Ajali mbaya: Basi la Mohammed Trans laua na kujeruhi tena

Mungu awape ahuen majeruh na kuwatia nguvu na ujasiri wafiwa ktk kipind hiki kigumu
 
Hapana ndg yangu! Bus lilopata ajari lilikuwa linaelekea Mwanza nami nilikuwa mbele na basi lingine la kampuni hiyohiyo linaloenda Dar na kwa sasa niko Moro tutatoka asubuhi. Nasikitika sana kwa watu wenye mawazo mgando fikra fupi wanao husisha utoaji wa taarifa hii na maswala ya kiitikadi na imani za kidini. Huu ni umbumbumbu na ujinga wa kukemewa kwa mlalamikaji hajui mtoa taarifa anaamini ktk itikadi gani wala dini gani. Ujinga mtupu!

Duh, pole zao sana walioumia na kupoteza maisha!
 
Naona mmeandika kwa sababu ni Bus la Mwislaam. Lingelikuwa la Mudhungu, mngelikaa kimya.

Wagalatia bana, kaaazi kweli kweli.

Poleni Wafiwa na Majeruhi. Mungu awalaze mahali pema Waliotangulia mbele ya haki.

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...etaka-kuwekeza-usd-20-billion-tanzania-5.html

mdau unautia aibu uislam,,,,,hebu acha kutupaka matope wenzio bhana,kuna ajali ngapi za makampuni ya wakristo na huripotiwa,binafsi naona ni vizuri MOHAMED TRANS IKAFUtWA KABISA,NI MOJA YA KAMPUN ZINAZOPATA AJALI MARA KWA MARA,YAAN HATA HILI LA AJALI UNALETA SERA ZA KIDINI???ALLAH AKBAR,
USIJE UKASEMA NA ALIYESABABISHA AJALI ALIKUA ANA LENGO LA KIDIN
 
Bajabiri,

Nilikuwa nataka niwakate ngebe wale akina ZOMBA ambao hawachelewi kuja na maneno "Mnamuandama kwa sababu ni MUISLAAM. Nashukuru wewe umeliona hilo. Si lengo langu kuwatia aibu la hasha.
Ni kutaka kuonyesha jinsi baadhi yetu wanavyotumia DEAN kutetea uzembe unaofanyika nchi hii.

BTW: Mie ni MKRISTO.
mdau unautia aibu uislam,,,,,hebu acha kutupaka matope wenzio bhana,kuna ajali ngapi za makampuni ya wakristo na huripotiwa,binafsi naona ni vizuri MOHAMED TRANS IKAFUtWA KABISA,NI MOJA YA KAMPUN ZINAZOPATA AJALI MARA KWA MARA,YAAN HATA HILI LA AJALI UNALETA SERA ZA KIDINI???ALLAH AKBAR,
USIJE UKASEMA NA ALIYESABABISHA AJALI ALIKUA ANA LENGO LA KIDIN
 
Soma hapo juu na uwe UNAANGALIA habari katika 3D. Ndiyo nyie mnakuja kuumbuliwa kwa kutokuelewa ujumbe.
mnafiki kweli wewe huo udini na ujinga utakufikisha pabaya kwani si kafara huu mwezi tunaajua sana count ajali zote uone huu mwezi umetuulia ndugu wengi sana .
 
Katika hali ya kusikitisha leo alfajiri basi la mohammed trans limepata ajari mbaya maeneo ya karibu na mji wa bukoba mda mfupi baada ya kutoka stand kuu. Inasemekana basi hilo liligongana na lory aina ya tiper na kusababisha kifo cha dereva wa lory palepale na majeruhi wengi abiria wa basi hilo.

Haijajulikana ka kuna vifo zaidi kwani inasemekana majeruhi walikuwa wengi na hali zao zilikuwa mbaya. Tafdhari mwenye taarifa za karibuni aendelee kutujuza.

Nawasilisha kwa masikitiko makubwa.

Taarifa hizi za ajali hasa mara tu ajali inapotokea ni za muhimu, hii inawapa tahadhari watumiaji wengine wa barabara husika, ndugu na wale wanaoweza kutoa msaada wa haraka. Ni wazi kabisa kwamba vikosi vyetu vya uokoaji vimelala na ndio maana wahanga hupata msaada masaa mawili baada ya tukio na kadharika. Matumizi mazuri ya mitandao ya kijamii yanaweza kuokoa japo maisha ya mtu bila wewe kujua. Tusikatishwe tamaa na wenye mawazo tofauti na haya ndio mabadiliko yenyewe!
 
Khaaa! kumbe zomba ni mwalimu wa lugha! Ha ha ha haaaa! Yaan haumuachii tu? mwenzio anaandika anavyotamka. Muelewe tu ALARI = AJALI

Mkuu na wewe umekosea. Aliandika AJARI sio ALARI. Nimecheka na pia mikono ikawasha ili niandike kuwa na wewe umekosea.... Sina baya ila naifurahia JF kwa mambo meeengi. Mengine yanasikitisha, yanafurahisha, yanachekesha, yanatia hasira, yanahuzunisha, n.k... Najua wote mmekosea ku-type tu i hope na mie sijakosea neno lolote maana wataibuka walimu wengine weeengiii kama mie.... teh teh teh.....
 
Umeona eeh? Makosa mengi huwa ni ya uchapaji tu ila watu hung'ang'ania kama vile tuko kwenye mtihani wa lugha.
 
Umeona eeh? Makosa mengi huwa ni ya uchapaji tu ila watu hung'ang'ania kama vile tuko kwenye mtihani wa lugha.
Kweli kabisa. Ila umeniacha hoi uliposema 'ameandika anavotamka!', dah bado nacheka.....
 
Tena??
Too much sasa.
Watatumaliza hawa kwa makafara yao!!!

Acha imani zako potofu kila nafc itaonja umauti,kufa ni haki ya kila kiumbe chenye pumzi,mkiskia ajali eti kafara 2rudina kwa Mungu ilo ndo la muhimu.
 
Tunawapa pole wale wote
waliofikwa na matatizo hayo. Tunazidi kuwaombea majeruhi wapone haraka.
Tunawaomba wenye mawazo ya kafara na ushirikina washindwe na walegee.
kwa wale wote waliopoteza maisha, mwenyezi Mungu awalaze mahali pema
peponi. Amen.

Amina!naunga mkono hoja.
 
kweli kabisa. Ila umeniacha hoi uliposema 'ameandika anavotamka!', dah bado nacheka.....

unajua nini? Umenifanya na mie nicheke sana! Bana eeh, mie siandiki barua ya kiserikali hapa kwamba natakiwa nitumie kiswahili fasaha.
 
Back
Top Bottom