Ajali ya Basi la ABOOD toka Morogoro

mizambwa

JF-Expert Member
Oct 8, 2008
4,422
1,790
Wajameni, ajali imetokea eneo la Mbezi Kimara. Likihusisha basi la kampuni ya ABOOD lililokuwa linatoka Morogoro kuelekea DSM. Inaelezwa kuwa kulikuwa na msafara wa kiongozi, hivyo dereva wa basi kwa kuwa alikuwa katika mwendo kasi alishindwa kulizuia basi likamshinda na kupinduka.

Kamanda wa Poilsi mkoa wa Kinondoni amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na watu kumi wamejeruhiwa vibaya.

OMBI: kwa mwenye taarifa mpya kuhusu ajali hii tunaomba kujulishwa.

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Pole kwa walioumia.
Wakati mwingine inaudhi sana kwa hawa viongozi kusimamisha wananchi waliowachagua kutumia barabara kisa tu eti ni mheshimiwa,wote tuwe na haki ya kutumia barabara.
 
Kwa mujibu wa redio one waliojeruhiwa ni 10 na hadi sasa hakuna taarifa za kifo/vifo
 
Duh inasikitisha saana poleni sana majeruhi ni kiongozi yupi na je,ni safari yenye tija kitaifa au ndio zile za ukaguzi wa miradi ?
 
dah... huruma bure yan!
na kweli mgari kama ule ukiwa kwenye mwendo kasi kuupisha msafara inakuwa vigumu kweli mmh!
 
Enjo...are yuu siriazi?
yes l am more than serious, kama huo msafara wa huyo kiongozi ungechukua tahadhari mapema km vile kutanguliza pikipiki au defender za askari huenda dreva wa basi hilo angepunguza mwendo taratibu na angepaki basi lake pembeni na ajali isingetokea, NIMESHAKUMBANA NA MKASA KAMA HUU TENA ALIKUA PINDA ALMANUSRA NIINGIE MTO RAU,
 
Hii misafara hadi inaboa jamani, ndo mana hawaoni uharaka wa kutafuta suluhisho la foleni Dar. Maana wao wanapita free. Hivi viongozi wetu wanaweza ya Thomas Sankara kuendesha gari lake town akiwa na mlinzi wake tu?
 
Magufuli wekeza fedha kwenye hiyo barabara ya Dar - Moro umalize hizi ajali... Wenzio Kenya wamejenga ile wanaita Thika SUPER HIGHWAY yenye LANES 10 kwa umbali wa KM 50, nyie mnaishia kugawana posho bila kuleta maendeleo ya kweli kwa hii nchi. Hii serikali ya awamu ya nne ni janga la kidunia.
 
baba mwanaasha anatusumbua kila j'mosi anaenda msoga kutambika,basi foleni tokea ubungo mpaka mailimoja-kibaha
 
Magufuli wekeza fedha kwenye hiyo barabara ya Dar - Moro umalize hizi ajali... Wenzio Kenya wamejenga ile wanaita Thika SUPER HIGHWAY yenye LANES 10 kwa umbali wa KM 50, nyie mnaishia kugawana posho bila kuleta maendeleo ya kweli kwa hii nchi. Hii serikali ya awamu ya nne ni janga la kidunia.

Hii serikali ya awamu ya nne ni JANGA - Ulukolokwitanga - JF Senior Expert Member
:A S embarassed:
 
yes l am more than serious, kama huo msafara wa huyo kiongozi ungechukua tahadhari mapema km vile kutanguliza pikipiki au defender za askari huenda dreva wa basi hilo angepunguza mwendo taratibu na angepaki basi lake pembeni na ajali isingetokea, NIMESHAKUMBANA NA MKASA KAMA HUU TENA ALIKUA PINDA ALMANUSRA NIINGIE MTO RAU,
Its owkay kama hiki ndicho ulichokimaanisha kwani mimi naamini msafara hauwi msafara kama hayo uliyoyataja yapo.. sasa nilisghangaa kutaka kumsulubisha kiongozi wakati yeye angekuwa hana kosa...
 
ingelikuwa ni raha kama na Viongozi nao wanakaa katika foleni, wangejua umuhimu wa kutatua kero ya foleni. Lakini leo wakisafari sisi tunawekwa pembeni hadi wapite kwa mwendo kasi kabisa. Na bila huruma wanasababisha ajali kama hizi. Ndio maana hawajui kero hii.

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Mara nyingi hii misafara husababisha ajali. Tatizo mamboyao ni kukurupuka tu. Poleni sana wahanga wa ajli hii
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom