Ajali Kazini - Ushauri Tafadhali!

Keykey

JF-Expert Member
Dec 1, 2006
3,250
740
Mie na mmbongo mwenzangu tuko mji mmoja hapa Ghuba, shughuli yetu ni 'maboxi'. Tunaishi kwenye shared apartment, tupo wabongo 2, mhindi na mhabeshi.
Mwenzangu jana kapata 'ajali'. Hawa housemate wetu wanakula sana pilipili na ukali wake hauna kifani! Hata sie tumeizoea kwa kiasi fulani.

Jana jioni, jamaa yangu alikuwa zamu jikoni na wakati anakatakata viungo, akatoka mara moja kwenda haja ndogo nahuko katika kujisaidia akijishika sehemu-sehemu na ndipo balaa likamkuta! Basi pilipili zimemwasha akawa analia kama mtoto mdogo, jana chakula cha jioni hakula, alijaribu kuoga maji mengi haikusaidia, amejifungia chumbani kalala mtupu, amewasha feni na ac lakini nafuu haikupatikana.

Leo huku ni mwisho wa wiki na kazi ni nusu siku lakini jamaa mzigoni hakutokea.

Naomba ushauri kwa haya yafuatayo:
1. Huduma ya kwanza: ukipatwa na ajali kama hii, unafanyaje? sitashangaa na mie yakanifika!
2. Matibabu: Je, inawezekana kuwa atakuwa amepata madhara kiafya na kama ni hivyo yapo matibabu yake?
3. Insurance: Je, watu wa bima wana policy inyohusu ajali kama hizi? maanake mtu unaweza kupoteza kiungo muhimu maishani mwako!

NAWASILISHA.
 
Hii ilikuwa mchanganyiko wa pilipili za kihindi na wa-ethiopia, kuna namna wanafanya ukali unaluwa zaidi ya kawaida.

Dawa ya kukata pilipili ni bia tuu, waulize walevi wote watakuambia. Angemwagia bia hapo .. yaani pooa kabisa.
 
Dawa ya kukata pilipili ni bia tuu, waulize walevi wote watakuambia. Angemwagia bia hapo .. yaani pooa kabisa.

Hapa tulipo bia ni bidhaa adimu hata ya dawa unaweza usipate.

Nilimpeleka hospitali jana, amepata nafuu - muuguzi wa zamu ansema alimpa 'huduma ya kwanza' na leo ameenda nae nyumbani kwake kuendelea 'kumhudumia'.
 
Nadhani kama silaha yake isingekuwa na mkono wa shweta madhara yangekuwa madogo...mshauri atahiri.
 
Back
Top Bottom