Ajali ya Meli: SMZ yakataa misaada ya VODACOM

SMZ wako sahihi kabisa kususia hiyo misaada ya Vodacom, ambao walikuwa wakiendesha mashindano ya miss "uchi" wakati nchi iko kwenye maafa, hayo ndio maamuzi magum licha wenzetu wako kwenye matatizo, pia pongezi za dhati zimfikie mh. Rais wa Zenji kwa kuonesha skills zake ktk kusolve issue ya kuokoa watu kupitia kamati husika

hawa si walikua wadhamini tuu au ukiwa mdhamini ndio unaendesha pia? Tumia akili jamani, msiwaonee!
 
Lakini vodacom si mwandalizi je tff nao watasusiwa kwani nao jana azam vs simba walicheza jana vodacom ni mdhamini si mwendeshaji wa ligi au mashindano ya miss tz naomba waunguja wafikilie kwanza
 
Na wafiwa nao wamesusa hio misaada...??!!!
Tuacheni siasa kwenye mambo ya maana pelekeni misaada kwa wahusika hayo mambo ya kususa na mengineyo mtayafanya baada ya hili janga kupita....

Kila mtu asuse kwa hiari yake kama watakataa kutumia mtandao wa Voda hilo ni chaguo lao lakini kwa sasa wapeleke misaada inapohitajika kwa wafiwa... unless kama wameshapata misaada ya kutosha (na kama ndio hivyo basi waanze kuwekeza ili wawaletee wananchi meli mpya na bora.)

Kwa nini wasijiangalie wenyewe kwanza kwa kuacha wananchi wanaangaika kwa meli/boti ambazo zimezeeka, na boti chache hadi watu wanajazana kwa kukosa usafiri?
 
ccm waliendelea na mbwembwe zao wakati wa msiba, alikua wakikata mauno kama nini kule Igunga , ni unafiki tu
292850_265340876820666_100000342668655_937397_1819611254_n.jpg


Wewe una chuki binafsi na CCM, hawa si wachezaji wa Yanga?
 
ckulaumu mana unatetea kibarua chako. kwani upo kitengo gani vodacom?
na wewe una chuki tu na wivu wa kike! kwani source ya hivo vifo ni VODA? mijitu ina majonzi lakini jinsi ilivyokuwa na miroho mibaya hata kujizuia kuandika upupu haiwezi!
 
Serikali ya Zanzibar haina mamlaka ya udhibiti kuhusu mambo ya Mawasiliano ya simu. Leseni ya kuendesha kusambaza mawasiliano hutolewa na TCRA iliyo chini ya Wizara husika kule Tanzania Bara.

Hivyo mwenye mamlaka ya kuwajibisha Vodacom au Kampuni yoyote ya mawasiliano ndani ya Jamhuri ya Tanzania ni TCRA na wala si vinginevyo.

Hapa ndipo hoja ya Tundu Lissu kuhusu muungano inapopata nguvu yake. Nitajadili hilo kulingana na michango ilioyoenda shule itakavyomiminika humu.
 
kazi ipo....ni kweli vodacom wana makosa.......wacha tuwapotezeee
 
Nyie wazenji, kama matatizo yanayowasibu wazenji mgeliyavalia njuga namna hii, Zanzibar could have been another Geneva katika maendeleo. Mnashupalia upuuzi. Mnawalazimisha watu wawe kama mlivyo. Not at all. Akitaka kuomboleza sawa asipopenda sawa.

All in all, hakuna aliyekuwa na nia ovu hata kidogo ya kudharau msiba mkubwa huu. Lakini msiwalazimishe kila mmoja alie. Anayetaka kulia ataguswa atalia asiyetaka mwacheni.
 
Mbona hata lıgi kuu ya Tanzanıa bara ılıendelea na vılevle wagomee mıchuano yoyote ya Tff?
 
nilitaka kulalamika lakini nilipoona hizi picha za maiti hawa sina haki ya kuwaamulia waZanzibari kwenye maamuzi yao

kwani Vodacom na wamiliki wa meli , wizara/vyombo vinavyohusiana na usafiri zanzibar ni nani mwenye kosa kubwa na anayestahili kuchomewa moto ofisi zake? mbona ligi kuu ya Vodacom iliendelea na hakuna complaints sana kama kwa haya mashindano ya u Miss? au hii kitu ya u Miss inafanana na mambo ya bar kule Zenji ndiyo maana jamaa wanataka kutolea tu upepo wao kwenye ofisi za Voda?
 
Mi sioni mantiki ya kuwahukumu vodacom, ajali imetokea wala si bahati mbaya ila imetolkea ;makusudi coz ya uzembe wa watu wanaojali pesa zaidi kuliko maisha ya watu.

Hata kama msibna ni wataifa lakini bado unabaki kwenye familia husika zaidi huwezi sema mi nishindwe fanya kazi niloiyeko Iringa coz ya msiba ulioko znz na kazi hii ndo inayosaidia mi niishi. Wakiwasusia voda si sjhanghai kwani waznz wengi wao wanatumia zantel, na sisi huku tukifuata tutakuwa wazembe coz wtanganyoika na waznz kutofautiana ni kawaida tu.
 
hawa si walikua wadhamini tuu au ukiwa mdhamini ndio unaendesha pia? Tumia akili jamani, msiwaonee!

Wasimlazimishe mtu kuwa na msiba ambao yeye nafsi yake haiutaki. Naye akifiwa usimjali. Tusilazimishane uchungu unatoka moyoni na si unafiki.
 
Mi nashangaa watu wanawaona vodacom ni wabaya baada ya kuserebuka na Miss Tz wakati wa msiba... tukio hilo si kubwa ukilinganisha na ukwepaji kulipa corporate tax toka imeanzishwa na hivyo kusababisha vifo vingi vya watanzania wengi zaidi (wanaokosa madawa hospitalini).
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom