Ajali mbaya Kibamba - Dar

Invisible

Robot
Feb 11, 2006
9,075
7,873
Kuna daladala imegongwa na Lory la mafuta muda si mrefu eneo la Kibamba - Morogoro Rd, Dar es Salaam.

Zimamoto wameelekea eneo la tukio kuzima moto. Taarifa zaidi naamini zitafuata

Kutoka Global Publishers
==========================

1269494529_breakingnuznewwwwww.jpg

ONYO PICHA HIZI SI NZURI KABISA

Leo majira ya saa kumi na nusu alfajiri, lori lenye namba za usajili T 189 ABP na tela lake lenye namba za usajili T 192 ABP lililokuwa limebeba mafuta kutokea jijini Dar es Salaam kuelekea Kibaha Pwani, limepata ajali mbaya na kuliangukia basi dogo la abiria (Hiace) lenye namba za usajili T 615 AJW katika eneo la Kibamba CCM, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, na kusababisha basi hilo dogo kupondeka vibaya.

Ajali hiyo ya kutisha imesababisha vifo vya watu 7 waliokuwa ndani ya basi dogo, baada ya lori hilo kulilalia basi hilo lililokuwa likitokea Kibamba kwenda Ubungo. Akiongea na mwandishi wetu aliyefika eneo tukio, Kamanda Mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani, Mohamed Mpinga , alisema kuwa basi hilo dogo aina ya Hiace lilikuwa na abiria saba ambao wote wamefariki dunia, na kati ya maiti hizo, ni maiti mbili tu ndizo zilizoweza kutolewa hadi muda huu tena zikiwa vipandevipande.

Katika maiti hizo zilizotolewa, moja ni ya mwanamke ambae hakuweza kutambuliwa kwa wakati ule na na mwanaume aliyetambuliwa kwa jina la Shukuru Hussein, maarufu kama Kibwetere, mkazi wa Kibamba. Aidha Kamanda Mpinga aliongeza kuwa bado utaratibu unaendelea kwa kuwa lori lilikuwa limejaza mafuta hivyo imeleta ugumu katika utoaji hadi mzigo wote utakapoisha na kuweza kufanya utaratibu wa utoaji.

Kamanda Mpinga aliweza kumtaja dereva wa lori ambaye amekimbia mara baada ya tukio hilo kutokea kuwa ni Kudura Adam na mmiliki wa Lori hilo ametambuliwa kwa jina la Mahamudu Mohamed.

Hata hivyo baada ya ndugu wa mmiliki wa Hiace kupatikana na kudai mwenyewe yuko Mkoani Kilimanjaro, walisema kuwa mmiliki huyo anaitwa Selemani Khalfan na Hiace yake huwa inalala Ubungo Kibo maeneo ya Rombo na kumtaja Dereva wa Hiace hiyo kwa jina moja kuwa ni Seif na Kondakta wake Faraji Ismail Kalama ambao mpaka sasa bado maiti zao hazijatolewa eneo la ajali.

1269506599_1.jpg

...lori likiwa limeangukia hiace ikiwa kama chapati..

1269506599_3.jpg

...mwili ukiwa umenasa kwenye gari hilo

1269506599_4.jpg

...waokoaji wakiangalia jinsi ya kunasua hiace lililo chini ya lori

1269506805_5.jpg

...sura ya mbele ya lori hilo

1269506805_8.jpg

...sura ya ajali hiyo nyuma ya lori...angalia jinsi hiace ilivyo!

1269506805_10.jpg

...mwili wa mtu anayedhaniwa kuwa kondakta wa daladala hilo

1269506805_11.jpg

...wana wa usalama eneo la tukio

1269506805_12.jpg

...mashuhuda wa ajali

1269506805_15.jpg

..mzee Hussein Mwagilo akilia kwa uchungu baada ya mwanae kufa katika ajali hiyo na kupatikana kipande cha mwili tu. mwanae alikuwa akijulikana kwa jina maarufu la Kibwetere au Shukuru Hussein

1269506805_16.jpg

Kunasemekana kutokea vifo vingi... Hili ni jambo la kusikitisha, idadi ya waliokufa ikipatikana nitakufahamisheni
 
Bad news kwakweli asubuhi yote hii jamani. MUNGU tuepushe na janga hili. Poleni wote mlioathirika na ajali hii. Asante Invisible
 
Mmmh jamani mambo yameanza tena tulikuwa tumetulia kusikia hizi ajali
Kuna nini jamani ..? inaumiza sana
 
duh. Mungu atunusuru na haya masahibu. Naomba kuuliza: kwa nini serikali isifanye hiyo barabara kuwa 'double road'? barabara ni nyembamba na haitoi 'room' ya kuovateki na mengine yanayofanana na hayo. Nyingi ya Barabara za Tanzania zimekaa kijima jima na haziendani na kukidhi ongezeko la watu na magari.
 
ka rahisi vile! sasa mathaklani lori limelalia kipanya unafanyaje ni udogo wa barabara au bad driving
 
Taarifa ni kuwa daladala halikuwaka moto, liliwahiwa... Kwa sasa wanapunguza mafuta kwenye lori ili kuanza kunasua miili ya marehemu iliyonasa kwenye daladala ambalo limelaliwa na lori hilo.

Fire wapo eneo la tukio na polisi wanaendelea kutoa ushirikiano
 
Kama saa 1:40 nilipishana na gari la fire likienda pande za huko!
 
Duh.. hawa zimamoto wanatoka wapi?
Nadhani hawakuwa mbali, haiwezekani wawahi hivi kwenda Kibamba... Ajali imetokea nadhani dakika kama 50 zilizopita, lakini kwakuwa imehusisha gari la mafuta ni muhimu kwao kuwepo eneo la tukio haraka iwezekanavyo
 
Taarifa ni kuwa daladala halikuwaka moto, liliwahiwa... Kwa sasa wanapunguza mafuta kwenye lori ili kuanza kunasua miili ya marehemu iliyonasa kwenye daladala ambalo limelaliwa na lori hilo.

Fire wapo eneo la tukio na polisi wanaendelea kutoa ushirikiano

Majonzi
 
Nadhani hawakuwa mbali, haiwezekani wawahi hivi kwenda Kibamba... Ajali imetokea nadhani dakika kama 50 zilizopita, lakini kwakuwa imehusisha gari la mafuta ni muhimu kwao kuwepo eneo la tukio haraka iwezekanavyo

Nilipishana na gari la fire ubungo!
 
Kuna jamaa hapa ofisini ameiona hiyo wakati anapita eneo la tukio anasema hakuna mtu anaweza kutoka mzima. Kwa kawaidia daladala linabeba watu zaidi ya 30 hadi 40 mida na asubuhi - My GOD.
 
ni kweli kabisa kuna ajali mbaya sana kibamba. daladala lilikua limeanzia safari zake kibamba limekutana na zahma karibu na KKKT ; nskia hali ni mbaya yana na watu wengi wameharibiwa vibaya sana kiasi kwamba maiti nyingine zinatoka kwa vipandevipande!!!

walio kwenye tukio wanasema kibamba hawajaona kitu kama hicho labda miaka mingi iliyopita... kibaya zaidi ni kwamba basi limeanzia hapo kwahiyo wengi wa marehemu wametokea si mbali na tukio la ajali!!!

Ni very sad day kwa wakazi wa kiibamba
 
very sad...tutalia kwa ajili ya ajali mpaka lini?????
 
Nawapa pole waliopatwa na ajali hii.
Naona maajali yamezidi sana, sijui tutoe visingizio gani, labda ndiyo wakati wa mavuno ya shetani. na sasa nimeahirisha safari yangu wakati wa Pasaka. nitakaa home.
 
Ajali ya kusikitisha hapa kwetu kibamba leo asubuhi saa 12
Hiace namba T615 AJW linalojimuvuzisha kutoka Ubungo Kwenda Mlandizi limegongana Uso kwa uso na Scania Tanker lenye Diesel no T192ABP na kutumbukia mtaroni..scania imeandika (yarabi iwe salama) kwa macho yangu nimeona maiti zisizopungua saba kwenye hiace na scania imeilalia hiace kabisa yaani scania ino juu hiace ico chini hata kuokoa haiwezekani..na sidhani kama kuna mtu atakuwa amepona ila kwenye scania dereva na konda anaweza akawa amepona..
sikuwa na kamera ya kufotoa ningeweka picha

Mpaka natoka eneo la tukio saa 7:45 am watu wa uokoaji hawajafika
ila polisi wamedhibiti ulinzi vizuri sana
 
Watu wengi wanahofiwa kupoteza maisha katika ajali iliyotokea leo huko Kibamba nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam. Ajali hiyo imehusisha lori la mafuta ambalo limeangukia daladala aina ya Hiace na kuliponda kama chapati. kazi ya kuchomoa maiti inaendelea. Watu wamekuwa wakidoa miguu na mikono na vipande vingine vya mwili katika daladala hilo.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom