Ajali ya Meli: SMZ yakataa misaada ya VODACOM

ona miili ya hao watoto malaika .......kweli ni makosa makubwa sana voda wamefanya
 
mi nahsuri wasusie na TBC..wasiangalie tbc tena maana hii nayo kama tv ya taifa ilionyesha upuuzi mwingi sana
 
Vodacom ndiyo wadhamini wa ligi kuu ya Tanzania bara, je,uamuzi wa kuahirisha kwa mechi hupangwa na nani? Si TFF ndiyo wenye dhamana jamani? Hivyo hivyo ndivyo ilivyo kwa Miss Tanzania wandaaji kwa maana ya akina Lundenga si ndiyo wenye dhamana ya kuahirisha mashindano?

Katika hili mimi naona tunataka kuwatumia Vodacom kukwepa majukumu yetu kama serikali.Ni wajibu wa serikali ya SMZ kuhakikisha usalama kwa usafiri wa wananchi wake na hilo si jukumu la Vodacom'
 
upumbavu katika rangi zake, kwani VODACOM ndio iliyoendesha ile meli hadi ikazama, kwani vodacom ndio waliruhusu meli ya mizigo ijaze abiria, kwani Vodacom ndio walipaswa kugawa lifejackets baada ya meli kutoboka, ujinga mwinge kwani VODACOM NDIO WALIOVUJISHA MAJI YAINGIE MELINI...HATUFIKIRI KWA KINA ...Tunawaza kipuuzi.

Mbona hawaituni TBC iliyopiga densi mchana kutwa, badala ya kuhabarisha WaTZ, mbona hatusikii wale wakaguzi wa meli kule pemba wamechulkuliwa hatua gani?

kwa serikali kujiingiza katika mgogoro huo ni kutowatendea haki Wawekezaji hao na ni uonezi usiokubalika, by the way aja;li imetokea Huko Znz kwa muda ule hakuna alijua kwa hakika ni janga kubwa kiasi katika siku ambayo Miss Tz ilifanyika
mkuu wewe ni vodacom protect ila ujajishitukiahivi jirani yako akiwa na msiba na wewe ukafanya sherehe ni sahihi?au mpaka uwe umeua mtu ndio lionekane kosa
 
SMZ wako sahihi kabisa kususia hiyo misaada ya Vodacom, ambao walikuwa wakiendesha mashindano ya miss "uchi" wakati nchi iko kwenye maafa, hayo ndio maamuzi magum licha wenzetu wako kwenye matatizo, pia pongezi za dhati zimfikie mh. Rais wa Zenji kwa kuonesha skills zake ktk kusolve issue ya kuokoa watu kupitia kamati husika

Hebu nikumbushe' Voda ndio walikuwa waandaji wa miss Tanzania au wadhamini? Au ndio waliolazimisha mashindano yaendelee?!
 
SMZ wako sahihi kabisa kususia hiyo misaada ya Vodacom, ambao walikuwa wakiendesha mashindano ya miss "uchi" wakati nchi iko kwenye maafa, hayo ndio maamuzi magum licha wenzetu wako kwenye matatizo, pia pongezi za dhati zimfikie mh. Rais wa Zenji kwa kuonesha skills zake ktk kusolve issue ya kuokoa watu kupitia kamati husika
naomba unisaidie...angalia picha zilizowekwa kwenye hii thread! Unawachukuliaje wale wazungu waliovaa vikaptula vifupi wakiwa wanatoa huduma ya kwanza....mimi naona wana utupu kama wa ma wale ma miss! Jamani tuomboleze msiba huu kwa amani tu..badala ya kuanza kuwaza mambo mabaya kwa wengine...haisaidii kabisa!
 
Jamani we need to use just simple commonsense kabla hatujaandika or kutoa comment yoyote kwa hili.

Moja hivi hiyo misaada ni wa serikali au walioathirika na lile janga.

Pili hivi yule mshindi wa miss tanzania anapokwenda miss world anaiwakilisha vodacom or tanzania.

Tatu hili shindano lipo chini ya basata au vodacom.

Nne unaniambie nisusie je umenipa option gani kama kwangu napata mtandao huo tu?

Tano naomba uliza je hao smz wameshachukua hatua gani kwa walioruhusu meli iondoke wakati ipo ovarloded?

Sita je tunaelewa nini maana ya neno mdhamini?

Saba je shughuli zote za burudani j1 zilisitishwa (akudo, twanga pepeta, zanzbr stars nk) hawakufanya maonyesho yao?

Nane tushapata majanga kama hayo na yakajirudia bila statment za kueleweka toka serikalini(mabomu, now meli) na tume zenye kutafuna hela bila majibu na ahadi hayatatokea tena.

Mwisho nikiwa kama mwananchi wa kawaida na mwenye uchungu na hii nchi tuelekeze mawazo yetu zaidi kwa hii serikali yetu imekazana kununua mashangingi ya kisasa (mil 300) inabeba mtu mmoja lkn kivuko cha watu 1000 hakuna bajeti je hili ni sahihi? Watu tunalalamika tususie je ni watanzania wangapi wanapata kula yao ya siku kupitia haya mashirika na ukipunguza kipato chake ye anapunguza cost za uendeshaji kwa kupunguza ajira je utakuwa umemkomoa nani yeye au mtanzania mwenzako?

Mwisho anayetakiwa kuwajibika kwa yote ni selikali yetu mimmi na wewe na kama wangetoa tamko kusitisha shughuli zote za burudani nani angebisha?

Naomba kuwasilisha
 
No offence kwa znz atakayejibu haya maswali
1.kuna mshiriki yoyote wa miss tz kutoka znz?
2.ile miss tz ilipangwa toka mwezi wa 6 kuna watu walitoka mbal kuja kwa hii ishu je nani angegaramikia hasara yote+usumbufu?
3.je igunga ccm walifanya nn?
4.vodacom walikuwa wadhamini wa hii shehere ina maana ikitokea majanga kama haya kazi zote zisitishwe kwa muda?
4.je tarehe 9/12 kila mwaka tunasherekea nn? 5.znz ni nchi ina rais ina mipaka'bendera'wimbo wa taifa'mm nafikiri znz wanataka kutuendesha kwenye kila kitu haiwezekani jaman'ndio ni pigo kwa taifa lakin kuihukumu voda mnakosea sana.
 
Jamani we need to use just simple commonsense kabla hatujaandika or kutoa comment yoyote kwa hili.

Moja hivi hiyo misaada ni wa serikali au walioathirika na lile janga.

Pili hivi yule mshindi wa miss tanzania anapokwenda miss world anaiwakilisha vodacom or tanzania.

Tatu hili shindano lipo chini ya basata au vodacom.

Nne unaniambie nisusie je umenipa option gani kama kwangu napata mtandao huo tu?

Tano naomba uliza je hao smz wameshachukua hatua gani kwa walioruhusu meli iondoke wakati ipo ovarloded?

Sita je tunaelewa nini maana ya neno mdhamini?

Saba je shughuli zote za burudani j1 zilisitishwa (akudo, twanga pepeta, zanzbr stars nk) hawakufanya maonyesho yao?

Nane tushapata majanga kama hayo na yakajirudia bila statment za kueleweka toka serikalini(mabomu, now meli) na tume zenye kutafuna hela bila majibu na ahadi hayatatokea tena.

Mwisho nikiwa kama mwananchi wa kawaida na mwenye uchungu na hii nchi tuelekeze mawazo yetu zaidi kwa hii serikali yetu imekazana kununua mashangingi ya kisasa (mil 300) inabeba mtu mmoja lkn kivuko cha watu 1000 hakuna bajeti je hili ni sahihi? Watu tunalalamika tususie je ni watanzania wangapi wanapata kula yao ya siku kupitia haya mashirika na ukipunguza kipato chake ye anapunguza cost za uendeshaji kwa kupunguza ajira je utakuwa umemkomoa nani yeye au mtanzania mwenzako?

Mwisho anayetakiwa kuwajibika kwa yote ni selikali yetu mimmi na wewe na kama wangetoa tamko kusitisha shughuli zote za burudani nani angebisha?

Naomba kuwasilisha
mkuu ,hakuna hata mmoja atakaye kujibu kwa hoja hapo. Mimi nadhani kuna chuki fulani iko nyuma ya hii kitu ya U Miss!!
 
Ndugu zangu, huu msiba ni mkubwa sana. Karibu kila kaya Pemba imeguswa na huu msiba. Vodacom were in a very unique position to stop this useless pagentry kwa sababu wao ndio main sponsor. But they chose not to. Kila siku wanatupigia kelele kwenye tv na radio kuwa ndio mtandao unaoongoza Tanzania, wanaongoza kwa lipi? What do they (Vodacom) stand for?

Pili, kuna tofauti sana pale Mkuu wa nchi (haijilishi ni Tanzania au nchi nyingine) anapotanga msiba wa kitaifa. Hivyo nilitegemea kwa multinational company kama Vodacom wajue 'defination' ya msiba wa kitaifa. Watu waliokufa ni zaidi ya 200 na kuna miili mingi bado iko baharini. Narudia huu ni msiba wa kitaifa bendera ziko nusu mlingoti, vodacom wanajua maana yake?

Tatu, Kufanya kosa sio kosa, ila kurudia kosa. Ni zaidi ya masaa 24 sasa tangu hii blunder ya Vodacom itokee, lakini hakuna official statement toka kwa hii kampuni ya simu. Hivi wana communications manager hawa watu? Wanajua maana ya neno samahani? Kama kweli walikosea kwa nini wasiombe msamaha? Kukaa kimya maana yake wanatuambia sisi watanzania kuwa 'they were right' kuendelea na sherehe zao sio?

Nne, Vodacom ni sponsor mmoja, tunaomba mtu mwenye orodha kamili ya sponsors wote aweke hapa jamvini. Tunakata tujue ni kampuni ipi haina utu.

Tano na la muhimu kabisa. Nani alikuwa mgeni rasmi kwenye hii show ya ma-miss? Tunaomba jina lake, na alisema nini kama inawezekana tafadhali. Hawa watu ni wa kufundisha adabu.
 
Ninachokiona katika kadhia hii kuna mpango wa makusudi ku-divert attention kutoka wazembe waliohusika na uzembe huu uliosababisha kupotea kwa maisha ya watanzania wengi wasio na hatia na kuanza kupoteza lengo kwa kuwazungumzia wasiohusika na jambo hili.

Kama wanataka waisusie na TBC1 iliyokuw inapiga ndombolo siku nzima wakati taifa limepatwa na msiba mkubwa.Angalau hawa tunaweza kuwamudu maana ni chombo cha serikali lakini kuwagusa Vodacom ni kuwaonea kabisa.

Ningetamani kusikia kila mmoja wetu akipiga kelele kutaka Meneja wa bandari na Wazira husika Zanzibar pamoja na mtu wa SUMATRA zanzibar wafukuzwe kazi. Mengine haya ni propaganda kama kawaida yetu hata kweny mambo mazito kama haya.
 
Hakika huku ndiko kutumia masaburi haswahaswa.

Biashara ya Vodacom ni kuuza airtime kwa maana kwamba voucher zitauzwa tu hata kama serikali nzima ya Tanzania ingekuwa imeangamia kwenye meli hiyo.

Mnaotumia masaburi hamjui kwamba ni abiria wangapi walioripoti ktuoka melini kwa kutumia simu za Vodacom. Hivyo kwenye maafa kama haya ndipo mawasiliano yanapotakiwa zaidi na ndipo Vodacom inatakiwa kufanya kazi overtime kuliko wakati wowote.

Kumbuka ajali kadhaa ambazo Vodacom imeokoa kwa wavuvi kupiga simu na kisha kuokolewa.

BIahsara ya urembo si fani ya Vodacom. Kudhamini urembo ni msaada tu toka Vodacom kama msaada huo kwa waliofiwa.

TUje kwenye suala la uzembe. Nyinyi wenyewe humu JF mmepiga kelele mapema kwamba vyombo vyote vya habari vilikuwa vinatangaza porojo zingine asubuhi siku ya tukio. Kama ni hivyo basi JF itangazwe kuwa ni chombo rasmi cha habari maana ndicho pekee kilichoripoti mapema wakati vingine viliripoti mnamo saa mbili asubuhi.

Ukitumia masaburi kufikiri utashindwa kubaini kuwa maandalizi ya Miss Tanzania si rahisi kuyazima ndani ya masaa machache yale. Kumbuka watu wameshakata tiketi toka kokote nchini na wako D'Salaam. Nasikia siku ya tukio umeme haukuwepo na hivyo generator zilikuwa zinawaka pale mliani City.

Hivyo, ni nani angegharamikia cost za kuahirisha shindano. Na waliotaka liahirishwe hadi lini maana maombolezo ni siku tatu. Na kumbuka kuwa uamuzi si wa Vodacom kwani japo Voda ni mdhamini mmoja lakini shindano lile linahusisha taasisi mbalimbali.

Kitu kingine tunatakiwa tukumbuke kuwa tumeanza kujenga utamaduni wa kufanya mambo ya hiari kama lazima. Hivi nani aliyetufundisha kwamba kumsaidia mtu imekuwa lazima. Hivi mimi hata jirani angu kama amekufa nikakataa kwenda msibani, ni kweli mnaweza kunishangaa, lakini nani alisema kwamba ni lazima nihudhunike.

Huyo, Zitto mnayemsema kuwa amezima simu yake inawezekana alikuwa bado mtoto mwaka 1994 ambapo Rwanda na Burudni zilipata maafa wakati marais wa nchi hizo waliotunguliwa na ndege. Kumbuka ndege ile ilikuwa imetokea Dar kama ile helikopta ya John Garang ilivyotokea Kampala. Kukawa na amombolezo.

Lakini wakati East Africa inaomboleza, wanyarwanda hapa Mwanza wakafanya sherehe kufurahis Habyarimana amekufa. Malecela akiwa waziri mkuu akawakamata. Nyerere akakemea kwamba kama wameshaangilia kufa kwa Abyarimana tatizo ni nini.

Binafsi ninapofiwa ninaona kuwa ni jukumu langu. Jirani aje asije ni uamuzi wake na sina sababu ya kunung'unika wakati tatiz limenifika. Hivyo mtu au kampuni kutoa misaada hata kama imekuwa ni mazoea bado ni hiari hata kama hatupendi.
 
vodacom wanaendelea kutuudhi wananchi kwanza hawalipi kodi,pili ni kampuni ya fisadi RA na tatu hawana ubinadamu kama tulivyoona yaliyotokea zanzibar.WITO WATANZANIA TUSUSIE BIDHAA ZA VODACOM
 
1.mfano: Kwenye arusi kamati ya sherehe ikisema -sherehe imeahirishwa mc ana uwezo wa kuendelea kuitangaza?????
2. Kwa mawazo yangu,jukumu la kusitisha onyesho lile halikuwa mikononi mwa vodacom ila kwa mtu mwingine ambae tunaona kigugumizi kumtaja na kumlaumu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom