Ajali ya Meli: SMZ yakataa misaada ya VODACOM

Kwa mfanya biashara mahiri tunasema Ndo ndo ndo si chululu. Na Vodacom wanalijua hilo ndio maana wameweka coverage nzuri huko.

Ni Bora kabisa kuwa BAN wasioperate na kuondoa kila kilicho chao kwani wao wana kibri na dharau dhidi ya maisha ya watu. Hili litakuwa fundisho kwao na wengine wanadharau mamlaka za SMZ.

Shame! Masuala ya biashara nayo mnayachukulia kisiasa?
Ukisikia kufirisika kimawazo ni pamoja na hili la kuwashupalia
Vodacom!
 
Kwani Yule mshindi alikuwa mshindi wa nini. Angalia title yake.

Kumbuka miongoni mwa waliofariki ni wateja zao? Je hawa wanathamini wateja wao?
Je maafa hayo yangetokea mafia au Ukerewe wangefanya hivyo?

Nasisitiza kuwa inabidi unafiki tuweke kando ili tatizo litatuliwe.
Kwenye maafa ndo tupo pamoja, hatujasahau kuwa hili swala la usimamizi wa shughuli za usafiri wajini Zanzibar WALISHAJITOA kwa vile si la Muungano.
Baraza La Wawakilishi lilitoa msimamo ulioafikiwa na wajumbe wote kuwa usimamizi wa shughuli za usafiri baharini si la Muungano.
Sasa leo watu wanakula matapishi yao hadharani kwa kukimbia kitanzi!!!
Vodacom mwamlaumu bure, pamoja na kwamba baadhi ya wamiliki wake ni mafisadi, lakini kwa hili la boti lenu mwawaonea.
Tunawahurumia sana wenzet huko Zbar lakini hili SI LA MUUNGANO.
 
<br />
<br />
Mkuu Raia Fulani, tafakari kabla ya kusema. Wazanzibar hawajitambui kivipi? Mbona hili shindano halikuitwa Miss Tanganyika. Hujui kwamba hakuna kitu Tanzania bila ya kuwepo Zanzibar. Acha upuuzi.

Ni kweli Miss Tanzania ni pamoja na zanzibar lakini Wazanzibar kuwashupalia Vodacom
inathibitisha kutojitambua pia kwa kuwa vodacom sio wanaoamua mambo kwenye
mashindaano haya ya Miss Tanzania bali wao wamedhamini tu, mdhamini ana mipaka yake
na hapa kuna Kamati ya utendaji iliyo chini ya uenyekiti wa Hashim Lundenga
 
Haya naona COMEDY inaendelea maana mpaka sasa hatuja mmiliki
wa meli ameshakamatwa ama laa,manahodha wako wapi nao
wameshakamatwa ama laa,aliyeiruhusu meli akijua imepakia kupita
uwezo wake ameshakamatwa ama laa,tunachoona ni watu wazima
wakiwa busy kweli kweli kupokea misaada na kuendelea kuomba
misaada on top wanaletewa wanachagua wakupokea, ndani ya voda
kuna magamba wawili natumai wanahisa ndani ya kampuni hawa ni
Alpha Tel ya muheshimiwa wa Monduli na aliyekuwa mzee wa igunga
sasa siji usikute bado wanatafutana pamoja na yote sidhani maamuzi
ya kukataa niyabusara lakini ndiyo aina ya viongozi tulionao na hapo
ndipo kikomo cha kufikiri nadhani tusubiri COMEDY Season II haijaisha
labda na TBL na SERENGETI sijui watatoa msaada na wakitoa tapokelewa
na
 
Kama angeshinda mpemba kwenye lile shindano wangemvalisha crown na kumshangilia kwa makofi na vigelegele!? Hao vodacom wangejisikiaje? Au akina Lundenga walishajua mshindi sio mpemba wakaamua kuendelea tu na shindano!?
Kwa ufupi wameonesha dharau kubwa sana kwa ndugu zetu na wanastahili adhabu. Vodacom wanatumia udhamini kujitanganza. Lakini walishindwa kutumia akili ndogo tu kutambua kuwa haikuhitaji kujitangaza kwa staili ile wakati tupo msibani. Huo ndio ujinga wao na kamwe hatungeweza kupokea ubani wa mtu aliyeshereheka huku akijua tuna maombolezo.
Wapeleke hizo hela kwenye promotion zao!
 
wameshajifunza kutokana na makosa hope next time watakua makini.
Hivi CCM kule Igunga mbona hatuwalaumu?
 
wameshajifunza kutokana na makosa hope next time watakua makini.
Hivi CCM kule Igunga mbona hatuwalaumu?

Vodacom hawajakosea chochote!
SMZ wanashindwa kuelewa kuwa kitendo chao cha kukataa ubani wa Vodacom ni UJINGA coz hizo hela sio za Vodacom ni zetu sisi wananchi ambao tumechangia kupitia sms zilizokuwa zinatozwa shs.1000. Vile vile wengine walichangia kupitia M-Pesa,lengo letu wachangiaji ilikuwa ni kfikisha ubani wetu kwa wenzetu wa Visiwani kutokana na msiba huu mkubwa.

Ikumbukwe kuwa kampuni kupitia Mwamvita Makamba waliiomba jamii ya watanzania na wateja wa Vodacom kwa ujumla wake wachangie fedha,hivyo basi SMZ kuzikataa hizo fedha ni kukataa fedha za wateja ambao ndio wa-TZ na sio kukataa fedha za Vodacom.Tunataka SMZ izipokee hizo fedha mara moja coz sio za Vodacom ni za wateja,kampuni imetumika kama "kapu" la kuzichangishia tu.

Nawasilisha...
 
Kwanini Vodacom imebebeshwa lawama nyingi kwa kutositisha onesho walilodhamini badala ya kuwabebesha lawama waliosababisha ajali ambao ni serikali ya ccm? Hapa pana mashaka.

Pili, katika kipindi hiki ambacho ccm wanavuana magamba, na baadhi ya wahusika wanaokwaruzana na wenzao ndani ya ccm wanahisa VODACOM, siwezi kuzuia hisia kuwa hapa pana mchezo mchafu. Nina mashaka na Move hii dhidi ya vodacom.

Sijasema vodacom hawajakosea - walikosea, japokuwa sijajua, wao kama wafadhili tu, uwezo wao wa kusitisha ghafla kitu ambacho walishaingia mkataba na wahusika wengine, ambao hata hivyo hawalaumiwi kabisa ktk sakata hili, kitu ambacho kinashangaza sana.

Mbona wanaosema tuwasusie vodacom, hawasemi tususie kuangalia TBC ambao walikuwa wanatumia kodi zetu kuonesha wanaokata viuno badala ya kututaarifa maafa ya kitaifa. Mashaka mengine haya.
Ninawaza tu, nina hitaji kueleweshwa pia.
[/QUOT

Nimepita tu Mkuu...Ila majibu yako fungua kwenye thread telezi si elekezi hapo juu kuhusu Mele kuzama utayapa...
 
Saafi saana hii inaitwa Keep hammering, Never over until it’s over. Thread kama hii hii imeshatiwa kwenye furushi huko habari mchanganyiko kusikosomwa sana kama hapa siasa forum.

INVISSIBLE Mkuu wangu sikuelewi unavyoonyesha kuguswa na hizi thread za VODACOM kwa mtazamo hasi, na umeamua kwenda kuzisokomeza huko Habari mchanganyiko kama takataka kwenye thread ya Bingmen mpaka imevunja Rekodi ya Post hapa JF haijawahi kutokea kwa namba ya michango na Views.

Unatutia shaka Mkuu, Unatushawishi kujiuliza VODACOM wamekupa nini? Maana unachokifanya ni kuuwa passé ya move wakati hoja imefika kwenye kina, mbona unaminya Uhuru wa Mawazo? Wacha watu waseme kupitia mijadala hii kwa kukubaliana kutokubaliana nidhamu itapatikana kwa watendaji wetu na somo kwa wazembe wengine.

Sifurahishwi na haka katabia kako Mkuu katika thread hizi kuhusu Mkasa wa VODACOM na Ajali ya Spice Islander huko Nungwi Pemba, au kama policy za forum zimebadilika tupe taarifa tutazingatia tu kuliko mchezo huu ambao kwa hakika unatia maudhi sana na kukatisha tamaa, tutasemea wapi sasa Tanzania hii kama na hapa napo tetenasi imeingia? Najua baada ya Muda itakuwa Kapuni na hii thread wala sitashangaa.

