Inasikitisha kwa kweli kwa kutokuwa na takwimu sahihi ya watu waliokuwepo kwenye meli.
idadi wanayo ila kutamka ni aibu kwelikweli
ni sawa na kusikia baiskeli imepata ajali ikiwa na watu kumi!
Unashangaa!! Ndio nchi yetu ilivyo, kuficha mambo wakati yapo wazi kabisa.Duuuuuuuuuuuuuuuuuu!!!!!!!!!!!
nani atathibitisha kuwa walikuwepo humo ni zaidi ya 3000..
Mbunge wa Ole, Rajab Mbarouk alisema anakusudia kupeleka hoja binafsi bungeni ili kumwajibisha Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kwa tukio hilo.
Akizungumzia suala la Waziri Mkuu mbunge huyo alisema: Sisi ni wasemaji wa wananchi siyo Serikali. Nina mpango wa kupeleka hoja binafsi Bungeni ili Waziri Mkuu awajibike.
Alieleza sababu za kutaka Waziri Mkuu awajibike kuwa ni pamoja na Serikali kupuuza swali lake alilouliza bungeni kuhusu usalama wa vyombo vya majini hadi sasa.
Si rahisi kuthibitisha kama walikuwa 3000 kamili, lakini ni rahisi kuthibitisha idadi halisi yoyote kwani waliofariki na kuonekana, walionusurika na waliopotea ni watu ambao wana jamaa zao. Ni suala la kupita kila shehia (jina la kata kwa ZNZ) na kujua waliopotea, walionusurika na waliokufa na kuonekana.nani atathibitisha kuwa walikuwepo humo ni zaidi ya 3000..
Ndugu za abiria waliokuwa wakizama na meli ya MV.SPICE walianza kupata taarifa mara meli ilipoanza kuingia katika dalili za wazi za kuzama,hiyo ilikuwa ni usiku wa saa saba.Meli ilipozama na kubaki watu wachache juu ya mgongo wa meli simu ziliendelea kupigwa na wahanga hao.
Hatimae meli ilizama na baadhi ya wahanga kudandia kwenye mlingoti wa meli huku wakiendelea kuomba msaada kwa majonzi kwamba muda wowote na wao wangezama hiyo ilikuwa ni baina ya saa 9 -10 alfajiri.Baada ya hapo hakukuwa na mawasiliano tena na watu hao.Simu baina ya ndugu ndizo ziliwaamsha watu wengi kote Tanzania.
Kwa maelezo ya waliookoka shughuli hasa za uokoaji zilianza asubuhi.Ni wazi kuwa kulikuwa na uzembe katika kila nyanja.Baadhi ya nyanja uzembe ulikofanyika ni kwenye mashirika ya simu.Jee hakuna kitu cha kuonesha ongezeko la watumiaji simu muda ambap si wa kawaida?.
Uzembe mkubwa itakuwa ulifanyika Zanzibar kwenyewe. Vyombo vya Usalama na wahusika wa bandari walikuwa wapi wakashindwa kuona hali ya meli tangu saa 12.30 jioni?.Ofisi ya kukutisha tiketi kwanini haikuwa na mawasiliano na wenzao wa Dar kuonesha kuwa hakukuwa na nafasi tena ya kupakia meli itakapofika Zanzibar.
Hali ya tukio iliendelea kuripotiwa kama lilivyokuwa mpaka pale serikali ya Jakaya Kikwete na vyombo vyote vya ulinzi ilipoamka na kuteka shughuli yote.Kuanzia hapo watu wakatakiwa kupata taarifa zilizoitwa sahihi kupitia vyombo vya habari vya serikali vilivyofanya kazi kubwa ya kupotosha idadi ya waliookolewa na maiti waliopatikana.
Wabunge na wawakilishi huko Pemba wanastahiki pongezi kwa kuweza kwa muda mfupi kupata takwimu za watu waliopanda kwenye meli hiyo na ambao mpaka sasa wanahesabiwa kwamba wamekufa.Kufuatia juhudi zao gazeti la Mwananchi lilmeandika.
MV Spice ilipakia abiria 3000