba naunga mkono TBC1 na Vodacom na Miss TZ, ila nakukumbusha kuwa hata wewe unawaumiza-ga sana Watz.............

Na kama ungekuwa umeumia sana usingezima simu ya Vodacom kwa siku moja bali ungejitoa kabisa kutumia mtandao huo- Huo ndio unakuwa msimamo wa mwanasiasa wa kweli ambaye yuko focused and mwenye kumaanisha
 
Naona ule mpango wake wa kuondoka na nusu ya Chadema bado uko hai.... Anatumia kila opportunity kupandisha chat. Hotuba yake ya kufunga Wizara ya Fedha + hii = Big problem kwa Chadema in future
\

Mhhhhh......watu waliona kitambo
 
Back
Top Bottom