Ajali ya Meli: SMZ yakataa misaada ya VODACOM

Mkuu wangu, hivi haya mashindano ya u miss si yanaandaliwa na BARAZA LA SANAA TANZANIA - BASATA? Vodacom ni sponsor tu. Hivi sponsor ana mamlaka ya kusimamisha mashndano ya kumtafuta miss tanzania?
Ligi kuu ya vodacom iliendelea jana kama kawaida. Vodacom walikuwa na uwezo wa kuisimamisha ligi? yeye si sponsor tu ...anayasimamia ligi ni TFF ..!
ninachokiona mimi humu ndani jamvi ni washindani wa vodacom ambao ni tigo, airtel na zantel wanajaribu kuichafua vodacom kwa kuwa wanashindwa kupambana nayo katika njia za kawaida. otherwise waende wakailaumu basata ambao ndio wadaaji wa shindano la miss tz, vodacom ni sponsors tu, hivyo hawapaswi kulaumiwa! kitu kingine cha muhimu ni kwamba nani alaumiwe yule aliyesababisha msiba utokee au yule ambae aliendelea kiufanya kazi wakati msiba unatokea?
 
Hakika huku ndiko kutumia masaburi haswahaswa.

Biashara ya Vodacom ni kuuza airtime kwa maana kwamba voucher zitauzwa tu hata kama serikali nzima ya Tanzania ingekuwa imeangamia kwenye meli hiyo.

Mnaotumia masaburi hamjui kwamba ni abiria wangapi walioripoti ktuoka melini kwa kutumia simu za Vodacom. Hivyo kwenye maafa kama haya ndipo mawasiliano yanapotakiwa zaidi na ndipo Vodacom inatakiwa kufanya kazi overtime kuliko wakati wowote.

Kumbuka ajali kadhaa ambazo Vodacom imeokoa kwa wavuvi kupiga simu na kisha kuokolewa.

BIahsara ya urembo si fani ya Vodacom. Kudhamini urembo ni msaada tu toka Vodacom kama msaada huo kwa waliofiwa.

TUje kwenye suala la uzembe. Nyinyi wenyewe humu JF mmepiga kelele mapema kwamba vyombo vyote vya habari vilikuwa vinatangaza porojo zingine asubuhi siku ya tukio. Kama ni hivyo basi JF itangazwe kuwa ni chombo rasmi cha habari maana ndicho pekee kilichoripoti mapema wakati vingine viliripoti mnamo saa mbili asubuhi.

Ukitumia masaburi kufikiri utashindwa kubaini kuwa maandalizi ya Miss Tanzania si rahisi kuyazima ndani ya masaa machache yale. Kumbuka watu wameshakata tiketi toka kokote nchini na wako D'Salaam. Nasikia siku ya tukio umeme haukuwepo na hivyo generator zilikuwa zinawaka pale mliani City.

Hivyo, ni nani angegharamikia cost za kuahirisha shindano. Na waliotaka liahirishwe hadi lini maana maombolezo ni siku tatu. Na kumbuka kuwa uamuzi si wa Vodacom kwani japo Voda ni mdhamini mmoja lakini shindano lile linahusisha taasisi mbalimbali.

Kitu kingine tunatakiwa tukumbuke kuwa tumeanza kujenga utamaduni wa kufanya mambo ya hiari kama lazima. Hivi nani aliyetufundisha kwamba kumsaidia mtu imekuwa lazima. Hivi mimi hata jirani angu kama amekufa nikakataa kwenda msibani, ni kweli mnaweza kunishangaa, lakini nani alisema kwamba ni lazima nihudhunike.

Huyo, Zitto mnayemsema kuwa amezima simu yake inawezekana alikuwa bado mtoto mwaka 1994 ambapo Rwanda na Burudni zilipata maafa wakati marais wa nchi hizo waliotunguliwa na ndege. Kumbuka ndege ile ilikuwa imetokea Dar kama ile helikopta ya John Garang ilivyotokea Kampala. Kukawa na amombolezo.

Lakini wakati East Africa inaomboleza, wanyarwanda hapa Mwanza wakafanya sherehe kufurahis Habyarimana amekufa. Malecela akiwa waziri mkuu akawakamata. Nyerere akakemea kwamba kama wameshaangilia kufa kwa Abyarimana tatizo ni nini.

Binafsi ninapofiwa ninaona kuwa ni jukumu langu. Jirani aje asije ni uamuzi wake na sina sababu ya kunung'unika wakati tatiz limenifika. Hivyo mtu au kampuni kutoa misaada hata kama imekuwa ni mazoea bado ni hiari hata kama hatupendi.

Kwenye red, sasa tatizo nini, na wao si wanahamasishana kwa hiari kutupa hizo chip za vodacom, by the way nimeshatupa from the same night. Je huo mfano wako wa raia wa Rwanda waishio Mwanza kufanya sherehe unataka kutuaminisha kuwa na wao walikuwa wanafanya sherehe kutokana na maafa hayo au? Hebu kafunguwe website TCU uangalie kama umepata mkopo au vipi hapa si saizi yako dogo.
 
Voda haijahukumiwa bali imekataliwa msaada wake tu,tena nadhani hii itakua nzururi kwa kwa kua wao ni wafanya biashara zaidi,huo msaada utawasaidia wao kukuza kipato chao.
 
simba vs azam ilichezwa lini kweli ? au ilikuwa kwa ajili ya kuwaliwaza wafiwa ? Why miss tz peke yake ? Baa ngapi zilikuwa wazi na watu wakiendelea na burudani kama kawaida.
Mbaya zaid watu walioshuhudia mis tz live na kucoment baadh ya matukio ndo hao hao waliokuwa wa kwanza kudai uzalendo kwenye social networks.
Pima mwenyewe nini cha kufanya
 
.............Naunga mkono hoja,nadhani ni kati ya mambo machache ambayo nimekubaliana na wanzanzibar.....VODACOM wanapaswa wajifunze utu,kuendesha shindano la umalaya wakati tuna msiba mkubwa namna hii,sidhani kama ni haki...watu wenye hekima wanajua kuwa Miss Tanzania ni shindano la kutafuta wasichana wazuri watakao uzika kwa mapedeshee.....

mkuu naona umemaliza kila kitu.
 
Tumepata taarifa kuwa Smz imekataa misaada ya Vodacom, na tunaambiwa ofisi za Vodacom znz ziko mashakani

Inaonekana kampeni ya kuisusia Voda imeshika moto, Mahmoud Thabit Kombo ndiye anayetumiwa na Vodacom kujaribu kuwaombea msamaha huko serikalini.

Vodacom wameahidi kutoa zaidi lakini taarifa zilizopo ni kuwa tayari bad publicity ishaspread na hata kama Vodacom wakiomba msamaha bado itakuwa ngumu kwa Serikali kujieleza kwa wananchi.

Wazanzibari waliopo UK (Zanzibar UK Trust na Friends of Zanzibar) wameamua kulalamika rasmi kwa ma trustees was Vodafone foundation UK.


Tutaendelea kuwahabarisha.

Duh! Wazenji wana Zantel yao kwa siku nyingi wamejitahidi kuhodhi soko la Zenji ikashindikana, naona sasa njia nyeupeee! Kuna wabongo wanadhani hapo kuna suala la utu, kama ni utu serikali inasimamiaje masuala ya usalama wa majini (siyo ya Sheikh wetu mtukufu).
 
MAFISDI, BIASHARA ZAO WATINGA KATIKA MAHAKAMA YA WALAZWA HOI KWA KESI YA DHIHAKA DHIDI YA MILA NA DESTURI YA YA MTANZANIA WAKATI WA JANGA

Hongera sana dr shein, vodakom ya rostam aziz ikae pembeni kabisa na dhihaka zao.

Wengine mnaopiga kelele mjue ya kwamba katika mahakama ya walazwahoi huwa hakuna huwa hakuna mkubwa sana, tajiri sana wala kitu kutembeza hongo kwa taifa zima hivyo msijali; wale wote waliokosea jamii yetu ya tanzania wataadhibiwa kwa foleni.

Hivi sasa ni zamu ya (1) vodakom ya fisadi rostam aziz, (2) baadaye mtatambua jinsi gani ccm iliyoa rushwa ya ubwabwa igunga siku na kula sendema jukwaani itakavyoadhibiwa, (3) na waandalizi wa miss tanzania wote kwa zamu. Msichezee hasira za walazwahoi na hasa pale ambapo mila na desturi hugeuzwa mzaha.

Chonde VODACOM ya Rostam Aziz, Miss Tanzania ya Lundenga, CCM, BASATA mjue hkuna kitu kinachoumiza mfiwa kama dhihaka kwa majonzi yake.

Masikini na wafiwa wetu nanyi matajiri kaeni pembeni na mali zenu. Bado nasema uamuzi wa SMZ ni sahihi kabisa!!!!!!!!!!!!
 
Leo CHADEMA wa JAMII FORUMS mnamtetea ROSTAM na kampuni yake ya VODACOM!!!!!

VODACOM mlikuwa mnalalamika ni kampuni ya FISADI ORIJINO leo imekuwaje?

Kweli FISADI ROSTAM kawashika pabaya
 
Jamani jamani, Watanzania tunakwenda wapi!. Utu wa mtu hauna thamani hata ya senti tano, lakini ukipotea hatuwezi kuurudisha kwa namna yeyote ile. Huwezi kuulinganisha na mali tulizonazo, leo tunazo, kesho hatuna, watu mamilionea pesa na mali zao wameziacha, lakini hawawezi kurudi. Kwa hili lilihitaji hekima na busara kidogo tu kwamba tunao-ishi nao ni watu, tunao-ongea nao ni watu, tunaofanya nao biashara ni watu, na wanaozaliwa ni watu. Kama tumefika pahala hakuna kuthamini utu wa mtu, basi tumekwisha watanzani na hilo ndio swali langu, Jamani Watanzania tunakwenda wapi?? Hii tabia ya ubinafsi hii inayojengeka ktk jamii yetu, siku wale waliowengi watakapoamua nao kuwa wabinafsi basi nadhani nchi hii hapatatosha, kama wengi wasemavyo.
 
Hivi TCU wameshatoa majina ya waliopata mikopo kwenye tovuti yao?...Naona upupu umezidi hapa jamvini.
 
Siku zote Wanzanzibari (serikali) hawajawahi kuunga mkono mashindano ya umiss. Partly for religious factors. Tukio la juzi ni coincidence tu kwa wao kuhalalisha walichokitaka siku zote. Mi nashangaa, badala ya kuzungumza kuwajibisha viongozi wazembe ambao kwa namna moja au nyingine wamepelekea kutokea kwa ajari hiyo public opinion inaelekezwa kwenye vodacam.

Pili ikumbukwe kuwa vodacom ni mshindani wa Zantel, kampuni ya Wazanzibar. Hii pia ni vita ya kibiashara. SINA HISA VODACOM , SINA NDUGU VODACOM WALA SINUFAIKI NAO KWA LOLOTE. WATANZANIA TUBADILIKE

Hivi unafahamu kinachofanyika katika mashindano ya umiss au unajaza post tu. Na kuhusu hiyo vita unayoisema, yes huwa wafanyabiashara wana vita za namna hiyo lakini ujuwe kuwa Zantel pia wanatumia facilities za vodacom katika kutoa huduma zao bara? Usiishi kwa hisia ishi kwa uhalisia, at least kampuni za simu ni miongoni mwa kampuni ambazo zina-public image isiyojinasibisha na tofauti za dini, kabila, umri wala utaifa. Kama ishu ni imani ya dini kwanini hawakususia before, pia je bara hakuna waislamu, mbona hawakutoa tangazo la kususia huduma? Nadhani hampati picture namna tatizo lilivyo-impact jamii ya kizanzibari. Ivi kweli kifo cha mtu mmoja katika familia kinafanana na vifo vya watu 18 kwa familia moja, tena karibu kila kaya. Je can you imagine kwamba familia hizi zitakuwa na nafasi ya kuangalia mashindano ambayo watu wanacheza, wanakunywa, wanaimba, yaani ni furaha tu?
 
Kitu pekee Wazanzibari wanazuiwa kufanya ni kulaumu serikali yao. Wanaaminishwa kuwa tatizo n vodacom na hivyo hasira zao zinaelekezwa huko. Sijui bank atawasaidia.
yaani wewe kweli ni great thinker nakuunga mkono hoja yako, na hii ndio hoja ambayo ilitakiwa ijadiliwe hapa jamii forum na sio vodacom
 
Leo CHADEMA wa JAMII FORUMS mnamtetea ROSTAM na kampuni yake ya VODACOM!!!!!

VODACOM mlikuwa mnalalamika ni kampuni ya FISADI ORIJINO leo imekuwaje?

Kweli FISADI ROSTAM kawashika pabaya

Huyu naye ana majonzi na anaomboleza vifo vya ndugu zetu waliozama baharini!
 
Wabongo acheni kuleta politics kwenye biashara,haya mambo yenu ya kufanya kila kitu siasa ndio yanawafanya mnalala giza na kuamka giza miaka 50 ya uhuru,acheni kufuata mkumbo,Zitto ni mwanasiasa na ndio kazi yake,alipiga kelele kuhusu madini na hatimaye mnajua nini kinachoendelea,labda na sasa anatafuta mlango wa kuingilia Voda? Tafakari.
 
Upuuzi mtupu...!

IMG_6969.JPG
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom