Ajali Ubungo Riverside

Bahati mbaya wakifa watu < 10 watu wengi hawashtuki, lakini haya ndo madhara ya kujenga barabara kwa kuunga unga kila wakati. Ajali nyingi zinasababishwa na ujenzi mbovu wa barabara zisizokidhi kiwango kinachotakiwa. Watu wamefanya deal hii miradi kiasi cha kila mwaka zinatengwa pesa za ukarabati. Yaani hiki kizazi kilichopo madarakani kina madhambi yasiyosahaulika.RIP waliopatwa na mauti, na get well soon majeruhi wote.
 
Ninasikitika kuawaarifu kua kuna ajali mbaya imetokea Ubongo Riverside ambapo gari aina ya lori limeacha njia na kugonga watu.

Kwa uchache inasemekana maiti 20 zimeokotwa eneo la ajali.

Habari zaidi zitawajia hivi punde
bwana ametoa bwana ametwaa jina lake lihidimiwe
 
Oh my god watanzania wenzetu wanapoteza maisha yan kila siku. Mungu awapumzishe kwa amani na kuwafariji ndugu zao katika kipindi hiki kigumu
 
Hii sasa ni freemason ila ngoja wale wakombozi walioko mtwara watatua hapo Dar na hata huku kanda ya kaskazini na patachimbika. Poleni wote waliofikwa na mauti na marehemu wote walale kwa Amani ya bwana!

hapo kwenye red sijakupata
unaweza kudadavua nielewe?
 
Wanaofanya mzaha na mambo ya kusikitisha kama haya ni utoto au uhayawani?! wewe unayeongeza idadi ya vifo unataka tukuelewe kwamba unafurahia watu kufa au nini?!

Ni maiti nne sio ishirini na ni magari mawili madogo yaliyohusika na ajari sio daladala
 
Nimepita hapo mahali hivi punde. idadi ya marehemu haiwezi kufikia hiyo idadi ulitoitaja Mkuu

Mkuu kwa taarifa niliyoipata toka kwa shuhuda mtu mmoja alikuwa bado kabanwa ndani ya gari yupo hai..na watu watatu wamefariki dunia mmojawapo akiwa mjamzito ( kichwa chake kimetanganisha na kiwiliwili )
 
Poleni sana mlionusurika na marehemu Mungu awapumzishe kwa amani, km kuna uzembe umetendeka wahusika wachukuliwe hatua. mwenye uwezo wa picha pls.
 
Wakombozi gani wa mtwara?ebu tujuze tafadhali mkubwa.
Hii sasa ni freemason ila ngoja wale wakombozi walioko mtwara watatua hapo Dar na hata huku kanda ya kaskazini na patachimbika. Poleni wote waliofikwa na mauti na marehemu wote walale kwa Amani ya bwana!
 
Ninasikitika kuawaarifu kua kuna ajali mbaya imetokea Ubongo Riverside ambapo gari aina ya lori limeacha njia na kugonga watu.

Kwa uchache inasemekana maiti 20 zimeokotwa eneo la ajali.

Habari zaidi zitawajia hivi punde
unahuakika na unachosema kuwa ni watu 20? usije kutupa habari ambazo siyo haitapendeza
 
mimi nilikuwepo tanker lilkuwa linatoka ubungom kuelekea buguruni kufika kituo cha daladala cha riverside likakuta daladala limepaki njiani na kwa kuwa lilikuwa mwendo kasi likashindwa kufunga breki likapanda ukuta na kugonga gari zilizo kuwa kwenye foleni zinatoka buguruni kuja ubungo,yule mwenye daladala mwenye makosa kakimbia,ajali ni mbaya sana kuna mama kakatika kichwa hapohapo,lecturer mmoja wa chuo kikuuu namfahamu kwa sura amepona pia ila amenusurika na gari yake.

Tulikuwepo mahali ajali ilipotokea,Kwa kweli hii ajali ilikuwa mbaya sana.leo ni mwenyezi Mungu tu aliyetuokoa,nawaombea waliopoteza maisha na Mungu awape faraja ndugu jamaa na marafiki.sheria za usalama barabarani hazifuatwi,watanzania hatujifunzi ........! kilichotukinga ni gari iliyokatiza mbele yetu sisi tukitokea barabara ya Buguruni,hata rafiki yangu alipaniki na kuachia usukani

duuuuhhh...!!! mbona hayo maeneo nina ndugu zangu....???

hebu tuwekeee picha za ajali hiyo hapa.....!!!
 
Mkuu kwa taarifa niliyoipata toka kwa shuhuda mtu mmoja alikuwa bado kabanwa ndani ya gari yupo hai..na watu watatu wamefariki dunia mmojawapo akiwa mjamzito ( kichwa chake kimetanganisha na kiwiliwili )
asee inasikitisha sana na hii ndio idadi ambayo nami nimeisikia
 
aaaah pumzika kwa amani muuza pweza wangu pale pembeni ya daraja....
 
Back
Top Bottom