Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,466
- 113,548
Nimeona TBC News usiku huu, kumetokea ajali nyingine ya basi la abiria katika kijiji cha Pandambili, Dodoma, ni basi la Taqwa lililokuwa likielekea Bujumbura, limepinduka na limeteketea kwa moto, Watu wengi wamepoteza maisha akiwemo dereva wa gari hilo.
TBC ilionyesha live basi likiungua na fire zikifika wakati basi limeishateketea.
Pia leo nimeshuhudia efective reporting ya vyombo vyetu vya habari, kuleta live kwa maana haswa ya live kama kwenye CNN.
Ni Pandambili ndipo palipotokea ajali iliyokatisha maisha ya Mbunge wa Tarime, Chacha Wangwe.
Mlioko Dodoma naomba tupatieni more update..
Kwa mujibu wa Blog ya Likwengule inayomilikiwa na Beda Msimbe taarifa ndio hii
Mtu mmoja amefariki dunia na wengine kupata majeraha baada ya basi walilokuwa wakisafiria kuelekea Bujumbura wakitokea Dar es salaam kupinduka,kushika moto na kuteketea katika eneo la Tanana, Kongwa mkoani Dodoma.
Taarifa kutoka eneo la ajali zinadai kuwa basi hilo lilipinduka kwanza kabla ya kushika moto na kuteketea.Mtu aliyefariki katika ajali hiyo ametambuliwa kuwa ni dereva wa basi.
Majira ya alasiri baada ya moto kuzimwa juhudi zilikuwa zinafanyika kulinyanyua ili kuweza kutambua idadi halisi ya maisha yaliyopotea.
Basi hilo la Taqwa lilipata ajali majira ya mchana na hakuna uhakika wa mali zilizoweza kuokolewa.

Mod, rekebisha headline, siyo breaking news tena, kumbe ajali imetokea asubuhi, mimi nimeiona TBC breaking news usiku huu nikafikiri ndio saa hizi kumbe ni recorded.
Mpaka sasa comfirmed dead ni wawili, dereva na mtoto mdogo mmoja.
Mungu awafaruji wafiwa, na uponyaji wa haraka kwa majeruhi.