Ajali ya fuso yazima shamrashamra za CCM Igunga

EasyFit

JF-Expert Member
Jul 4, 2011
1,269
1,082
  • Nusura achelewe muda wa kuchukua fomu.
MAPOKEZI yaliyokuwa yameandaliwa kumpokea na kumsindikiza kuchukua fomu mgombea ubunge wa Jimbo la Igunga kupitia CCM, Dk Peter Kafumu jana yaliingia dosari baada ya kutokea kwa ajali iliyosababisha kifo cha mtoto mwenye umri wa miaka 12.

Ajali hiyo ilitokea saa 5:30 asubuhi katika eneo liitwalo Parking (maegesho ya magari makubwa) Mjini Igunga, ambako mtoto huyo aligongwa na kupasuliwa kichwa na lori aina ya Mitsubishi Fuso.

CCM kilikuwa kimefanya maandalizi makubwa ambapo pikipiki aina ya Bajaji zaidi ya 20 na magari yalikuwa katika msafara wa kumpokea Dk Kafumu katika eneo hilo la Parking.

Baiskeli na pikipiki za kawaida pia zilikuwa katika mpango wa mapokezi huku zikiwa zimepambwa kwa bendera za CCM na kila upande wa mji ukiwa na bendera hizo.Kutokana na tukio hilo, Dk Kafumu alilazimika kuchukua fomu bila shamrashamra zozote kutokana na muda kutomruhusu kuahirisha uchukuaji huo.

Msimamizi wa uchaguzi jimbo la Igunga, Magayane Protas alisema pamoja na tukio hilo kutokea ni lazima fomu zichukuliwe kwa kuwa kesho (leo) hatakuwa na nafasi kutokana na kuwapo na ratiba nyingine ya kikao cha viongozi.

“Nimewaambia lazima wachukue fomu leo kwa kuwa kesho (leo) nitakuwa na kikao na uongozi,” alisema.

Kafumu alichukua fomu saa 8:00 mchana.

Source: Mwananchi.
 
Yote haya ni sehemu tu ya matokeo ya KILIO CHA WALAZWAHOI nchini pindi wanapoona genge la mafisadi nchini wakiingia Igunga kwa mbwembwe, mikogo na ufedhuli wa kujitutumua na mali ya wizi wa mali za umma kwenye kampeni zao.

Ni sharti Mafisadi wote wamrudie Mungu nchini, kutubu na kurudisha mali zote hazina ya taifa; la sivyo zahama huenda usiishe kwao tangu sasa. Mambo yataendelea KI-GUNDU GUNDU KWA CCM kila kona wasipotubu hadharani kwa umma wa Tanzania.

gundu tayari kwa Magamba au ndio wametoa kafara????
 
Sidhani kama ni busara kuchanganya kifo cha mtu na siasa. Nadhani watu hawaelewi uchungu wa kumpoteza mtu lakini likikukuta ndiyo utapata akili. Mungu aiweke roho ya marehemu peponi.
 
Ifike mahali sasa CCM waache kutumia watoto/wanafunzi wa shule za msingi kwenye kikutano/kampeni zao. Kwani wamekuwa wakiwatumia watoto ili kuaminisha wananchi kuwa mikutano/kampeni zao zinahudhuriwa na watu wengi
 
Sote kwa pamoja tukemee JINI UFISADI ambayo hivi sasa Rostam Aziz aonekana kumachilia huru na kuanza kufyonza ovyo damu za Watanzania kwenye kampeni Igunga.

Jini ufisadi, toka hapo Igunga kuwaachia wenyeji kujichagulia kiongozi wampendaye baada ya zaidi ya miaka 15 kupita bila wao kupata fursa ya kufanya hivyo kwa maslahi yao wenyewe!!!!!!
 
Sidhani kama ni busara kuchanganya kifo cha mtu na siasa. Nadhani watu hawaelewi uchungu wa kumpoteza mtu lakini likikukuta ndiyo utapata akili. Mungu aiweke roho ya marehemu peponi.

sidhani kama ni busara inabidi maneno umwambie mgombea wako wa ccm anayepita kila mahala akitangaza msiba huo na kutaka
kutumia kama mtaji wake wa kisiasa badala ya kuwaombea na kuiachia familia, majirani na viongozi wao wa kidini ktk hiki kipindi kigumu kwao. CCM haiwezi kukwepa lawama ktk hili kwa maana wameshaonywa siku nyingi tabia ya kutumia watoto wadogo kwenye siasa badala
yake wawaache wasome lakini wamekuwa wakikaidi na wamefikia mahala hapa iringa vijijini kufunga shule kadhaa za msingi kwa ajili ya
kwenda kuhudhuria mkutano wa mgombea wa ccm mwaka jana 2010. ajali ni ajali lakini ajali zingine ni za uzembe kwani angekuwa
shuleni mtoto huyu badala ya kusombwa na ccm kila mtu anajua yasingetokea haya yaliyotokea kwahiyo ccm wako responsible na kifo cha mtoto huyu.
 
Dalili ya mvua ni mawingu.
Magamba yametabiriwa vibaya.
Daktari arudi kwenye nafasi yake aachane na mambo ya siasa.
 
Hawa nao wamezidi na mafuso yao, ona yameanza kuua watu wasio na hatia, naichukia CCM kama nimchukiavyo shetani.
 
Nasikia lilikuwa limetoka kusomba wanaCCM wa majimbo ya jirani kuja kuongeza nguvu.
 
Sidhani kama ni busara kuchanganya kifo cha mtu na siasa. Nadhani watu hawaelewi uchungu wa kumpoteza mtu lakini likikukuta ndiyo utapata akili. Mungu aiweke roho ya marehemu peponi.
msitumie malori kubeba washabiki wenu!
Kama wanawakubali waacheni waje wenyewe, kwa nini mnawabeba kama ng'ombe?
 
Sidhani kama ni busara kuchanganya kifo cha mtu na siasa. Nadhani watu hawaelewi uchungu wa kumpoteza mtu lakini likikukuta ndiyo utapata akili. Mungu aiweke roho ya marehemu peponi.
Wa kulaumiwa ni huyo kafumu anayetumia kifo cha huyo mtoto kama mtaji wa kisiasa. Oooh tutashiriki kwenye kumuhifadhi...maneno kibao, ila kuna dalili kuwa CCM wamemtoa kafara huyu malaika wa mungu! shame on them wamejipa laana hawashindi N'go!
 
Sidhani kama ni busara kuchanganya kifo cha mtu na siasa. Nadhani watu hawaelewi uchungu wa kumpoteza mtu lakini likikukuta ndiyo utapata akili. Mungu aiweke roho ya marehemu peponi.
Mkome kutumia watoto kwenye siasa.
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom