Ajali mbaya: Basi la Mohammed Trans laua na kujeruhi tena

Tiger One

JF-Expert Member
Apr 11, 2012
568
310
Katika hali ya kusikitisha leo alfajiri basi la mohammed trans limepata ajari mbaya maeneo ya karibu na mji wa bukoba mda mfupi baada ya kutoka stand kuu. Inasemekana basi hilo liligongana na lory aina ya tiper na kusababisha kifo cha dereva wa lory palepale na majeruhi wengi abiria wa basi hilo.

Haijajulikana ka kuna vifo zaidi kwani inasemekana majeruhi walikuwa wengi na hali zao zilikuwa mbaya. Tafdhari mwenye taarifa za karibuni aendelee kutujuza.

Nawasilisha kwa masikitiko makubwa.
 
Tunawapa pole wale wote waliofikwa na matatizo hayo. Tunazidi kuwaombea majeruhi wapone haraka. Tunawaomba wenye mawazo ya kafara na ushirikina washindwe na walegee. kwa wale wote waliopoteza maisha, mwenyezi Mungu awalaze mahali pema peponi. Amen.
 
Nchi hii ajali zote hizi zinatokana na RUSHWA. kwa sababu ya mdudu rushwa sheria zote za barabarani huwa hazifuatwi.
Trafiki polisi akipiga mkono anapewa buku mbili. ukiwa na mashtaka polisi unakunjua mkono siku inapita.

Kama ni kafara basi kafara hii inaitwa RUSHWA na haiwezi kuisha mpaka mfumo mzima kuanzia magogoni mpaka kwa VEO ubadilike.
 
Muwe mnasoma kila kitu na mkaelewa na siyo kusoma kama siyo Great Thinkers.

Nilitegemea mtakuwa mmenielewa ila naona mwataka kutafuniwa kila kitu.

Nimeweka hii LINK hapo chini na ukisoma ujumbe wa #85 by: Don Draper, utaelewa nilimaanisha nini.

Soma hapa na uunge na maneno yangu: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...etaka-kuwekeza-usd-20-billion-tanzania-5.html
Real? Haya ***** mtozeni mwingine atasema freemason, Lord have mercy!

Unapotaka kupost kitu humu tumia akili si mate!!!! ikishindikana endelea kusoma post za wengine kuliko kuandika ujinga kama huu kwenye red

Kumbe na wewe uko hivi...
 
Wewe nawe ni ajali sio "ajari".

Hapana ndg yangu! Bus lilopata ajari lilikuwa linaelekea Mwanza nami nilikuwa mbele na basi lingine la kampuni hiyohiyo linaloenda Dar na kwa sasa niko Moro tutatoka asubuhi. Nasikitika sana kwa watu wenye mawazo mgando fikra fupi wanao husisha utoaji wa taarifa hii na maswala ya kiitikadi na imani za kidini. Huu ni umbumbumbu na ujinga wa kukemewa kwa mlalamikaji hajui mtoa taarifa anaamini ktk itikadi gani wala dini gani. Ujinga mtupu!
 
Hapana ndg yangu! Bus lilopata ajari lilikuwa linaelekea Mwanza nami nilikuwa mbele na basi lingine la kampuni hiyohiyo linaloenda Dar na kwa sasa niko Moro tutatoka asubuhi. Nasikitika sana kwa watu wenye mawazo mgando fikra fupi wanao husisha utoaji wa taarifa hii na maswala ya kiitikadi na imani za kidini. Huu ni umbumbumbu na ujinga wa kukemewa kwa mlalamikaji hajui mtoa taarifa anaamini ktk itikadi gani wala dini gani. Ujinga mtupu!

Ajali. Hapana nini sasa.
 
Katika hali ya kusikitisha leo alfajiri basi la mohammed trans limepata ajari mbaya maeneo ya karibu na mji wa bukoba mda mfupi baada ya kutoka stand kuu.
Inasemekana basi hilo liligongana na lory aina ya tiper na kusababisha kifo cha dereva wa lory palepale na majeruhi wengi abiria wa basi hilo.
Haijajulikana ka kuna vifo zaidi kwani inasemekana majeruhi walikuwa wengi na hali zao zilikuwa mbaya.
Tafdhari mwenye taarifa za karibuni aendelee kutujuza.
Nawasilisha kwa masikitiko makubwa.

Mkuu, hivi imekuwaje - mbona kutoka stand unapanda mlima kwa takribani maili kama nne hivi kabla ya kufikia tambarare! Hapo sioni uwezekano wa Mohammed trans kwenda mwendo wa kasi, unless kama lory lilikuwa lina teremka mlima kwenda mjini lilipata matatizo ya brake na kuligonga Bus labda! Nimesikitishwa sana na ajali hiyo, sina shaka majeruhi wata hudumiwa ipasavyo, R.I.P dereva.
 
Back
Top Bottom