Mie binafsi sipost tena juu ya jambo hili maana Starter Pack yangu ilikuwa the right shot na imejibu na kitaeleweka tu, si wanasiasa kwa viongozi wa Dini wote wameamka na wanapaza sauti zao kila kona kuhusu kadhia hii… ntakuwa nadandia treni kama hivi kufikisha ujumbe wangu.

Wakatabahu

Mwanafamilia


GR


kaka haya malalamiko nimeyaona hata kule FACEBOOK

Huyu invisible kwanza siku ya tukio alikuwa kalala na wakati huo members kwenye the most popular forum ya JF kule siasa walikuwa over 600 lakini kutokana na utaratibu ambao hataki kuelezea sababu zake ni zipi ni lazima akiamka ndio apitishe threads au la

baada ya kulalamikiwa sana alipoamka ndipo thread ya kuzama kwa meli ikahamishiwa kule lakini within few hrs nadhani STEVE DII au PAIN KILLER wakaifanyia editing wanavyotaka wao...then zikaanza marathon za kufuta au kuhamisha threads za AJALI NA MAAFA zznzibar

sababu maybe hawaoni umuhimu wa kuwajulisha wananchi na hawaoni sababu za kuonyesha huzuni zao kwa sababu waliokufa wote ni WAISLAM na cha ajabu kule thread ya MWANAKIJIJI inayozungumzia same thing ilikuwa inaachwa.

Its really sad, mwenzetu kazidiwa na emotions badala ya kuacha watu watoe maoni yao withing the guidelines za JF!
 
bongo bana!!! sasa wamkomoa nani? VODACOM au WAHANGA??? walioukataa huo msaada ni wale ambao hawajapatwa na dhoruba

Laiti kama vodacom wangepeleka msaada moja kwa moja kwa wahanga sidhani kama wangeukataa.

kuna watu wameanza kuleta SIASA HAPO!!!

chukuwa msaada wape waathirika wenyewe ndo waukatae sio nyie ma MIDDLE Man

Sheikh huwajui wazanzibar na hasa wapemba naomba wasikie hivyohivyo kupitia vyombo vya habari wakikataa kitu wanakataa wapo radhi wawapigie kura marohani kuliko kulazimishwa kumpigia mtu wasiemtaka eti kwa kukosa choice.
 
kaka haya malalamiko nimeyaona hata kule FACEBOOK

Huyu invisible kwanza siku ya tukio alikuwa kalala na wakati huo members kwenye the most popular forum ya JF kule siasa walikuwa over 600 lakini kutokana na utaratibu ambao hataki kuelezea sababu zake ni zipi ni lazima akiamka ndio apitishe threads au la

baada ya kulalamikiwa sana alipoamka ndipo thread ya kuzama kwa meli ikahamishiwa kule lakini within few hrs nadhani STEVE DII au PAIN KILLER wakaifanyia editing wanavyotaka wao...then zikaanza marathon za kufuta au kuhamisha threads za AJALI NA MAAFA zznzibar

sababu maybe hawaoni umuhimu wa kuwajulisha wananchi na hawaoni sababu za kuonyesha huzuni zao kwa sababu waliokufa wote ni WAISLAM na cha ajabu kule thread ya MWANAKIJIJI inayozungumzia same thing ilikuwa inaachwa.

Its really sad, mwenzetu kazidiwa na emotions badala ya kuacha watu watoe maoni yao withing the guidelines za JF!

Aisee unajitafutia matatizo kuzungumza mambo yanayofanana na ukweli shauri yako ukipigwa BAN mie simo.
 
Yes SMZ, Yes Naunga mkono.. nawatia hamasa zaidi.. Watu wamezama majini.. ndugu zetu, marafiki zetu tuliowajali.. halafu nani asiye na utu anayetetea hili.. unaweza kutetea kwa kuwa hayajakufika, yakikufika utajua uchungu wake.. Imagine mojawapo wa hao washindani wa miss tz, nduguye angepotea kwenye ajali, au ndugu wa mmojawapo wa majaji wa shindano au.. unadhani shindano lingefana.. HAWANA UTU JAMANI..

MBAYA ZAIDI.. Chama tawala (usiumie, msinizibe mdomo wacha nseme) Ikiwa Bado shughuli za uokozi zinaendelea, Watu wako kazini wakiokoa ndugu zetu, mama zetu na dada zetu, walioshikiliwa na mauti ya maji (mbaya), watoto wasiojua lolote wanamezwa na ukatili wa maji, wanawake wasiojua kuogelea maskini ya mungu maji yanawazamisha kwa kifo cha uchungu na kilio, wanapiga kelele ila maji kwa ukatili yanaingia mdomoni na kuwanyamanzisha milele, wakati huo huo shirika la uokozi la Afrika kusini likikimbia kuingia ichini kuongeza nguvu ya kuwaokoa ndugu zetu hawa.. cha ajabu CCM Inazindua kampeni zake IGUNGA.. jumamosi hiyo-hiyo (Kitendo hicho unakiita UTU!!).. tena chini ya Aliyekuwa Rais wa JMT.. aibu.. sipati picha wakati SA rescue team inaingia nchini kwa helcopter, wanachungulia chini TZ, wanaona wanachi wamekusanyika, wanatamani kushuka wakidhani wamefika kwenye tukio, wanashangaa wanaona mauno ya ze comedy.. wakitupa macho kule mitaarabu ya TOT inamiminika.. nadhani watakuwa wamejiulia is this the right country or we were missleaded!!?? SMZ imulike tochi yake na huko CCM nao wapate BAN vilevile..

Upanga wa SMZ usiishie hapo, Maalim Seif, Mtu wa Pemba, Katibu Mkuu wa CUF, mtu tunayejua yuko makini.. wakati taifa bado liko kwenye maombolezo mazito.. jamaa anaorganize ufunguzi wa kampeni IGUNGA (No excuse.. ni katibu mkuu.. ndo mtendaji wa shughuli zote za chama hata kama siye yeye aliyeorganize ila hajitoi kwa hili, ni ofisi yake.. ni yeye).. asee!! hii sasa ni zaidi, Wapemba CUF mliyokubali kuifia zat uchaguzi, CUF kipenzi chenu !! ai huku watu wanapanda Punda, wanazindua kampeni.. aisee Mie sina tafsiri ya jambo hili.. Please please.. Inauma.. tafadhali SMZ BAN kitu hii..
Ni kweli kwamba msaada wa pesa unawasaidia wahanga, ila msaada kwa mtu anayekung'onga ni msiba mwingine!!
 
Mbona ujiulizi Rais Kikwete alihairisha Safari yake ya Ughaibuni kwa nini?

Je Vodacom au hata hao waandaaji wana mamlaka ya juu kuliko Rais kisheria?

Jiulize . Je maafa hayo yangetokea mafia au Ukerewe, je wangefanya shindano hilo?

Fikiria kabla kunena.


Cha kutumaini sina; ila damu yake Yesu;
sina wema wa kutosha; dhambi zangu kuziosha.................
Kwake Yesu nasimama ndiye mwamba ni salama.................
ndiye mwambani salama.

Njia yangu iwe yeye hunipa wokovu..................
Mawimbi yakinipiga nguvu zake ndio nanga...............
Kwake Yesu nasimama ndiye mwambani salama............
Ndiye mwambani salama.

Itengenezeni njia ya Bwana; yanyoosheni mapito yake; maana hakuna ajuaye siku wala saa atakayokuja mwana wa Adamu.
Jiulize ukifa leo utakwenda wapi mkono wa kuume alioketi Bwana Yesu au mkono wa kushoto aliketi mwovu.

Kesheni mkiomba msije mkaingia majaribuni.
Usihukumu usije ukahukumiwa maana kila auhukumuye naye atahukumiwa na kila auwaye kwa upanga naye atauwawa.

la msingi tutafute chanzo na kama chanzo ni uzembe basi hukumu iende kwa wazembe kwa mujibu wa kanuni na taratibu zilizowekwa ila sio kwa mujibu wa maneno yako au vile upendavyo iwe. Maana ingekuwa kila hukumu inatolewa vile mtu apendavyo iwe dunia ingekuwa zaidi ya machukizo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom